Ningeshangaa sana kama haya yanayotokea yasingetokea, kila mtu wakati wa uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi aliona jinsi vigisufigisu zilivyotawala, tuliona wazi demokrasia ilivyoendeshwa, kati ya watu ambao walikuwa mstari wa mbele kuhakikishia wananchi kuwa CCM ndiyo chama pekee kinachofuata misingi ya utu na utawala bora Nape ni mmoja wapo.
Huwezi kabisa kumtenga Nape na ushindi wa CCM, Nape alisimama kidete na kuaminisha umma kuwa chaguo sahihi ni CCM. Sina uhakika kama kwenye Chama Cha Mapinduzi kuna kiongozi mwenye nguvu kama Nape, Nape anaijua CCM sana na alikuwa humo na uwezo wake unajulikana.
Hata sasa kama sio hizo nguvu alizo nazo naamini angeshatumbuliwa kwa kauli ya juzi kumlaani Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Sina uhakika kama kunakiongozi yeyote kwa sasa mwenye uwezo wa kulaani mteule wa rais, lakini Nape ameonyesha kuwa yeye sio kiongozi wa kutishwa au kubabaishwa.
Kwakuwa Nape ananguvu ushawishi wa kisiasa na uthubutu usiotetereka, namshauri atumie nguvu hizo iki kuhakikisha Tanzania haiendi mrama, ukiwa nje ya mfumo huu hutakuwa na fursa ya kusema au kukemea, kibaya zaidi hakutakuwa na mtu anayeweza kusema ukweli au kukemea na kulaani pale inapobidi, wengi ni waoga na wasingependa ugali wa watoto ukosekane.
Naamini haya mambo ni magumu ila kwa aina hii ya uongozi uliyopo dawa sio kususa au kuondoka kwenye mfumo, dawa ni kuhakikisha watanzania wanafuraha na nchi yao.