Nape-Maandamano ni biashara CHADEMA

Nape-Maandamano ni biashara CHADEMA

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
napezmkutano_300_183.jpg

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema vyama vya upinzani nchini vimeshindwa kufanya kazi za siasa badala yake vimegeuka kuwa vya wanaharakati. Aidha ametaka maandamano yanayohamasishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yapuuzwe kwa kile alichosema ni biashara ya kuuza picha za vurugu nje ya nchi kwa ajili ya kupata misaada kutoka mataifa makubwa.

Nape alisema hayo jana Korogwe Vijijini wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Mombo huku katika baadhi ya maeneo nchini, jana polisi wakilazimika kutumia mabomu ya machozi kudhibiti maandamano baada ya wafuasi wa chama hicho kukaidi.

Katika mkutano huo ambao ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mkoani Tanga, Nape alisema vyama vya upinzani ni wanaharakati ambao kazi yao ni kutengeneza vitu na matukio ya ajabu waendelee kupata fedha nje ya nchi wafanye mambo yao.

"Hata kama yako matatizo ndani ya CCM, hakuna kitu kilicho kamili. Lakini (CCM) bado ni chama pekee cha siasa kilichobaki hasa kutokana na vyama vingine kuwa wanaharakati."

Maandamano Alisema kwa muda mrefu kumekuwepo maswali juu ya kile ambacho Chadema kinapata kwenye maandamano ambayo mwisho wake huishia wananchi hasa vijana kupoteza maisha.

"Maandamano ni haki iliyopo kwenye katiba, lengo lake likiwa wakati mwingine kushinikiza jambo fulani lenye maslahi kwa walio wengi kufanyika.
"Maandamano yenyewe yanayoruhusiwa na Katiba yana utaratibu wake na sheria za kufuata kabla ya kuandamana, lakini toka Chadema wameanzisha utaratibu wa maandamano wamefanikiwa kubadili nini zaidi ya kupoteza maisha ya watanzania wasiokuwa na hatia," alihoji.

Nape alisema alitegemea maazimio ya mkutano mkuu wa Chadema yangejikita kwenye mambo ya maendeleo hasa umoja na mshikamano tofauti na azimio kuu la kufanya maandamano nchi nzima bila kikomo.
"Lakini sasa tunajua siri ya maandamano yao, hali ya chama chao mbaya sana, kisiasa na kiuchumi. Katika kujaribu kutatua tatizo hilo wakabuni vurugu na fujo kupitia maandamano.

"Picha za maandamano hayo watazipeleka nje ya nchi ili kuombea misaada ya pesa kwa kisingizio cha kupambana kujenga demokrasia kana kwamba nchini hakuna demokrasia na utawala bora," alisema Nape.

Alisema uzoefu unaonesha maandamano yote yaliyoandaliwa na chama hicho, yamekuwa yakisababisha uharibifu wa mali na upotevu wa maisha ya watanzania hususani katika mikoa ya Arusha, Iringa, Singida, Morogoro, Mbeya na Mwanza.
"Ndugu zangu huwezi kujenga umaarufu wa chama kwa kutumia damu za watu," Nape alisema na kuasa vijana na makundi mengine kuepuka maandamano hayo.
Aliendelea kusema, "Kisa cha kuandamana ni kutaka waonekane wanakamatwa na polisi, ndio maana wanapiga picha na kuwapelekea watu wao Ulaya, ili wawaletee fedha waendelee kushiba kwenye matumbo yao.

"…maana polisi wanataka mwenyekiti atoe maelezo wanakwenda kujazana kwa sababu wanajua kuwa polisi hawatawaruhusu kuingia, polisi wanapowazuia, wanaendelea kuwapiga picha," alisema.

Kwa mujibu wa Nape, sera ya vyama vya upinzani imegeuka ya kugawa nchi na wananchi wake badala ya kushindana kwa sera na mipango ya maendeleo.
Katika mkutano mkuu wa Chadema wa hivi karibuni, azimio kuu lililotangazwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe lilikuwa ni kufanya maandamano nchi nzima bila kikomo kushinikiza bunge la katiba kusitishwa.

CHANZO:Habari Leo
 
Huwa najiuliza hivi ni kweli wanaccm hawa anaozungumza nao hawataki maadili ya viongozi wa umma yawepo kwenye aktiba? hawataki mbunge adhibitiwe ili akae na wananchi wake na sio kuhama jimbo? hawataki ufisadi na rushwa vidhibitiwe kwa kupunguza madarakaya raisi na kuunda taasisi imara zinazojitegemea? Hizo haki za sijui wasanii, wafugaji na wakulima zitapatikankje kama viongozi hawadhibitiwi na kutekeleza yale wananchi wanayotaka?
 
Huyu Nape kichwani mweupe sana,mikutano yake yote mikoanianarudi rudia uongo huo huo hana jipya bora ye aingize posho
 
Yeye na Kinana ndio wanajifanya ndio wenye nchi zaidi ya wengine mbona yeye na Kinana kila siku wanafanya maandamano kweli watanzania ni watu wa kuswagwa tu
 
Kama nilijua vile. Kabla ya kupoteza muda wangu kusoma article yote nikacheki SOURCe kwanza! Hahahahahahahaaa kumbe Habari Leo?!

Sihangaiki na hii thread tena!
 
Kama nilijua vile. Kabla ya kupoteza muda wangu kusoma article yote nikacheki SOURCe kwanza! Hahahahahahahaaa kumbe Habari Leo?!

Sihangaiki na hii thread tena!

Kama maandamano ni biashara aache kutumia polisi wa mbwa,rungu ,fimbo,mabomu ya kutupa na guruneti ili sisi chadema tufanye biashara hii kwa kuwa biaahara lengo lake kuu ni shilingi kuzaa shilingi.
 
nape nijanga hana jipya!yeye badala yakuielekeza serika kupunguza mfumko wa bei yeye anaiandama cdm?amani itapatikanaje ikiwa rasmali za taifa zinawanufaisha wachache yeye nape akiwa miongoni!ama anadhan watanzania niwajinga?leo hii mtanzania mdogo ndo amebesha mzigo mzito,gharama za umeme maji,yanamwangamiza mtu mdogo?mbona hayo hayaoni?hosp na shule kote nivilio je watu watashindwa kuandamana?mzimu wa nyerere unawatafuna,maisha bora kwa mtanzania yapo?kauli hiyo ya chama chake ameikimbia,aje ayaonge maneno hayo mikoa ya arusha,mwanza na kilimanjaro tuone kama hajatolewa belenge,kweli tutaona mengi!
 
Huwa najiuliza hivi ni kweli wanaccm hawa anaozungumza nao hawataki maadili ya viongozi wa umma yawepo kwenye aktiba? hawataki mbunge adhibitiwe ili akae na wananchi wake na sio kuhama jimbo? hawataki ufisadi na rushwa vidhibitiwe kwa kupunguza madarakaya raisi na kuunda taasisi imara zinazojitegemea? Hizo haki za sijui wasanii, wafugaji na wakulima zitapatikankje kama viongozi hawadhibitiwi na kutekeleza yale wananchi wanayotaka?
Maccm yaliwekeza kwenye ujinga na umaskini. Matokeo yake watz. tulio wengi tumekuwa wapumbavu, na tunafiki kipumbavu.
 
Mtu wa Dili anawaza kidilidili muda wote ....ndio Nnape huyu ambaye haujui Babake ,,,,,,,,,
 
Mjinga kama Nape hawana lolote zaidi ya usukule unawasumbua!

Mwisho wao waja soon!
 
... Mtoto Wa Kwenye Mbio Za Mwenge, Hana Akili Kabisaa
 
!... Ni Bora Kuuza Picha Kuliko Pembe Za Ndovu Na Kuiba Wanyama Hai.!
 
Hivi huyu Nape analipwaga au anafanya kazi ya kujitolea kwenye chama, kama analipwa anapata shilingi ngapi kwa siku, kwa siku au kwa mkutano analipwa sh ngapi ili tuweze kuelewa anachosemaga!
 
napezmkutano_300_183.jpg

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema vyama vya upinzani nchini vimeshindwa kufanya kazi za siasa badala yake vimegeuka kuwa vya wanaharakati. Aidha ametaka maandamano yanayohamasishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yapuuzwe kwa kile alichosema ni biashara ya kuuza picha za vurugu nje ya nchi kwa ajili ya kupata misaada kutoka mataifa makubwa.

Nape alisema hayo jana Korogwe Vijijini wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Mombo huku katika baadhi ya maeneo nchini, jana polisi wakilazimika kutumia mabomu ya machozi kudhibiti maandamano baada ya wafuasi wa chama hicho kukaidi.

Katika mkutano huo ambao ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mkoani Tanga, Nape alisema vyama vya upinzani ni wanaharakati ambao kazi yao ni kutengeneza vitu na matukio ya ajabu waendelee kupata fedha nje ya nchi wafanye mambo yao.

“Hata kama yako matatizo ndani ya CCM, hakuna kitu kilicho kamili. Lakini (CCM) bado ni chama pekee cha siasa kilichobaki hasa kutokana na vyama vingine kuwa wanaharakati.”

Maandamano Alisema kwa muda mrefu kumekuwepo maswali juu ya kile ambacho Chadema kinapata kwenye maandamano ambayo mwisho wake huishia wananchi hasa vijana kupoteza maisha.

"Maandamano ni haki iliyopo kwenye katiba, lengo lake likiwa wakati mwingine kushinikiza jambo fulani lenye maslahi kwa walio wengi kufanyika.
“Maandamano yenyewe yanayoruhusiwa na Katiba yana utaratibu wake na sheria za kufuata kabla ya kuandamana, lakini toka Chadema wameanzisha utaratibu wa maandamano wamefanikiwa kubadili nini zaidi ya kupoteza maisha ya watanzania wasiokuwa na hatia,” alihoji.

Nape alisema alitegemea maazimio ya mkutano mkuu wa Chadema yangejikita kwenye mambo ya maendeleo hasa umoja na mshikamano tofauti na azimio kuu la kufanya maandamano nchi nzima bila kikomo.
“Lakini sasa tunajua siri ya maandamano yao, hali ya chama chao mbaya sana, kisiasa na kiuchumi. Katika kujaribu kutatua tatizo hilo wakabuni vurugu na fujo kupitia maandamano.

“Picha za maandamano hayo watazipeleka nje ya nchi ili kuombea misaada ya pesa kwa kisingizio cha kupambana kujenga demokrasia kana kwamba nchini hakuna demokrasia na utawala bora," alisema Nape.

Alisema uzoefu unaonesha maandamano yote yaliyoandaliwa na chama hicho, yamekuwa yakisababisha uharibifu wa mali na upotevu wa maisha ya watanzania hususani katika mikoa ya Arusha, Iringa, Singida, Morogoro, Mbeya na Mwanza.
"Ndugu zangu huwezi kujenga umaarufu wa chama kwa kutumia damu za watu,” Nape alisema na kuasa vijana na makundi mengine kuepuka maandamano hayo.
Aliendelea kusema, “Kisa cha kuandamana ni kutaka waonekane wanakamatwa na polisi, ndio maana wanapiga picha na kuwapelekea watu wao Ulaya, ili wawaletee fedha waendelee kushiba kwenye matumbo yao.

“…maana polisi wanataka mwenyekiti atoe maelezo wanakwenda kujazana kwa sababu wanajua kuwa polisi hawatawaruhusu kuingia, polisi wanapowazuia, wanaendelea kuwapiga picha,” alisema.

Kwa mujibu wa Nape, sera ya vyama vya upinzani imegeuka ya kugawa nchi na wananchi wake badala ya kushindana kwa sera na mipango ya maendeleo.
Katika mkutano mkuu wa Chadema wa hivi karibuni, azimio kuu lililotangazwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe lilikuwa ni kufanya maandamano nchi nzima bila kikomo kushinikiza bunge la katiba kusitishwa.

CHANZO:Habari Leo

hili vuvuzela muachane nalo,,halijui likifanyacho
 
Huwa wanasema KITANDA HAKIZAI HARAMU lakini kwa hili na NAPE linakuwa tofauti na tukikumbuka kuwa huyu Nape hana malezi ya baba na ndio maana amekaa kimamamama yaani anaendekeza mipasho ya kwenye kanga na Taarabu.
 
Si anafanya kampeni ya siasa?Nape ajenge hoja ya namna ya kuwaondolea umma wa Watanzania umasikini.sasa ni kitu gani cha maana kakizungumza?wananchi wa Mombo nawajua;wale wamekusanywa vijijini kama kawaida ya ccm na kujifanya kukosoa Vyama vingine vya siasa;ni taratibu gani za kufanya maandamano ambayo CHADEMA wamezivunja?mngemuuliza azitaje;mi nasemaga hivi:ccm ka si kutumia polisi,hawa ni chakula kabisa ya CDM
 
Back
Top Bottom