Napenda sana kula pweza, ila wauza pweza wa Dar asilimia 99 ni Wachafu na wala hawajui usafi ni nini

Nahonyo

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
5,374
5,016
Nimekua mpenzi sana wa kula pweza, ila kula pweza Dar, kwa hawa wauzaji wetu barabarani, inataka uwe unafanana nao, usijue uchafu ni nini.

Unaona mtu amechagua mkia wa pweza, anaomba akatie vipande, jamaa anashika kwa mkono tu bila kunawa, akili ya kutumia uma, kushikia pweza anaekatwa hawana, mkono huo huo anashika pweza, anapokelea hela, anashikia stick anayojichokonolea kwenye meno.

Bakuli sasa ya kuwekea Supu, ni za plastick mpaka zimeingia rangi ya mchuzi wa pweza, jiulize maji wanayooshea baada ya mteja wa kwanza kuitumia, je vijiko vinanavyoingia ndani ya mdomo, wa kila mteja anekunywa supu, vinaoshwaje.

Ndugu zangu wauza pweza mjipende kwanza nyie ili muwapende wateja wenu pia, Pweza tunapenda ila.
 
Yapo maeneo baadhi ambayo wauzaji wamestaarabika usafi unazingatiwa at least.

Ila maeneo mengi hata mimi niliyoyaona wauzaji asilimia kubwa wako rough mno, nadhani hiyo inatokana na wateja wake alio watageti eneo hilo wengi wana falsafa za "we don't care"
 
Ni kweli kabisa, ila Sio wauza pweza tu...kwa Dsm wafanyabiashara wengi ni WACHAFU, hata mama Ntilie na watu wa magengeni pamoja na wauza miwa

Sio kama Wafanyabiashara wa Moshi na Arusha

Chukieni mpaka mpasuke, ninyi ni wachafu
 
Nakubaliana na wewe kabisa, hata mimi ni shabiki mkubwa wa nyama ya pweza na ngisi, na nikiwaona wakiuzwa barabarani huwa nawatamani sana, lakini nikisogea karibu na mazingira wanayouzia, na jinsi wanavyowekwa, kwa kweli hamu yote huniisha kabisa.

Nadhani hii sasa ni FURSA kwa wajasiriamali kwamba, kuna watu wengi wanatamani kula pweza, au ngisi hivyo wajiongeze, wajitokeze wawe wanafanya biashara hiyo katika mazingira mazuri, safi na salama.
 
Nimekua mpenzi sana wa kula pweza, ila kula pweza Dar, kwa hawa wauzaji wetu barabarani, inataka uwe unafanana nao, usijue uchafu ni nini.

Unaona mtu amechagua mkia wa pweza, anaomba akatie vipande, jamaa anashika kwa mkono tu bila kunawa, akili ya kutumia uma, kushikia pweza anaekatwa hawana, mkono huo huo anashika pweza, anapokelea hela, anashikia stick anayojichokonolea kwenye meno.

Bakuli sasa ya kuwekea Supu, ni za plastick mpaka zimeingia rangi ya mchuzi wa pweza, jiulize maji wanayooshea baada ya mteja wa kwanza kuitumia, je vijiko vinanavyoingia ndani ya mdomo, wa kila mteja anekunywa supu, vinaoshwaje.

Ndugu zangu wauza pweza mjipende kwanza nyie ili muwapende wateja wenu pia, Pweza tunapenda ila.
Nunua wabichi ukatengeneze mwenyewe ukiwa ndani ya apartment yako hapo mikocheni. Vitu vya kula barabarani vina ladha yake na hizo ndo ladha yake sasa!
 
Mikocheni ndipo wanapouza pweza au sijakielewa, mnachotakiwa kuelewa, mimi nimetoa maoni yangu juu ya bidhaa ni ipendayo ya pweza muhimu ni wao kujirekibisha, fedha inashikwa na watu wengi, na kila mtu ana namna ya kuntuza, sasa unatoka kushika fedha, alafu bila kunawa unatushikia pweza.
 
Hizo zinaitwa raha za uswahilini mkuu
 
8dafcf4d65ea85f42fbcebaa12cd59f7.jpg
 
Nunua wabichi ukatengeneze mwenyewe ukiwa ndani ya apartment yako hapo mikocheni. Vitu vya kula barabarani vina ladha yake na hizo ndo ladha yake sasa!
Yaan ladha ya pweza inaongezwa na ule uchafu uchafu wa muuzaji Mara kaingiza mkono kwenye suruali ndani kajikuna kidogo mara umechagua mkia anaushika na mkono ule ule aliojikuna kwenye suruali (ndani) alafu anakukatia na anakuwekea mchuzi na ndimu chumvi kidogo afu anakupa ule 😆 na wewe unakula
 
Nimekua mpenzi sana wa kula pweza, ila kula pweza Dar, kwa hawa wauzaji wetu barabarani, inataka uwe unafanana nao, usijue uchafu ni nini.

Unaona mtu amechagua mkia wa pweza, anaomba akatie vipande, jamaa anashika kwa mkono tu bila kunawa, akili ya kutumia uma, kushikia pweza anaekatwa hawana, mkono huo huo anashika pweza, anapokelea hela, anashikia stick anayojichokonolea kwenye meno.

Bakuli sasa ya kuwekea Supu, ni za plastick mpaka zimeingia rangi ya mchuzi wa pweza, jiulize maji wanayooshea baada ya mteja wa kwanza kuitumia, je vijiko vinanavyoingia ndani ya mdomo, wa kila mteja anekunywa supu, vinaoshwaje.

Ndugu zangu wauza pweza mjipende kwanza nyie ili muwapende wateja wenu pia, Pweza tunapenda ila.
Ni kweli. Walitakiwa wawe wanashika na uma wakati wanakata. Ikiwezekana watumie disposable cups kwenye kunywa. Ukiwa ni mtu mwenye kinyaa huwezi kula. Kuna wanaoweza kusema mtu atengeneze nyumbani lakini kuna inconvenience nyingi pia
 
Yaan ladha ya pweza inaongezwa na ule uchafu uchafu wa muuzaji Mara kaingiza mkono kwenye suruali ndani kajikuna kidogo mara umechagua mkia anaushika na mkono ule ule aliojikuna kwenye suruali (ndani) alafu anakukatia na anakuwekea mchuzi na ndimu chumvi kidogo afu anakupa ule 😆 na wewe unakula
Hahaha

Hiyo inaitwa yaliyomo yamo
 
Watanzania kiujumla wanapenda maeneo machafu,watu wengi waliofungua migahawa mizuri yenye mazingira masafi na mazuri wameishia kufunga biashara zao kwa kukosa wateja!! Ila ile migahawa michafu iliyopo kwenye mazingira machafu ndio watu wanajazana kupata huduma!! Watanzania wengi wanaamini sehemu nzuri ni kwa ajili ya wazungu na wageni wengine kutoka nje!! Mfano hayo majuice ya miwa, ukifungua ofisi nzuri ya kuuza juice ya miwa yenye mazingira safi na vifaa bora hakuna mtanzania atasogea hapo! labda kama ni diaspora au mzungu.
 
Unapajua pale kariakoo wanapouza supu ya mangozi ya Ng"ombe au bugiruni pale wanauza mapupu? Nenda saizi ukaone nyomi lake
 
Back
Top Bottom