NAPE gear your brain before you open your mouth | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NAPE gear your brain before you open your mouth

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mjomba wa taifa, Jun 1, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jana nape amesikika kupitia redio clouds akisema aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige sio saizi yake ni mtu wa chini sana ambaye hoja zake zinapaswa kujibiwa katika ngazi ya shina. Kama kiongozi hupaswi hata siku moja kuropoka kuwa ukubwa wa cheo chako huwezi kufanya jambo dogo kwa dharau.

  Kama kiongozi mwenye maadili, ulipaswa kukaa kimya ama kutumia lugha inayoendana na cheo ulichokabidhiwa matokeo yake umejiingiza katika mipasho ambayo haina tofauti na walevi uswailini.

  Umesikika ukisema kuwa wanachama wa CCM wanaotimkia CHADEMA hawana madhara kwa chama kwani hawafiki idadi inayoripotiwa. Umefikia kusema mkutano wa CHADEMA wa Jangwani haukuwa na idadi ya watu zaidi ya 3,000. Hivi kwa ule umati uliofurika Jangwani unasema hawakufika watu 3,000? shame on you. Una mhadaa nani?

  Umesikika pia ukisema hutishwi na wimbi la wana-CCM wanaoondoka na kujiunga CHADEMA maana hata hao walioanzisha vyama vya upinzani walitokea CCM, hiyo kauli ipo siku itakutokea puani. Tafadhali acha propaganda za kizamani ambazo zinaonesha nafasi uliyopewa si size yako. Viongozi wako wote hawapati usingizi kwa kuhofia M4C then we una-joke kuwa huhofii. Usidhani wewe unaipenda zaidi CCM kuliko wale wote waliotangulia na yakawashinda wakavua magamba.

  Kumbuka kuna waliowahi kuwa viongozi vijana wa nchi hii waliobweteka na madaraka waliyopewa na kuanza kudharau watu mitaani na hatimaye haohao wananchi waliowadharau wakawaondoa madarakani.

  Take my words please, gear your brain before you open your mouth.
   
 2. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ubongo wa jamaa una matatizo,sijui kama anaweza kukuelwa,Nape anataka kuwasadikisha watanzania
  kuwa hakuna kinachoendelea kwenye nchi hii na wala hakuna mabdiliko,wakati ukweli halisi anauona na
  watanzania wote wanaona.mwanzo walisema upinzani vyama vya msimu wamechanganyikiwa kuona CDM
  si cha msimu,ooh chama cha ukanda na ukabila"wameaibika kwa umati ulifurika jangwani ambao kila mtanzania
  aliona LIVE" Nape atamdanganya nani tena.walisema chama cha udini M4C Mtwara imedhihirisha kuwa
  propaganda za jamaa na wenzake hazina tena mashiko.mwisho wa siku Nape atakishuhudia alichokiona Sadam
  Husein,ndipo akakubali kuwa huwezi kushindana na nguvu"
   
 3. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyie yaachen magamba, yakanyagane, yameshikwa pabaya......
   
Loading...