Nape Nnauye jipe moyo, macho mbele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye jipe moyo, macho mbele

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by andrews, May 30, 2012.

 1. a

  andrews JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape Nnauye jipe moyo, macho mbele…

 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Habari kama hii Nape huwa anazikimbia kwa sababu yeye hataki kuambiwa ukweli. Anataka mipasho na kufarijiana!
   
 3. a

  andrews JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KUNA UWEZEKANO MKUBWA CCM IKAWA CHANZO CHA KUCHOMWA MAKANISA ILI KUWAGAWA WATANZANIA,WALIANZA KWA KUWAPAKA MATOPE CUF BAADA YA KUUNGANA NAO WAKAHAMIA CHADEMA ETI UDINI WAKASHINDWA SASA UKASKAZINI NINA WASIWASI KUNA MKONO WA CCM:israel:
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Nape hajui ya jana wala leo,amekulia raha ndo maana walomtuma huyu mtoto wa kigogo akaiue ccm wanajivunia pamoja nae mOU yao kufanhkiwa.nape amekulia maisha ya kitajiri na sasa anazivuna huku watanzania wakila mchicha pori.
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,674
  Trophy Points: 280
  MWALIMU Evarist Lukiko alinifundisha mwaka 1985 somo la Kiingereza. Alikuwa mwalimu mzuri sana wa somo hilo na mimi ni mmoja wa wanafunzi aliowapenda sana kwa kuwa nilikuwa naelewa haraka sana somo lake. Alikuwa ni mwalimu mcheshi sana lakini makini sana kwenye kazi yake na hakusita kumwadhibu mwanafunzi pale alipobaini katenda makosa. Kilichofanya nimkumbuke leo ni maneno yake aliyoyatumia kabla ya kumwadhibu mwanafunzi.
  Kwanza hakupenda kabisa kumchapa mtoto kwenye viganja ama sehemu nyinginezo. Alipenda sana kumchapa mwanafunzi makalioni. Kabla ya kuchapa alimwita mwanafunzi mhusika mbele ya darasa na kumsimamisha akiwa ameegemea dawati la mwalimu. Kisha alimwambia maneno yafuatayo kwa kumtaja mwanafunzi kwa jina lake. Kwa mfano angeweza kusema, "Mkama, jipe moyo, macho mbele, tega ‘makalio' tusahihishe makosa."
  Mwalimu Lukiko alituambia kwamba yeye aliamini kwamba mtoto anayekosa nidhamu, anayeshindwa kufuata sheria za shule, asiyezingatia masomo, nk, mara nyingi utakuta akili zimekimbilia ‘makalioni' na akazikalia na kuacha kichwa kikiwa kitupu! Na kwamba ndiyo maana yeye alipenda sana kutuchapa makalioni ili akili zikimbie huko na kurejea kichwani na kumfanya mwanafunzi awe mwanafunzi kweli mwenye nidhamu, mwenye uwezo wa darasani, mwenye busara, na kadhalika.
  Lakini ilikuwa inauma sana wakati wa kuadhibiwa, wakati wa kuchapwa. Alikuwa na fimbo kali sana zinazouma mno. Ulikuwa ukiwadia wakati wa kuchapwa, anayetakiwa kuchapwa aliumia, alitokwa machozi kabla ya kuchapwa na kwa kweli aliwaza sana kabla ya kutega ‘makalio'. Hali iliyokuwa ikimkuta mtu anayetakiwa kuchapwa ndiyo ninayoiona ikiwakumba ndugu zetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) hususan rafiki yangu Nape Nnauye. Huyu ni rafiki yangu na kwa kiasi fulani nampenda huyu jamaa! Na hasa kilichonifanya nikampenda ni uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki.
  Kabla ya kampeni za uchaguzi ule nilimsikia Nape akitamba kwenye vyombo vya habari kwamba CCM itashinda uchaguzi huo kwa kishindo. Akatoa wito kwa CHADEMA tena akisema alikuwa anaomba kila kukicha ili CHADEMA katika uchaguzi huo wamsimamishe Dk. Slaa na CCM wamshinde na kumshusha hadhi kisiasa na hatimaye ashindwe kugombea urais mwaka 2015. Nikamweleza Nape kwamba CHADEMA itashinda uchaguzi ule na kwamba kumsimamisha Slaa ni sawa na kuua mbu kwa tofali na uharibifu wa rasilimali fedha na rasilimali watu. Tulimsimamisha ‘dogo janja' na kushinda kwa kishindo. Kilichonifurahisha kwa Nape ni jinsi alivyokubali matokeo haraka!
  Kihistoria, Nape ni mmoja wa wanamtandao wa moja ya mitandao midogo iliyotokana na kuvunjika ama kuparaganyika kwa mtandao mkuu uliomwingiza Kikwete madarakani. Mtandao wa Nape ni ule unaoongozwa na Samuel Sitta unaoitwa: "wapiganaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama cha mafisadi". Kuna taarifa nyingi zimedai na kina Nape wamekuwa wakikanusha kijuujuu tuhuma za kwamba walipoona wamezidiwa na mtandao wa wenzao walihofia kwamba wanaweza wasipate nafasi ya kugombea ubunge kupitia ‘chama cha mafisadi'. Walichokifanya kama tulivyoelezwa na aliyekuwa mwenzao ndugu yetu na mpiganaji maarufu kwa leo Kamanda Fred Mpendazoe, walianza mkakati wa kuanzisha CCJ ili baadaye wang'atuke na CCJ nzima na kujiunga na CHADEMA ili kukipa nguvu ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2010.
  Ukipima maelezo ya Mpendazoe na majibu ya Nape na rafiki yake Sitta, kama una akili timamu utakuwa na kila sababu ya kukubaliana na Mpendazoe. Na kama tukiamua kukubaliana na Mpendazoe japo kwa sasa, basi Mpendazoe anasema pale Sitta alipohakikishiwa kurudi kwenye ubunge na uspika na mkuu wa kaya na Nape akaahidiwa na mkuu huyo kumpa angalau ukuu wa wilaya, wakageuka na kuamua kubaki ndani ya chama hicho. Baadaye wakaja kufanya mkakati wa kumwaminisha mkuu wa kaya kwamba ule mtandao mwingine mdogo ambao wao waliuita wa mafisadi, ndio unaokikosesha chama hicho mvuto na imani kwa wananchi. Mkuu wao kwa umahiri wa ‘usanii' akaiita hali hiyo sawa na chama kuvaa gamba. Akatangaza kukivua chama gamba akimaanisha kuwatimua toka kwenye nyadhifa zao wale wote walioitwa na akina Nape mafisadi.
  Wakati akitangaza mkakati huo alishachukua baadhi ya wanamtandao wa wapiganaji ‘feki' dhidi ya ufisadi na kuwaingiza kwenye serikali yake mfano kwa kuwapa uwaziri Sitta, Mwakyembe, Nyalandu na Nape (ukuu wa wilaya).
  Baada ya kutangaza kuvua gamba akaamua kutimua sekretarieti yote ya chama na kubadilisha baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Katika mageuzi hayo ndipo alipomteua Nape na vijana wenzake kuongoza sekretarieti ya chama. Ninachotaka kukieleza hapa ni kwamba Nape aliingia na matumaini makubwa sana kwenye uongozi wa chama. Alitangaza kwa nguvu sana kuvuliwa kwa magamba akiwa anawataja kabisa majina kina Lowassa, Chenge na Rostam Aziz kama ndio magamba. Kitu kimoja ambacho hakukitambua ni kwamba mkuu wa kaya hakukutana barabarani na hao aliowaita magamba na kwamba falsafa ya kuvua gamba ilikuwa danganya toto.
  Baada ya muda alijikuta kuvua gamba kunashindikana na akalazimika kula matapishi yake kwa kuruka kauli zake mbele za waandishi wa habari akidai eti hajawahi kutaja majina.
  Lakini ni kalamu hii hii ya Mwigamba iliyomtabiria kifo cha kisiasa Nape wakati akiwa busy kutangaza kuvua gamba. Kama ana kumbukumbu atakumbuka nilimwandikia makala nzima hapa kwenye huu ukurasa huu na kumwambia kwamba naliona jeneza lake la kisiasa muda si mrefu.
  Nikamtahadharisha kwamba kama anataka kubaki na heshima kidogo ambayo alikuwa amekwishajijengea, aiage CCM na kujiunga na CHADEMA kwa vijana wenzake kina Zitto, kina Mnyika, nk. Nikamkumbusha jinsi alivyomuita Lowassa fisadi kwenye mradi wa jengo jipya la UVCCM makao makuu na hatimaye akaukosa uenyekiti wa jumuia hiyo na kutimliwa kabisa uanachama wa jumuia hiyo. Hakunielewa!
  Lakini baadaye alijikuta anabadilisha mwelekeo na kuachana kabisa na agenda ya kuvua gamba na kuwatimua mafisadi ndani ya chama.
  Siku hizi haisemi kabisa! Nape alikuwa ameingia na mkakati kwamba wakishatimua wale waliowaita mafisadi, Watanzania watakiona chama kimekuwa safi na hatimaye watakipenda na mwaka 2015 kitarudi madarakani na mmoja kati ya ‘mabest' zake (anaweza kuwa Sitta, ama Mwandosya, ama Membe, nk) atakuwa rais naye atauonja uwaziri na labda na yeye afanye fanye usanii na baadaye aje kuwa rais. Hakujua kilichokuwa kinamngoja wala hakutaka kuusoma vizuri unabii wa kalamu hii.
  Amekwama! Na amekwama kwa sababu moja amekuja kugundua kwamba wenzake hasa mkuu wa kaya hawana nia ya kuvua gamba. Inasemekana wakati fulani aliwahi kuwatonya marafiki zake wa karibu kwamba NEC isipoamua kwa dhati kuwavua gamba mafisadi, angejiuzulu.
  Lakini mimi nilisema hakuna Mwana CCM huo ujasiri na kweli alishindwa kujiuzulu. Mbali na hilo kalamu kama hii ya Mwigamba zilijitahidi sana kuwaelimisha wadanganyika kwamba wasidanganyike kwa kuwa chama hicho cha zamani ni cha mafisadi watupu. Niliwahi kusema hata mitume kumi na wawili wa vita feki dhidi ya ufisadi nao ni mafisadi. Mambo yamemwendea kombo rafiki yangu Nape.
  Baada ya kukwama akabadili stahili. Sasa akawa ni mtu wa kukishambulia CHADEMA muda wote akisaidiana na makada wake wengine.
  Na hapo sasa ndipo akazidi kujichongea jeneza la kisiasa. Kitendo cha kulishambulia ‘tumaini jipya' la watanzania kwa sasa, hakiwezi kueleweka mbele ya Watanzania hao hao! Kwa hiyo kwa muda sasa rafiki yangu huyu amejikuta akikinga mafuriko kwa mikono. Kadiri anavyojitahidi kupambana na CHADEMA ndivyo chama hicho kinavyozidi kupaa!
  Nikiwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha najivunia sana moto wa M4C. Mwenyekiti wetu wa taifa akiwa Arusha wakati kabla ya kuanza kampeni za Arumeru Mashariki, aliamua kukaa nasi uongozi wa mkoa na kutengeneza mkakati wa kuwahusisha wanachama na Watanzania kwa ujumla katika kukiendesha chama na hatimaye kushinda uchaguzi ule mdogo. Tukakubaliana kwamba wananchi ndio wakichangie chama fedha na ndio washiriki kampeni kwa sehemu kubwa.
  Lakini katika kuwaza tukafiria kwa nini kile tunachokibuni kisiwe cha kitaifa. Kwamba uwe ni mkakati wa kushinda uchaguzi wa Arumeru na ule mkuu wa 2015. Kwamba kuanzia sasa chama kiende na huo mkakati hadi ushindi wa 2015. Mwenyekiti akashauri ‘slogan' ambayo ilikuwa tayari imeshabuniwa na chama mapema. M4C – Movement for Change. Tukakubaliana na kuizindua kwa ajili ya Arumeru hapa hapa Arusha.
  Wakati chama kinaelekea kuuzindua rasmi mkakati huo kitaifa jijini Dar es Salaam, sisi Arusha tena tukaamua kuuhuisha na kuupa nguvu. Tukabuni operesheni ambayo itakuwa mkono wa kuume wa mkakati wetu wa M4C. Tukaja na Operesheni "Vua Gamba, Vaa Gwanda". Tukaitekeleza kwa mafanikio makubwa sana hapa Arusha na hatimaye ikaanza kushika kasi mikoa mingine. Ni matamanio ya vijana wetu wa BAVICHA mkoa wa Arusha chini ya Kamanda, Ephata Nanyaro, kwamba hivi karibuni wana Arusha tupandishe bendera ya CHADEMA yenye nembo ya M4C mpaka kileleni mwa Mlima Kilimanjaro pale ilipo bendera ya taifa. Na hiyo iwe ni alama kwamba M4C isambae nchi nzima na kuleta mapinduzi makubwa. Naamini na ninawaombea vijana wetu waufanikishe mkakati huo na nimewaahidi kwamba mimi kamanda wao nitakuwa nao hadi kileleni.
  M4C imezinduliwa rasmi Jangwani kwa kishindo. Kishindo ambacho kwa kweli kinamuumiza sana rafiki yangu Nape. Amekuwa aking'aka kwamba wanaovua gamba na kuvaa gwanda ni makapi toka kwenye chama chake na kwamba wanashukuru kwa kuwa walikuwa mzigo. Lakini nimemwona wakati M4C inazinduliwa Jangwani yeye alikuwa mkoani Kagera na kwa namna ya kuweweseka akasema hata kama atabaki yeye mwenyewe kwenye chama chake, eti hakitakufa. Akasahau kwamba ukishasema chama unazungumzia kikundi cha watu kuanzia angalau wawili. Sasa sijui atakuwaje mmoja halafu mmoja huyo awe chama. Muhimu ni kwamba anaweweseka na anaona kabisa kuna hatari watu wakaisha ndani ya CCM akabaki yeye na wapiganaji wenzake feki dhidi ya ufisadi. Lakini kuonyesha kuweweseka zaidi, nilimshuhudia Nape akidai eti yeye sasa anazindua "Vua Gwanda, Vaa Uzalendo". Nashangaa wale wale aliowakataa walipovua gamba na kuvaa gwanda, leo anatakata wavue gwanda na kuvaa uzalendo. Wakivaa uzalendo watakuwa wanachama wa chama gani? Maana uzalendo unapatikana kwenye gwanda na si kwenye gamba.
  Leo nina neno moja tu kwa Nape. Naamini ningemuuliza Mwalimu Lukiko angesema Nape na wenzake walishahamishia akili zao tumboni na kuacha vichwa vitupu. Na kwa hiyo wanahitaji kuchapwa matumboni ili akili zirudi kichwani, warejee kuwa watu wanaofikiri kwa kutumia vichwa na siyo matumbo kama alivyowahi kutamka ‘mtume' Samuel Sitta. Ndiyo maana nadiriki kumwambia, "Nape Nnauye, jipe moyo macho mbele, tega tumbo tusahihishe makosa!"
  Inauma rafiki yangu Nape, kwa juhudi kubwa unazofanya kuihujumu CHADEMA halafu unashuhudia utitiri ule wa Jangwani Jumamosi iliyopita! Hapana hata ningelikuwa mimi ningeweweseka. Lakini ndiyo hivyo, tega tumbo tusahihishe makosa ndugu yangu. Tukishasahihisha makosa mkaanza kusikia matangazo BBC yakitaja, "Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CCM…" Mtashangaa.
  Kwa makamanda wote, mbele kwa mbele mpaka kieleweke!
   
 6. V

  Vancomycin Senior Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Samson Mwigamba

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MWALIMU Evarist Lukiko alinifundisha mwaka 1985 somo la Kiingereza. Alikuwa mwalimu mzuri sana wa somo hilo na mimi ni mmoja wa wanafunzi aliowapenda sana kwa kuwa nilikuwa naelewa haraka sana somo lake. Alikuwa ni mwalimu mcheshi sana lakini makini sana kwenye kazi yake na hakusita kumwadhibu mwanafunzi pale alipobaini katenda makosa. Kilichofanya nimkumbuke leo ni maneno yake aliyoyatumia kabla ya kumwadhibu mwanafunzi.

  Kwanza hakupenda kabisa kumchapa mtoto kwenye viganja ama sehemu nyinginezo. Alipenda sana kumchapa mwanafunzi makalioni. Kabla ya kuchapa alimwita mwanafunzi mhusika mbele ya darasa na kumsimamisha akiwa ameegemea dawati la mwalimu. Kisha alimwambia maneno yafuatayo kwa kumtaja mwanafunzi kwa jina lake. Kwa mfano angeweza kusema, “Mkama, jipe moyo, macho mbele, tega ‘makalio’ tusahihishe makosa.”

  Mwalimu Lukiko alituambia kwamba yeye aliamini kwamba mtoto anayekosa nidhamu, anayeshindwa kufuata sheria za shule, asiyezingatia masomo, nk, mara nyingi utakuta akili zimekimbilia ‘makalioni’ na akazikalia na kuacha kichwa kikiwa kitupu! Na kwamba ndiyo maana yeye alipenda sana kutuchapa makalioni ili akili zikimbie huko na kurejea kichwani na kumfanya mwanafunzi awe mwanafunzi kweli mwenye nidhamu, mwenye uwezo wa darasani, mwenye busara, na kadhalika.
  Lakini ilikuwa inauma sana wakati wa kuadhibiwa, wakati wa kuchapwa. Alikuwa na fimbo kali sana zinazouma mno. Ulikuwa ukiwadia wakati wa kuchapwa, anayetakiwa kuchapwa aliumia, alitokwa machozi kabla ya kuchapwa na kwa kweli aliwaza sana kabla ya kutega ‘makalio’. Hali iliyokuwa ikimkuta mtu anayetakiwa kuchapwa ndiyo ninayoiona ikiwakumba ndugu zetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) hususan rafiki yangu Nape Nnauye. Huyu ni rafiki yangu na kwa kiasi fulani nampenda huyu jamaa! Na hasa kilichonifanya nikampenda ni uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki.
  Kabla ya kampeni za uchaguzi ule nilimsikia Nape akitamba kwenye vyombo vya habari kwamba CCM itashinda uchaguzi huo kwa kishindo. Akatoa wito kwa CHADEMA tena akisema alikuwa anaomba kila kukicha ili CHADEMA katika uchaguzi huo wamsimamishe Dk. Slaa na CCM wamshinde na kumshusha hadhi kisiasa na hatimaye ashindwe kugombea urais mwaka 2015. Nikamweleza Nape kwamba CHADEMA itashinda uchaguzi ule na kwamba kumsimamisha Slaa ni sawa na kuua mbu kwa tofali na uharibifu wa rasilimali fedha na rasilimali watu. Tulimsimamisha ‘dogo janja’ na kushinda kwa kishindo. Kilichonifurahisha kwa Nape ni jinsi alivyokubali matokeo haraka!

  Kihistoria, Nape ni mmoja wa wanamtandao wa moja ya mitandao midogo iliyotokana na kuvunjika ama kuparaganyika kwa mtandao mkuu uliomwingiza Kikwete madarakani. Mtandao wa Nape ni ule unaoongozwa na Samuel Sitta unaoitwa: “wapiganaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama cha mafisadi”. Kuna taarifa nyingi zimedai na kina Nape wamekuwa wakikanusha kijuujuu tuhuma za kwamba walipoona wamezidiwa na mtandao wa wenzao walihofia kwamba wanaweza wasipate nafasi ya kugombea ubunge kupitia ‘chama cha mafisadi’. Walichokifanya kama tulivyoelezwa na aliyekuwa mwenzao ndugu yetu na mpiganaji maarufu kwa leo Kamanda Fred Mpendazoe, walianza mkakati wa kuanzisha CCJ ili baadaye wang’atuke na CCJ nzima na kujiunga na CHADEMA ili kukipa nguvu ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2010.

  Ukipima maelezo ya Mpendazoe na majibu ya Nape na rafiki yake Sitta, kama una akili timamu utakuwa na kila sababu ya kukubaliana na Mpendazoe. Na kama tukiamua kukubaliana na Mpendazoe japo kwa sasa, basi Mpendazoe anasema pale Sitta alipohakikishiwa kurudi kwenye ubunge na uspika na mkuu wa kaya na Nape akaahidiwa na mkuu huyo kumpa angalau ukuu wa wilaya, wakageuka na kuamua kubaki ndani ya chama hicho. Baadaye wakaja kufanya mkakati wa kumwaminisha mkuu wa kaya kwamba ule mtandao mwingine mdogo ambao wao waliuita wa mafisadi, ndio unaokikosesha chama hicho mvuto na imani kwa wananchi. Mkuu wao kwa umahiri wa ‘usanii’ akaiita hali hiyo sawa na chama kuvaa gamba. Akatangaza kukivua chama gamba akimaanisha kuwatimua toka kwenye nyadhifa zao wale wote walioitwa na akina Nape mafisadi.

  Wakati akitangaza mkakati huo alishachukua baadhi ya wanamtandao wa wapiganaji ‘feki’ dhidi ya ufisadi na kuwaingiza kwenye serikali yake mfano kwa kuwapa uwaziri Sitta, Mwakyembe, Nyalandu na Nape (ukuu wa wilaya).

  Baada ya kutangaza kuvua gamba akaamua kutimua sekretarieti yote ya chama na kubadilisha baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Katika mageuzi hayo ndipo alipomteua Nape na vijana wenzake kuongoza sekretarieti ya chama. Ninachotaka kukieleza hapa ni kwamba Nape aliingia na matumaini makubwa sana kwenye uongozi wa chama. Alitangaza kwa nguvu sana kuvuliwa kwa magamba akiwa anawataja kabisa majina kina Lowassa, Chenge na Rostam Aziz kama ndio magamba. Kitu kimoja ambacho hakukitambua ni kwamba mkuu wa kaya hakukutana barabarani na hao aliowaita magamba na kwamba falsafa ya kuvua gamba ilikuwa danganya toto.

  Baada ya muda alijikuta kuvua gamba kunashindikana na akalazimika kula matapishi yake kwa kuruka kauli zake mbele za waandishi wa habari akidai eti hajawahi kutaja majina.

  Lakini ni kalamu hii hii ya Mwigamba iliyomtabiria kifo cha kisiasa Nape wakati akiwa busy kutangaza kuvua gamba. Kama ana kumbukumbu atakumbuka nilimwandikia makala nzima hapa kwenye huu ukurasa huu na kumwambia kwamba naliona jeneza lake la kisiasa muda si mrefu.

  Nikamtahadharisha kwamba kama anataka kubaki na heshima kidogo ambayo alikuwa amekwishajijengea, aiage CCM na kujiunga na CHADEMA kwa vijana wenzake kina Zitto, kina Mnyika, nk. Nikamkumbusha jinsi alivyomuita Lowassa fisadi kwenye mradi wa jengo jipya la UVCCM makao makuu na hatimaye akaukosa uenyekiti wa jumuia hiyo na kutimliwa kabisa uanachama wa jumuia hiyo. Hakunielewa!

  Lakini baadaye alijikuta anabadilisha mwelekeo na kuachana kabisa na agenda ya kuvua gamba na kuwatimua mafisadi ndani ya chama.

  Siku hizi haisemi kabisa! Nape alikuwa ameingia na mkakati kwamba wakishatimua wale waliowaita mafisadi, Watanzania watakiona chama kimekuwa safi na hatimaye watakipenda na mwaka 2015 kitarudi madarakani na mmoja kati ya ‘mabest’ zake (anaweza kuwa Sitta, ama Mwandosya, ama Membe, nk) atakuwa rais naye atauonja uwaziri na labda na yeye afanye fanye usanii na baadaye aje kuwa rais. Hakujua kilichokuwa kinamngoja wala hakutaka kuusoma vizuri unabii wa kalamu hii.
  Amekwama! Na amekwama kwa sababu moja amekuja kugundua kwamba wenzake hasa mkuu wa kaya hawana nia ya kuvua gamba. Inasemekana wakati fulani aliwahi kuwatonya marafiki zake wa karibu kwamba NEC isipoamua kwa dhati kuwavua gamba mafisadi, angejiuzulu.

  Lakini mimi nilisema hakuna Mwana CCM huo ujasiri na kweli alishindwa kujiuzulu. Mbali na hilo kalamu kama hii ya Mwigamba zilijitahidi sana kuwaelimisha wadanganyika kwamba wasidanganyike kwa kuwa chama hicho cha zamani ni cha mafisadi watupu. Niliwahi kusema hata mitume kumi na wawili wa vita feki dhidi ya ufisadi nao ni mafisadi. Mambo yamemwendea kombo rafiki yangu Nape.
  Baada ya kukwama akabadili stahili. Sasa akawa ni mtu wa kukishambulia CHADEMA muda wote akisaidiana na makada wake wengine.

  Na hapo sasa ndipo akazidi kujichongea jeneza la kisiasa. Kitendo cha kulishambulia ‘tumaini jipya’ la watanzania kwa sasa, hakiwezi kueleweka mbele ya Watanzania hao hao! Kwa hiyo kwa muda sasa rafiki yangu huyu amejikuta akikinga mafuriko kwa mikono. Kadiri anavyojitahidi kupambana na CHADEMA ndivyo chama hicho kinavyozidi kupaa!

  Nikiwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha najivunia sana moto wa M4C. Mwenyekiti wetu wa taifa akiwa Arusha wakati kabla ya kuanza kampeni za Arumeru Mashariki, aliamua kukaa nasi uongozi wa mkoa na kutengeneza mkakati wa kuwahusisha wanachama na Watanzania kwa ujumla katika kukiendesha chama na hatimaye kushinda uchaguzi ule mdogo. Tukakubaliana kwamba wananchi ndio wakichangie chama fedha na ndio washiriki kampeni kwa sehemu kubwa.
  Lakini katika kuwaza tukafiria kwa nini kile tunachokibuni kisiwe cha kitaifa. Kwamba uwe ni mkakati wa kushinda uchaguzi wa Arumeru na ule mkuu wa 2015. Kwamba kuanzia sasa chama kiende na huo mkakati hadi ushindi wa 2015. Mwenyekiti akashauri ‘slogan’ ambayo ilikuwa tayari imeshabuniwa na chama mapema. M4C – Movement for Change. Tukakubaliana na kuizindua kwa ajili ya Arumeru hapa hapa Arusha.

  Wakati chama kinaelekea kuuzindua rasmi mkakati huo kitaifa jijini Dar es Salaam, sisi Arusha tena tukaamua kuuhuisha na kuupa nguvu. Tukabuni operesheni ambayo itakuwa mkono wa kuume wa mkakati wetu wa M4C. Tukaja na Operesheni “Vua Gamba, Vaa Gwanda”. Tukaitekeleza kwa mafanikio makubwa sana hapa Arusha na hatimaye ikaanza kushika kasi mikoa mingine. Ni matamanio ya vijana wetu wa BAVICHA mkoa wa Arusha chini ya Kamanda, Ephata Nanyaro, kwamba hivi karibuni wana Arusha tupandishe bendera ya CHADEMA yenye nembo ya M4C mpaka kileleni mwa Mlima Kilimanjaro pale ilipo bendera ya taifa. Na hiyo iwe ni alama kwamba M4C isambae nchi nzima na kuleta mapinduzi makubwa. Naamini na ninawaombea vijana wetu waufanikishe mkakati huo na nimewaahidi kwamba mimi kamanda wao nitakuwa nao hadi kileleni.

  M4C imezinduliwa rasmi Jangwani kwa kishindo. Kishindo ambacho kwa kweli kinamuumiza sana rafiki yangu Nape. Amekuwa aking’aka kwamba wanaovua gamba na kuvaa gwanda ni makapi toka kwenye chama chake na kwamba wanashukuru kwa kuwa walikuwa mzigo. Lakini nimemwona wakati M4C inazinduliwa Jangwani yeye alikuwa mkoani Kagera na kwa namna ya kuweweseka akasema hata kama atabaki yeye mwenyewe kwenye chama chake, eti hakitakufa. Akasahau kwamba ukishasema chama unazungumzia kikundi cha watu kuanzia angalau wawili. Sasa sijui atakuwaje mmoja halafu mmoja huyo awe chama. Muhimu ni kwamba anaweweseka na anaona kabisa kuna hatari watu wakaisha ndani ya CCM akabaki yeye na wapiganaji wenzake feki dhidi ya ufisadi. Lakini kuonyesha kuweweseka zaidi, nilimshuhudia Nape akidai eti yeye sasa anazindua “Vua Gwanda, Vaa Uzalendo”. Nashangaa wale wale aliowakataa walipovua gamba na kuvaa gwanda, leo anatakata wavue gwanda na kuvaa uzalendo. Wakivaa uzalendo watakuwa wanachama wa chama gani? Maana uzalendo unapatikana kwenye gwanda na si kwenye gamba.

  Leo nina neno moja tu kwa Nape. Naamini ningemuuliza Mwalimu Lukiko angesema Nape na wenzake walishahamishia akili zao tumboni na kuacha vichwa vitupu. Na kwa hiyo wanahitaji kuchapwa matumboni ili akili zirudi kichwani, warejee kuwa watu wanaofikiri kwa kutumia vichwa na siyo matumbo kama alivyowahi kutamka ‘mtume’ Samuel Sitta. Ndiyo maana nadiriki kumwambia, “Nape Nnauye, jipe moyo macho mbele, tega tumbo tusahihishe makosa!”

  Inauma rafiki yangu Nape, kwa juhudi kubwa unazofanya kuihujumu CHADEMA halafu unashuhudia utitiri ule wa Jangwani Jumamosi iliyopita! Hapana hata ningelikuwa mimi ningeweweseka. Lakini ndiyo hivyo, tega tumbo tusahihishe makosa ndugu yangu. Tukishasahihisha makosa mkaanza kusikia matangazo BBC yakitaja, “Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CCM…” Mtashangaa.

  Kwa makamanda wote, mbele kwa mbele mpaka kieleweke!

  SOURCE : KALAMU YA MWIGAMBA
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  NIMENUKUU: MWALIMU Evarist Lukiko alinifundisha mwaka 1985 somo la Kiingereza. Alikuwa mwalimu mzuri sana wa somo hilo na mimi ni mmoja wa wanafunzi aliowapenda sana kwa kuwa nilikuwa naelewa haraka sana somo lake. Alikuwa ni mwalimu mcheshi sana lakini makini sana kwenye kazi yake na hakusita kumwadhibu mwanafunzi pale alipobaini katenda makosa. Kilichofanya nimkumbuke leo ni maneno yake aliyoyatumia kabla ya kumwadhibu mwanafunzi.

 8. kejof2

  kejof2 JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 1,721
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  asee hzi insha
   
 9. M

  MAKAWANI Senior Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chadema kama Bacelona! Tumetimia kila idara!
   
 10. I

  Iramba Junior Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said mkuu! Ni aibu tupu kwa chama tawala kutumia njia kama hizi za kuhujumu CDM!
  Ndugu zangu shaka ondoweni kwani kamanda Mbowe amewahakikishia Tz na dunia kwamba CDM will never shake kwani hao watu wanaotaka kuyumbusha hawajai hata kwenye kiganja. Kama kweli wamemwelewa kamanda siku ya Jmosi pale CDM square nadhani CCM wangejitahidi kurejesha trust kwa Watanzania na siyo vinginevyo and this is the only way kwa CCM kurudisha heshima ingawa kwa sasa wamechelewa sana
   
 11. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  ngoja aje ajibu mapigo pamoja na le mutuz ze baharia.
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Waraka umetulia kweli. Nape hata mie nasema jipe moyo.macho mbele.tega .........,tukuchape, tusahihishane na kusonga mbele.
  Bora kutubu na kujisasahisha leo na si kungoja kesho usiyoijua!
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Kwani naye huyu kesha pata ile ajira ya kina Rejeo & co baada yakukikosa kitumbua cha EALC?
   
 14. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  siku haipiti vizuri bila kalamu ya Mwigamba
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mi nadhani Nape bado ana nafasi ya kuiaga ccm na kuungana na Wapambanaji wa kweli
   
 16. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukiikosa kalam ya mwigamba .........jimalizeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
Loading...