Nape awatenga ASP

Status
Not open for further replies.

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Wakati chama cha Mapinduzi(CCM)kikijiandaa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kuwa chama hicho kimekusudia kuanza kujitathmini kwa kukumbuka kazi ya kupigania Uhuru iliyofanywa na chama cha TANU kilichozaliwa tarehe 7 Julai, 1954.

Swali langu ni je kama sherehe hizo zitafanywa na wanachama wote wa CCM, wanachama waanzilishi wa chama cha ASP kilichoungana na TANU watakuwa upande gani, wageni waalikwa? Je hili haionekani kama Nape anataka kuzalisha mtafaruku mwingine ndani ya chama chake. Naomba kuwasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom