Nape: Siondoki CCM kwani nina hisa nyingi sana; siogopi wakubwa kama kuchukia na wachukie nimejitoa maisha yangu

Angelisema maneno haya bungeni spika wa bunge angelipatia ufumbuzi, lakini anasema haya maneno kwa wananchi wakiwa hawawezi kufanya lolote.
Kwa nchi yenye demokrasia ya kweli hapo ndipo mahali sahihi pa kusemea. Hao ndiyo waajiri wake.

Ila wacha kijana naye apate wakati mgumu; huwezi shinda vita within ni heri ubakie kimya.
 
Mkuu wewe utakua team jiwe
By the way kila mtu hata ww ungekuwa yeye ungekua hivo hivo njaa
Unafikiri mimi ni kijana si ndiyo? Mimi hata siku moja tangu vyama vingi vinaanzishwa sijawahi kuwa na timu sasa wewe unanijaza maneno kwa mtazamo wako huyo Nape si ndiyo mwasisi wa goli la mkono na ndiyo mwasisi wa kuzuia bunge live sasa tumuiteje kama siyo njaa za kunyimwa ulaji
 
Mungu amjaalie Nape Nnauye katika safari yake ndefu katika ulingo wa siasa,mabonde na mwitu makorongo ya kutisha na wanyama wakali vyote vinamsubiri,ila chama imara kitamvusha wala askonde.
 
Ukokotozi wa Siasa ni muhimu katika kutoa maamuzi, lakini maslahi mapana ya Taifa ni muhimu zaidi.
====
TUJITEGEMEE.
 
Amesahau kuwa kusema ukweli kwenyewe ukiwa CCM ndiyokujiondoa kwenyewe ndani ya CCM?, amesahau kuwa mpigania haki ndani ya CCM ni adui wa CCM na hatakiwi kuwepo ccm?,amesahau kuwa msema ukweli ni mpenzi wa Mungu na siyo mpenzi wa CCM kwa kuwa CCM inachuki na wapinzani wanaoikosoa CCM pamoja na kushangilia pale raia wanapotekwa na kupotezwa na watu wasiojulikana ikiwa ni pamoja na kupora matakwa ya wananchi ya kujichagulia kiongozi anayefaa na kuwalazimisha kuongozwa na kiongozi ambaye alikataliwa na wananchi kwa njia ya kura ilimradia awe ni mwenye rangi ya kijani?.
 
Mbunge wa mtama, Nape Nnauye aliongea na wananchi wake jana wa jimbo la Mtama ambapo aliongea kwa hisia kali kuhusu Serikali kuweka sheria mpya ya ushuru wa korosho ambao utaenda Serikali Kuu wote tofauti na zamani ambapo ulikuwa ukibaki kwa wakulima kwa asilimia kubwa.

Nape amesema Serikali imefanya sivyo kwa kuwa ushuru wa korosho umeongezeka na wakaamua kukwapua hizo hela bila kuwa na sababu ya msingi.

Nape aliendelea kusema kuwa Serikali inasema hela zinaibiwa lakini wanashindwa kuthibitisha zinaibiwaje na wala kuwakamata hao wezi.

Ameendelea kusema yeye atawatetea wananchi na haogopi wakubwa kama kuchukia na wachukie na amejitolea maisha yake kusema ukweli daima kwani CCM ni ukweli daima. Nape amesema ataendelea kufuatilia jambo hilo na kusisitiza kuwa kuteleza si kuanguka.

Aidha Nape Nnauye amesema hawezi kukihama chama hicho tawala kwa kuwa ana hisa nyingi. Amewataka wananchi kuondoa hofu juu yake akiwataka kupuuza maneno yanayosema kuhusu hatima yake CCM, kusisitiza kuwa hataondoka katika chama hicho.

“Nimechaguliwa kuwatumikia wananchi wa Mtama. Yapo maneno mengi yanazungumzwa, hasa kuhusu hatima ya mbunge wenu. Tusipate shida kwenye chama changu cha kijani,” amesema Nape.

“Nina hisa nyingi najua mmenielewa, furaha yangu ni kuwatumikia hayo mengine ni bla bla tu.”


Kiufupi Nape anatapatapa na sio anatapa tapa pasipokujuwa anafanya nini ila namuonea huruma maana wanaokijuwa chama wanamsikilizia nakuona kulikuwa na makosa kumpa nafasi kubwa za chama a leo ankisumbuwa chama. Kiufupi anako elekea nikutenda dhambi ambayo haisameheki nadhani mnanielewa. Wazee kwa muda tofauti wamesha muhusia atulie na asiongee ila bado anawashwa washwa ila muwasho huu anawashwa atakuta ana dil na mtu sie watu wanajuwa Rais anafanya kazi watanikubalia Nape anagusa sharubu za wenye nchi akifikiri atakuwa salama. Hakuna atakaye deal na yeye kwa bunduki au silaha ila this time atajiukumu mwenyewe kwa dhambi zake Mwenyewe. Hana uwekezaji kama wa akina Lowasa wala hana influence ktk chama inasumbuwa watu. Mm namuonea huruma kiukaeli kabisa. Yajayo yanafurahisha.
 
Ila hata asipopitishwa ATASUMBUA sana, na kwa kuwa JIWE lina huluka ya kutengeneza kesi likikushindwa ndo yanakukuta ya LISSU

Yani naonaga Watu wapumbavu lakini we unaongoza. Hivi kwa akili yako huyo jiwe wako angetaka roho ya huyo L ndo mission ile iwe ya kitoto hivyo. Do you really know the essence of p’s power. Please go to kindergarten and advertise your „intellectual poverty.“
 
Yani naonaga Watu wapumbavu lakini we unaongoza. Hivi kwa akili yako huyo jiwe wako angetaka roho ya huyo L ndo mission ile iwe ya kitoto hivyo. Do you really know the essence of p’s power. Please go to kindergarten and advertise your „intellectual poverty.“
JIWE akili yake ni ndogo, ndio maana Mission zake zote anazopanga zinabumbulika, linabaki linaona aibu tu halijui cha kufanya:

1. Kupanga yeye na Makonda eti walazimishe kurusha kipindi SHILAWADU cha kumdhalilisha GWAJIMA

2. Kupanga mauaji ya Lissu, mwishowe hajafa. Kapigwa risasi eneo lenye ulinzi mkali wa polisi na CCTV, eti siku ya tukio polisi wanaambiwa wasiwepo. CCTV baada ya tukio zinaondolewa na KALEMANI -Waziri wa Nishati na Mrithi wa Jimbo la Jiwe, mpaka leo hakuna hata DOTI LA UPELELEZI wa POLISI. Na kama haitoshi JIWE lilishamkamata na kumtishia maisha zaidi ya 6, leo kwa roho mbayaa hata wabunge wenzake wa CCM limewakaza wasiende kumwona.

3. Kununua WAPINZANI - Akili ndogooo
 
Nape amechanganyikiwa tu.Hata Lowassa aliapa hatatoka ccm,mwisho wa siku aliondoka tu,huyo Napelepe ni mtu mdogo sana kutunishia misuli chama chetu.Hii cancer tunailea wenyewe ilipofikia ni kutwaa kadi yetu tu,tuone atabwabwaja wapi
 
Mwigulu baada ya kufurushwa kwenye uwaziri mbiombio alikimbilia jimboni kwake kuongea na wananchi wajimboni kwake, Nape naye na viongozi wengine waliovuliwa madaraka yao walikimbia harakaharaka kufanya mikutano na wapiga kura wao na wote wanatoa maneno yanayofanana kwa kiasi Fulani.

Mara hii nayo siku zote Nape hajawahi kuitisha mkutano na wapiga kura wake, lakini baada ya kupigwa mkwara na mh Rais kati ya wale wa wabunge 17 wa Lindi na Mtwara amekimbia harakaharaka kwenda kuongea na wapiga kura wake,wangekuwa wapinzani wamefanya haya wanayofanya wabunge wa CCM wangeshitakiwa kwa makosa ya uchochezi lakini kwa vile ni wa CCM wako sahihi wakati hiyo inaweza kuwa ni njia ya kumchonganisha Magufuli na wapiga kura.
 
Nape anajua kabisa nje ya CCM hana maisha kwani bila ccm hakuna mtu ambaye angemjua mwanzoni alikuwa anatembelea nyota ya baba yake ila sasa hivi ndio anataka kupotea kabisa ajifunze kutii wakubwa
 
Back
Top Bottom