Quruxbadan
JF-Expert Member
- Aug 12, 2013
- 232
- 80
Najua watu wengi mtanichukulia vibaya, kutokana na observation nliyofanya katika muda nliokuepo shuleni, nimeona kua hiki kipindi cha dini kinachokuepo kila ijumaa asubuhi hakifai kabisa kuepo, kinachochea udini na utengano baina ya wanafunzi. Wanafunzi wakiwa huko wanakua brain washed sana, Muislamu anafundishwa kua mkristo ni adui yake na mkirsto nafundishwa muislamu ni adui yake na anatakiwa ampige vita.hawa hawa ndo wanatakiwa wakae darasa moja na kushirikiana katika masomo mbalimbali. Hili si jambo geni ktk shule zetu za serikali. Ikumbukwe kua hawa vijana ndo taifa la kesho ikiwa watalelewa katika misingi ya kuchukiana je hapo baadae nchi yetu itakua katika hali gani??
Nawasilisha kwenu wadau
Nawasilisha kwenu wadau