Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nape Nnauye amesema kuwa sababu ya yeye kuwa mkali na kupiga kelele kuhusu maji ni kutokana na maeneo ambayo wapiga kura wake huchota maji.
Nape amechapisha picha zikionyesha watu wakichota maji katika visima na kuandika,
"Huku ndiko wanakochota maji baadhi ya wapiga kura wangu! Sasa mtaelewa kwanini napiga kelele na maji".
Akichangia hutoba ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Nape Nnauye alisema mabadiliko yanayofanywa na Rais Magufuli hayatakuwa na manufaa kama huduma za jamii hazitoboreshwa, huku akishauri bajeti hiyo kuongezwa.
Aidha, Nape Nnauye ameijibu juu Serikali kuhusu kupunguzwa kwa bajeti ya maji kutoka zaidi ya bilioni 900 kwa mwaka 2016 /2017 hadi kufikia bilioni 672. 2 kwa mwaka 2017 /18 ikiwa ni punguzo la asilimia 30.
Mbali na Nape, wabunge wengine waliopata nafasi ya kuchangia hutoba hiyo akiwemo, Zitto Kabwe, Mussa Mbarouk, Suleimani Bungara, Tunza Malapo na Dk. Mary Nagu waliunga mkono hoja bajeti ya Wizara hiyo kuongezwa kwani maji ni tatizo linalowakumba wananchi wengi nchini.