idoyo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2013
- 3,051
- 1,423
Mbunge mteule wa Mtama (CCM) Bw. Nape Nnauye amesema CCM wanatamani sana jimbo la Moshi na kama wangekuwa wanachakachua matokeo wangekuwa wameshatwaa jimbo hilo. Maeneo mengine ambayo wanatamani zaidi ni Pemba na Karatu. Ameyasema hayo alipokuwa akijibu hoja za mbunge mteule wa Ubungo (CHADEMA) Bw. Saed Kubenea wakati wakihojiwa na Ivona Kamuntu, AzamTV. Kubenea amewatuhumu CCM na NEC kuhusu wizi wa kura. Pia Nape amesikitishwa na kile alichokiita 'kupigwa' kwa CCM kwenye mji mkubwa wa Dar es Salaam.