Kupigana kwa vijana ndani ya uvccm ni mapito tu, hata enzi ya za mzee nnauye waliwahi kuchapana viboko ndani ya uvccm.
-Hapo baadaye nchi kuongozwa na vyama vingine inawezekana, ila kwa trend ya vyama vya sasa upinzani bado sana hakuna mwenye nafasi kwa miaka 50 ijayo hakuna upinzani wa ukweli,may be kije chama kingine cha upinzani baadaye sana.
Nape asema jambo lilonishangaza sana kwenye kipindi cha mikasi baada ya kunogewa kusafishwa miguu na kusema hakuna chama cha upinzani nchini kinachowanyima wao kama ccm usingizi, wakati anatambua kabisa namna wanavyo kiogopa chadema
anadai lema kashinda arusha kwa sababu ya popularity ya watu wa arusha wanamenda lakini hakuna alilolifanya zaidi ya maandamano ila anasema wakifanya uchaguzi sasa hivi watashinda asubuhi kweupe. Kweli chali anaota ndoto za mchana.
Atanichafulia siku yangu! But anyway, itakuwa imeshakuwa late nitaenda kulala. Unajua ningeweza angalia chanel nyingine lakini ile tu kuelewa jamaa yuko EATV ni tosha kunichafulia siku!!
Muraaaaaaaaaaaaaaaaaa huyu Nape Nauye kaniacha hoi muraaaaaaaaaaaaaa,eti upinzani wanaweza kuchukua nchi ila sio hawa wa sasa"mantiki ya hoja hajazingatiwa hapa" .Halafu muraaaaaaaaaaaa anasema eti angekuwa mgombea ubungo angeshinda ubunge poti!!!!!!!!!!.
Siku ya jumatatu usiku katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesikika ktk kipindi cha mkasi akidai kuwa 'HATA UCHAGUZI UKIITISHWA KESHO ARUSHA CCM itampiga Godbless Lema kwa kura nyingi asubuhi asubuhi.
Napenda kumwambia Nape kuwa Lema hakushinda Arusha kwa chaguo lao bovu ila Lema ameshinda na Hata wangemleta JK angepigwa chini kwa aibu.
NAPE kuing'oa CHADEMA Arusha ni ndoto za mchana hata kama hatafanya kitu kwa miaka mitano ijayo.NAPE wakati mwingine unajidhalilisha kwa kuwadanganya waelewa na SIASA RAHISI ZA MWAKA 47.