NAPE AMPONGEZA SAMATTA KWA KUWA MCHEZAJI BORA

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye amempongeza mchezaji wa mpira wa miguu wa Taifa Star Mbwana Samatta baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka Afrika 2016 kwa wachezaji wanaocheza soka Barani Afrika.iliyotolewa nchini Nigeria.

Nnauye ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na watumishi wa Wizara wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo leo jijini Dar es salaam.

Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.

Nnauye amewataka wachezaji wengine kufuata nyayo za mchezaji huyo kwa kuongeza juhudi, nidhamu katika michezo na watambue kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

Akifafanua zaidi Nnauye alibainisha kuwa kilichomfikisha Samatta hapo ni kujitambua na kujituma katika ajira yake.

Samatta ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Barani Afrika kwa kupata alama 127 dhidi ya Robert Kidiaba aliyepata alama 88 na Baghdad Bounedjah alama
 
Forwarded as received.., hahahahahaaa
 

Attachments

  • 1452315539818.jpg
    1452315539818.jpg
    56.9 KB · Views: 12

Similar Discussions

Back
Top Bottom