Napenda wanawake wanaojisitiri kimavazi kuliko wa vimini na mawigi

chifusongea

Senior Member
Jan 8, 2016
164
152
Najua wengine watasema naishi enzi za ujima lakini kiukweli nikimwona binti kajisitiri nguo iliyofunika mwili vizuri, kichwani ana mtandio au kilemba huwa najihisi faraja kubwa sana moyoni.

Shida nikiona wale wa visuruali vya kuchanika, vimini na mawigi ya kichina huwa najihisi kutapika.
Sasa sijui ni ushamba wangu au kuna wanaume wengine hali kama hii huwakuta.

Nawakilisha.
 
hata mimi hivyo hivyo unaisi kutapika fulani ivi!viwigi,vimini,visuluali mieleni,mivipodozi,mipafyumu,milangi mdomoni na kwenye macho! ni shiiiiiiidddddddddddddaaaa! mke anaye faa hafai kuwa na hayo makolokolo! mke mwema yupo natural! sio kuforce maisha!
 
ukweli ni kwamba hayo ni maono au matakwa yako.... japo siku hizi mambo yamebadilika sana unaweza kuniona navaa ushungi 24/7 kumbe ni mchafu wa matendo kupindukia sifai afadhali yule avaae hizo nguo zisizojistiri ila lile vazi limenifanya kuonekana ni mwema na maovu yangu yamejificha nyuma yake.

hijab isn't just what you are wearing but its also what you do and say. its who you are
 
Najua wengine watasema naishi enzi za ujima lakini kiukweli nikimwona binti kajisitiri nguo iliyofunika mwili vizuri,kichwani ana mtandio au kilemba huwa najihisi faraja kubwa sana moyoni.
Shida nikiona wale wa visuruali vya kuchanika,vimini na mawigi ya kichina huwa najihisi kutapika.
Sasa sijui ni ushamba wangu au kuna wanaume wengine hali kama hii huwakuta.Nawakilisha.
Uko sawa kiongozi.... ndio maana kwenye swala kuoa, nita enda kugonga hodi kwenye familia za kiarabu!! Na nnaamini mpango wangu utatiki tu....
 
Najua wengine watasema naishi enzi za ujima lakini kiukweli nikimwona binti kajisitiri nguo iliyofunika mwili vizuri, kichwani ana mtandio au kilemba huwa najihisi faraja kubwa sana moyoni.

Shida nikiona wale wa visuruali vya kuchanika, vimini na mawigi ya kichina huwa najihisi kutapika.
Sasa sijui ni ushamba wangu au kuna wanaume wengine hali kama hii huwakuta.

Nawakilisha.
Nakuunga mkono, uvaaji huu inabidi uwe sheria.ningependa Magufuli na serikali yake waaende muongozo ya mavazi ya kiaamaadili.
 
Naona umefurahiii madame... ndio hiko hivyo napenda sana mabinti wa kislamu wanavyojistiri hususani waarabu japo kuna wengine ni vimeo..
mabinti kujisitir sio kwa waarabu tu dear hii ni lazima kujisitir kwa mwanamke wa kiislamu na ni wajibu ajistiri na ukiona mwanamke wa kiislam hajisitiri faham mawili either dini anaijua ameamua kua mpuuzaji tu au haelew chochote kuhusiana na dini yake.
 
Kweli kabisaa swala la kujistiri mwili ni la maana sana kwa mwisalamu. Nimewahi kuishi na waislamu(waswahili) kipindi kirefu tu mji mmoja na nimewahi kuwa na best friends ambao ni waarabu na kuwa nao karibu muda mrefu tu.... LAKINI TU NIKWAMBIE HIVI KWENYE SWALA LA MAVAZI KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA SHOMALI NA ABDALLAH...KUNA TOFAUTI KUBWA SANA KATI YA SHAJANI NA AISHA. YAANI KUNA HAO WENGINE UTAMUONA ANAVAA VIZURI SIKU YA IJUMAA TU MIDA YA SWALA IKIFIKA JIONI YUKO KWENYE PEDO KAMA KAWAIDA. Ndio maana ukaona kma nimespecify hivii hapo mwanzoni
 
Back
Top Bottom