Nape Nnauye: Upinzani unaweza kuingia ikulu

Nape Nnauye: Upinzani unaweza kuingia ikulu

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
Katika hali isiyotegemewa na wengi ndgu. Nape Nnauye amekiri ya kuwa kwa hali ilivyo sasa WAPINZANI wananafasi kubwa ya kuingia ikulu.
Hii ni kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM na huku upinzani ukijipenyeza hadi vijijini.
Pia aliongeza ya kwamba MAFISADI NA KUNDI LAO ndani ya chama wanamchukia kutokana na misimamo yake dhidi ya Mafisadi.

Habari zaidi. Dira ya Mtanzania.

Kwa hali ilivyo kusini mwa nchi CCM wamesoma alama za majira.
Huwezi kumfanya mtu mjinga milele.
 
Wacha amalize sarakasi zote lakini sisi tunamuelewa kuwa ni product ya hao anaowaita mafisadi, na hata fedha anayotumia kila siku kutukana CHADEMA inatoka kwa mafisadi hao hao, yeye na wao tumeshawaweka kwenye kapu moja.
 
Jamani mbona hamuhoji source ya hii habari?
 
Haeleweki, kuhamia CHADEMA anaogopa, Kubaki CCM hana imani nayo, ndo hivyo dogo
 
Katika hali isiyotegemewa na wengi ndgu. Nape Nnauye amekiri ya kuwa kwa hali ilivyo sasa WAPINZANI wananafasi kubwa ya kuingia ikulu.
Hii ni kutokana na mambo yalivyo ndani ya ccm na huku upinzani ukijipenyeza hadi vijijini.
Pia aliongeza ya kwamba MAFISADI NA KUNDI LAO ndani ya chama wanamchukia kutokana na misimamo yake dhidi ya Mafisadi.
Habari zaidi. Dira ya Mtanzania.

Kwa hali ilivyo kusini mwa nchi ccm wamesoma alama za majira.
Huwezi kumfanya mtu mjinga milele.
Huyu jamaa amezidi UKIGEU GEU, mara wapinzani watasambaratika, mara wataingia Ikulu, mara sekretariat mupya chini ya Kiboko ya TEMBO na FARU itaingiza ccm Ikulu, sijui kesho ataibuka na nini!!!

Isijekuwa hajapata POSHO siku nyingi kaamua kutoa hii kauli kuwa BLACKMAIL viongozi wake wampe Per Diems za kwenda mkoani kujifanya anaenda kusawazisha mambo. Hawa watu wanaoishi kiujanja ujanja chunga sana, wanamanipulate mambo ili wapate fursa za kula hela.
 
Nadhani kuna uzi ulibandikwa humu juu ya issue ya yeye kufukuzwa kabla ya 2014, yawezekana ameisha nusa harufu so kaanza kutubu na kujitakasa, shida yangu ni hii, nani atampokea huyu? CHADEMA waliisha wahi kumkataa huyu dogo, madongo mengi anayotupaga kwao ni hasira pia alizonazo kwao CHADEMA.
 
Huyu si ndiye majuzi tu alileta uzi hapa kwamba UPINZANI ulipoteza nafasi ya kuingia IKULU 2010, kwasababu CCM walikuwa hakujipanga. Lakini 2015 UPINZANI usahau kabisa kwasababu CCM imejipanga.
 
Unauliza source?mbona aliri hilo hata alipokuwa anahojiwa kwenye mkasi juz kati?jamaa kesha kubali msemo wa wahenga"unaweza kudanganya kila siku lakini huwezi kumdanganya kila mtu kila siku".
 
Kwa yeyote anayefualia upepo wa kisiasa kwa sasa anajua kabisa kuwa magamba maji yapo shingoni, kwani imefika mahali magamba wenyewe mmoja baada ya mwingine wataanza kukiri kuwa njià ni nyeupe kwa CDM kuingia Ikulu mwakà 2015!!
 
Back
Top Bottom