Napataje connection ya kazi kwenye migodi ya Barrick

digalangosha

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
1,574
Reaction score
2,292
Poleni kwa mzigo wa tozo, kodi na vat

Point yangu ni moja, since then nilikua napenda sana kufanya kazi kwenye migodi (kazi ya ndoto yangu) lakini sijawahi kupata connection za huko.

Kwenye maisha hujui utatokea wapi, anyone mwenye connection ntashukuru sana, japo najua mkono mtupu haulambwi.

1662050356.jpg
 
maeneo ya connection utaweza kupata ni haya hapa: tripple 777, juliana beach kidibwi, level 8( soda elfu kum), las vegas, copen hagen, michigan n.k, ila siyo kwengineko. tafuta 20000, nenda hayo maeneo kama ndan ya mwez tu, utakuja kunishukuru. siyo conection unaenda kumuomba mpwayungu village, unategemea nini? nakutania mwanangu mpwayungu village hahahahahaha
 
😆
 
Huko migodini huwa wanatangaza sana kazi na applications ni online inategemea na qualification zako na exposure, ila kama hujawa nguli na experience yakutosha + exposure tafuta hela kiasi nenda maeneo kama Bulyanhulu, Geita au Northmara aka Nyamongo kasotee kwenye vikampuni vidogo vidogo vya contractors then ukiingia huko ndani unaweza kupata connection kwa kukutana na watu hapa na pale.

Kama una muda, kajifunze uendeshaji wa mitambo ya underground kama Scoop, drill rigs au bogger, unaweza kupata vigezo vya entry level ukaingia kama trainee operator.
nimesema underground maana kwasasa kunalipa sana kuliko open cut.

Kwa wale vijana wenye vyeti vya ufundi either veta au qualified engineers mjitahidi sana kusotea kazi za underground au kwenye makampuni ya drilling maana kwa sasa mining world wide kuna demand kubwa sana ya mafundi, maoperators, wa underground mines na drilling operations na ndio kwenye hela za kutia vichaa huko.
 
Ngoja leo nisaidie vijana.

Mining, Oil and gas activities zinalipa sana ukiingia vizuri hasa ukianzia kwenye hand-on then ukagrow to management level huwa kuna hela sana ukikaa pazuri na sio hela tu bali unakuwa na demand kubwa sana.

Ukitoka shule kama wewe ni graduate engineer au kijana wa veta focus sana hayo maeneo na ujikite sana kwenye kujifunza kwenye floor kwa miaka kadhaa kabla then sasa anza kutafuta hela.

Mining, Oil and gas ndio field pekee ambazo ukijipanga vizuri unaweza kuwa unaajirika worldwide cha msingi uwe competent tu.
Makampuni mengi makubwa yana programes za trainee engineers, jitahidini muingie kwenye hizi programes hata usote miaka 2~3 poa tu komaa lakini baada ya hapo inaweza kuwa hadithi.
 
Kwa wale Graduates engineers, ukutoka Shule ukapata kakazi hata ka mshahara mdogo, utumie muda wako vizuri na uwekezaji kwenye career yako.

Siku hizi kuna vicourse vingi sana online ambavyo unaweza kuvitumia kukuza career yako kwa kuspecilize kwenye maeneo tofauti tofauti na ukawa competent na gharama unakuta ni ndogo sana na vingine unakuwa mpaka certified kwa kufanya mitihani.

Ukitoka shule tumia 5yrs kufanya kazi kwa bidii uwe competente na uwekeze kwenye field yako ili uwe marketable world wide uachane na vihela mbuzi hivi na interview zamajungu utumishi, you will always interviewed online via skype, webex nk.
 
kijana ukiwa secondary jifunze sana Computer skills na matumizi ya applications mbalimbali kama Excell, word na full package ya microsoft office, ukimaliza Form IV make sure uko competent kwenye matumizi ya computer na uongeaji wa kiingereza (wazazi tujitahidi kwenye hili, achana na siasa za wanasiasa tengeneza familia yako na wewe mwenyewe).
 
Tunarudi kwenye connection migodini:

kwasasa kuna migodi minne mikubwa inayooperate.
North Mara ~ pale nyamongo, tarime.
Bulyanhulu ~ Kakola kati ya kahama na Geita.
Geita Gold ~ Geita town.
Shanta mine ~ Chunya aka makongosi.

Hiyo migodi yote iko active inaoperate, upatikanaji wa kazi kwa watu ambao ni proffesional huwa ni kuomba kazi online na kama sio proffesional unapaswa kufika eneo husika kuangalia deiwaka za kila siku za macontractors unaweza kupata connection za uhakika na uzoefu humo.

wasoteaji wengi huwa wanaungaunga kwenye hayo maeneo kwa kushare magheto na kusaidiwa na wakongwe maisha ya kila siku, mfumo huu unakupa uzoefu wa kujuana na watu mbalimbali ambao unaweza kuta wana connection za ndani ya migodi, lakini pia maeneo ya migodi ni maeneo ya starehe na maeneo hayo wakongwe wengi hufika kufanya starehe na kupitia watu hao unaweza kupata connectio ~ watu wema wapo bado wanaoweza kutoa msaada.
 
Huko migodini huwa wanatangaza sana kazi na applications ni online inategemea na qualification zako na exposure, ila kama hujawa nguli na experience yakutosha + exposure tafuta hela kiasi nenda maeneo kama Bulyanhulu, Geita au Northmara aka Nyamongo kasotee kwenye vikampuni vidogo vidogo vya contractors then ukiingia huko ndani unaweza kupata connection kwa kukutana na watu hapa na pale.

Kama una muda, kajifunze uendeshaji wa mitambo ya underground kama Scoop, drill rigs au bogger, unaweza kupata vigezo vya entry level ukaingia kama trainee operator.
nimesema underground maana kwasasa kunalipa sana kuliko open cut.

Kwa wale vijana wenye vyeti vya ufundi either veta au qualified engineers mjitahidi sana kusotea kazi za underground au kwenye makampuni ya drilling maana kwa sasa mining world wide kuna demand kubwa sana ya mafundi, maoperators, wa underground mines na drilling operations na ndio kwenye hela za kutia vichaa huko.
Huu uendeshaji wa scoop na hiyo mitambo mingine unajifunzia wapi?
 
Ndugu yangu vyuo vyote ambavyo vinatoa mafunzo ya uendeshaji wa mitambo vimejikita katika mafumzo ya mitambo ya ujenzi na mitambo ya open cast mining kama vile excavator, wheel loader, dump trucks etc.
Kwa hiyo mitambo yote ya underground mining kama scoop/bogger, IT, spray mech, Agitator, charge unit, trucks, jumbo, solo etc mafunzo yake hutolewa pale pale mgodini kwa sababu hakuna chuo Tanzania hii ambacho kina mitambo hiyo.
Hivyo basi kuhusu connection ni kama ilivyoainishwa hapo awali ni kuanzia kwenye kampuni za sub contractors ili upate connection ya kuingia kampuni mama au kama una ndugu yako boss basi unaweza kuingia moja kwa moja. Ila hutafikia kwenye mitambo moja kwa moja lazima kwanza uanzie kuwa offsider (ni kazi ngumu kiasi na kama ni mtoto mayai utakimbia mapema) halafu baada ya muda unaweza kupanda na kuwa service crew baada ya hapo ndio unaweza kwenda kwenye mitambo baadhi au idara ya ulipuaji baruti.
Naomba kuwasilisha.
 
Huu uendeshaji wa scoop na hiyo mitambo mingine unajifunzia wapi?

Kiukweli kwa Tanzania hakuna mahala wanatoa training ya hizo Scoop na underground rigs labda upate bahati ya kuajiliwa kama trainee watakufundisha migodini.

ila kama una uwezo SA huwa vyuo vipo vingi na fee ni ndogo sana almost 1.5mil or 2mil unapewa na cheti vingine vina mpaka hostel na course za mwezi tu, hapo tayari unapata entry level yakuingia underground.

Otherwise ujifunze uperator wa machine za kawaida surface au construction then utafute experience kwenye ujenzi wa barabara huko then utumbukie mining uforce uende underground.
 
Tunarudi kwenye connection migodini:

kwasasa kuna migodi minne mikubwa inayooperate.
North Mara ~ pale nyamongo, tarime.
Bulyanhulu ~ Kakola kati ya kahama na Geita.
Geita Gold ~ Geita town.
Shanta mine ~ Chunya aka makongosi.

Hiyo migodi yote iko active inaoperate, upatikanaji wa kazi kwa watu ambao ni proffesional huwa ni kuomba kazi online na kama sio proffesional unapaswa kufika eneo husika kuangalia deiwaka za kila siku za macontractors unaweza kupata connection za uhakika na uzoefu humo.

wasoteaji wengi huwa wanaungaunga kwenye hayo maeneo kwa kushare magheto na kusaidiwa na wakongwe maisha ya kila siku, mfumo huu unakupa uzoefu wa kujuana na watu mbalimbali ambao unaweza kuta wana connection za ndani ya migodi, lakini pia maeneo ya migodi ni maeneo ya starehe na maeneo hayo wakongwe wengi hufika kufanya starehe na kupitia watu hao unaweza kupata connectio ~ watu wema wapo bado wanaoweza kutoa msaada.
Umefafanua kwa moyo mweupe sana.
 
Huu uzi umenivutia sana hasa baada ya kusoma michango/ushauri wa ndugu Nangu Nyau...

Kwa uzoefu wangu upatikanaji wa kazi za migodini hautofaitiani sana na maeneo mengine ya sector binafi kwanza lazima uwe na connection ikusaidie kupata taarifa, pili lazima uwe na sifa kulingana na nafasi iliyotangazwa pia ukiwa na refa (mtu wa kukupigia debe) huwa inasidia sana, utaratibi huwa mara nyingi hufuatwa kama kazi inayotangazwa ni yakitaaluma,
Kwa kazi ambazo si zakitaaluma hizi zinachangamoto sana kuzipata maana zaidi ya asilimia 90 ni lazima uwe na refa maana ni kazi ambazo zinaweza kufanywa na watu wengi ili mradi tu uwe na basic education.

Nafkri na mimi nimeongezea kwa walio nitangulia...
 
Lingine la kuongozea ambali linaihusu sana serikali, Serikali ijaribu kukaa chini na wafanyakazi watanzania ambao ni skilled waliopo kwenye operations au waliowahi kupita kwenye operations na kuwa promoted kwenye higher ranks kuanzia Underground mines, Open cut mines pamoja na waliopo kwenye oil and gas.

Lengo la kukaa nao hasa ni kuangali practically mahitaji ya soko na namna ya kufanya kutengeneza skills za vijana wetu ili wengi waweze kuajirika kwenye mid skilled levels and higher na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira.

Nchi kama Australia, Canada na Scotland zimeendelea sana kwa kuwekeza kwenye trades mbalimbali ambazo hutengeneza vijana wengi kwenye kazi za mines na oil and gas jobs, Engineering trades kuanzia mining, mechanical, geology, electrical, oil and gas zinaweza kutatua kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira na vijana wetu wengi wakawa proffesionals sehemu mbalimbali duniani.

Dunia ina mahitaji mengi sana kwenye taalum ambazo ni risk kama mining, oil and gas, tukitengeneza vijana wengi huko wengi wataajirika world wide na kupunguza tatizo kwa kiasi kikubwa maana kazi hizi nyingi mishahara ni mizuri na wengi watapata fursa ya kuja kuwekeza na kutoa ajira vijana wengi.

Serikali ianze kutoa scholarships mbalimbali Australia, Canada, Scotland, Germany na India vijana wengi kwenda kwenye short courses za kuanzia mwaka mmoja mmoja kusomea trades mbalimbali.
Serikali pia itoe scholarships kwa engineers walioko mining, oil and gas kwenda kusomea na kuangalia namna kadhaa za kuboresha mitaala ya shule na kutengeneza vocational training kubwa kwenye kanda tatu zitakazokuwa full equiped na watalaam wakutosha kutoka nje na ndani pamoja na kushinikiza makampuni yote kuwa na trainees, internships na apprentice programes kazi zao.
 
Kiukweli kwa Tanzania hakuna mahala wanatoa training ya hizo Scoop na underground rigs labda upate bahati ya kuajiliwa kama trainee watakufundisha migodini.

ila kama una uwezo SA huwa vyuo vipo vingi na fee ni ndogo sana almost 1.5mil or 2mil unapewa na cheti vingine vina mpaka hostel na course za mwezi tu, hapo tayari unapata entry level yakuingia underground.

Otherwise ujifunze uperator wa machine za kawaida surface au construction then utafute experience kwenye ujenzi wa barabara huko then utumbukie mining uforce uende underground.
umeandika ukweli mtupu, hongera sana kwa mchango wako huu mzuri
 
Kiukweli kwa Tanzania hakuna mahala wanatoa training ya hizo Scoop na underground rigs labda upate bahati ya kuajiliwa kama trainee watakufundisha migodini.

ila kama una uwezo SA huwa vyuo vipo vingi na fee ni ndogo sana almost 1.5mil or 2mil unapewa na cheti vingine vina mpaka hostel na course za mwezi tu, hapo tayari unapata entry level yakuingia underground.

Otherwise ujifunze uperator wa machine za kawaida surface au construction then utafute experience kwenye ujenzi wa barabara huko then utumbukie mining uforce uende underground.
Mkuu unaweza kunisaidia link za hivyo vyuo huko SA? Na vipi upatikanaji wa ajira baada ya kurudi bongo?
 
Huko migodini huwa wanatangaza sana kazi na applications ni online inategemea na qualification zako na exposure, ila kama hujawa nguli na experience yakutosha + exposure tafuta hela kiasi nenda maeneo kama Bulyanhulu, Geita au Northmara aka Nyamongo kasotee kwenye vikampuni vidogo vidogo vya contractors then ukiingia huko ndani unaweza kupata connection kwa kukutana na watu hapa na pale.

Kama una muda, kajifunze uendeshaji wa mitambo ya underground kama Scoop, drill rigs au bogger, unaweza kupata vigezo vya entry level ukaingia kama trainee operator.
nimesema underground maana kwasasa kunalipa sana kuliko open cut.

Kwa wale vijana wenye vyeti vya ufundi either veta au qualified engineers mjitahidi sana kusotea kazi za underground au kwenye makampuni ya drilling maana kwa sasa mining world wide kuna demand kubwa sana ya mafundi, maoperators, wa underground mines na drilling operations na ndio kwenye hela za kutia vichaa huko.
Umetisha sana mkuu...maelezo mafupi lakini yameshiba
 
Mimi ni kijana wa mazingira nipo hapa kupata madini na connection
Ni hivyo tuu
 
Back
Top Bottom