Napata shida sana, baada ya kujua mtoto siyo wangu

zinc

JF-Expert Member
May 24, 2013
1,392
1,067
Wakuu JF,

Matumaini yangu nyie ni wazima hapa,

Yaani ninawamiss na ninawapenda wadau wa ukweli,

Kwanza mnanisadia nikipata tatizo binafsi, hata marafiki zangu wanaonieleza shida zao, nikiona nashindwa kuwasaidia, huwa nakuja kuomba ushauri kwa niaba yao hapa, na mmekuwa mnaonyesha nia ya kuwasaidia.

Nisiongee sana, mwaka 2013 kuna msichana nilimpata, ni mzuri sana, tuliamua kuanzisha uhusiano na mwanzoni tulifurahiana, sasa sijui ghafla mtoto kashika mimba, hakuniambia, baadae nikaja kueleza hii ishu humu ndani, ikawa kama ndiyo nimetibua. Nikapata ushauri wa baadhi ya members kuwa nitulie then nizungumze nae, ili tumalize ki utuzima. Nikasikiliza na nikaona vema nifanye hivyo.

Sasa mwisho wa siku shemeji yenu, wifi yenu, dada yenu akajifungua salama salmini, nimehudumia, nikarudisha mapenzi na upendo tele, that's why wanaomfahamu. Sasa nimeyasikia maneno yake akimuambia mama yake kuwa ananipenda lakini anaona aibu kunieleza ukweli kwamba mimi siyo baba mtoto.

Naomba niishie hapa maana, sina mood nzuri wakuu
 
Duh, pole aisee.

Kama unaweza, m-confront kiustaarabu, kwamba unafahamu kuwa huyo mtoto si wako, and you're giving her this one and only chance akueleze kwanini alikuficha.

Baada ya hapo I suggest you take a break from the relationship, hii itawapa both of you time ya kutafakari on what you want. Kama kweli amejutia kosa na bado yuko interested ku-have you back in her life, basi unaweza ukaendelea nae as long as unampenda na you are willing to forgive her kwa alichofanya.

Ila kama utaona huwezi kuendelea nae, cause it's very painful mtu kukufanyia jambo hilo, basi mwambie tu it's over na kila mtu aendelee na maisha yake.
 
Achana na huyo mwanamke,wewe ni mwanaume acha kufikiria fikiria hovyo kwa kutumia moyo,tumia ubongo.

Tena umesikia mwenyewe akisema unataka nini cha zaidi?
 
Pole sana,kama ulimsikia akimwambia mama yake ,huo ndo ukweli,mjulishe ajue ha kwamba unajua huyo mtoto si wako,then take break.
 
Duh, pole aisee.

Kama unaweza, m-confront kiustaarabu, kwamba unafahamu kuwa huyo mtoto si wako, and you're giving her this one and only chance akueleze kwanini alikuficha.

Baada ya hapo I suggest you take a break from the relationship, hii itawapa both of you kutafakari on what you want. Kama kweli amejutia kosa na bado yuko interested ku-have you back in her life, basi unaweza ukaendelea nae as long as unampenda na you are willing to forgive her kwa alichofanya.

Ila kama utaona huwezi kuendelea nae, cause it's very painful mtu kukufanyia jambo hilo, basi mwambie tu it's over na kila mtu aendelee na maisha yake.
Mkuu hapa hamu sina. Naona kama nipo ndotoni. I can't think wisely from this
 
Mkuu hapa hamu sina. Naona kama nipo ndotoni. I can't think wisely from this
Basi mi nakushauri usifanye/mweleze chochote, for the time being, mpaka pale akili yako itakapokuwa kidogo imetulia.It might be hard, but try your best.
Uzalendo ukikushinda na ukaamua kum-confront basi try to do it in a calm manner.
 
hamna haja ya kuwachana nae...wanaume wengi tunalea watoto wa wanaume wengine..makosa yalitokea na adhari zake zipo ila zingatia uhusiano wenyu wa sasa..hamna haja ya kurudi square one kama mshaendeleza maisha yenyu..
 
Mkuu pole kwa taarifa za kushitukiza lakini lipo tumaini kwa watu wanaopitia katika shida kama yako. Cha kufanya mwambie kuwa ungependa kupima DNA ili kujua kama kweli mtoto ni wa kwako... Vipimo vikithibitisha majibu kuwa mtoto si wa kwako then hapo mlango uko wazi. Hiyo itakuwa sababu tosha ya wewe kutoka kwenye huo uhusiano na kuanza upya... Kama Flora Mbasha ameweza, wewe utashindwa nini? Maadam wewe ni mtoto wa kiume bado unaweza ukaaanza upya... Mwangalie mzee Mengi ana vitoto vidogo alivyo zaa na Kay Lin lakini maisha yanasonga.
 
Kiongoz hakuna kitu kinachotesa kam kutojua ukweli,ongea na mama ake akupe ukweli afu ndo umbane yeye atasema ukweli,wanawake wan roho za ajabu Sana usiwachukulie poa,..na Kama ukingudua ukweli achan nae uyo manzi ni muuaji tena shetani kabisa,ni hayo mkuu,pole sana
Mwenye ukweli ni mke sio mama mkwe,ambane mwanamke wake shahidi akiwa mama mkwe.Lakini kama umesikia,Si umwambie tu nimekusikia na nimejua ukweli!!
 
Wewe mwenyewe ukimwangalia huyo mtoto hakuna features zako kabisa? Kapime kwanza blood groups zenu kwa kuanzia. Je, mmefunga ndoa kwa taratibu sahihi? Kama hapana, basi achia ngazi endapo mtoto sio wako.
 
Back
Top Bottom