Naona wadhamini wengi msimu ujao TPL.

evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Messages
2,021
Points
2,000
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2015
2,021 2,000
Wasaalam wakuu,

Niingie kwa mada moja kwa moja.Ligi yetu baada ya kuisha na kutokuwa na mdhamini mkuu na hata kupelekea mshindi kutokujulikana anapewa nini, labda ni kutokana na TFF kutokufikia muafaka na hao wadhamini.

Kwa msimu ujao hata kusipokuwa na mdadhamini mkuu, naona kwa mbali wadhamini wengine kwa ngazi ya vilabu kujitokeza kwa wingi, na hii ni kutokana kuona kuwa Mpira unalipa,mpira ni pesa na mpira ni biashara kwa sasa. Jicho langu kwa udhamini ni kama ifuatavyo;

1) Klabu ya Simba, wekundu wa msimbazi pamoja na kuwa na udhamini mnono wa SportPesa na Mo Energy bado naona moja ya bank kubwa ikipiga charter yake kwenye Uzi wa simba msimu ujao.

2). Club ya Young African, wana jangwani hawa ukiacha SportPesa na maji ya Afya ambayo hayapo kwa Uzi,lakini naona young African wakienda kupata mdhamini mwingine atakaewapiga tough kuelekea msimu mpya wa ligi.

3). Azam fc, hawa matajiri wa jiji wamechafuka na juice ya African Fruits pamoja na maji Uhai mgongoni, Azam fc wadhamini wenza wameshapata wengine, baada ya kuachana na NMB msimu ulioisha, nao ni GF truck ambapo tayr washaweka chata yao kwa kifua cha azam(rejea Uzi waliovaa Fainali ya FA).

4). Lipuli fc, wanapaluengo hao ambao wametinga fainali ya FA nao nawaona wakipiga Uzi wenye chata ya maziwa ya Faraj ASAS wa hukoko Iringa. Lipuli msimu uliopita walikuwa plain lakini now, tumeona jezi zikiwa na nembo ya ASAS (rejea fainali FA).

5). KMC. hawa wabishi wa kino, wamekuwa mwiba kwa ligi kuu hususan kwa vibonde na kila wanaekutana nao, kwenye nusu final ya FA niliwaona wakiwa na nembo lakini sikujua ni akina nani walokuwa wapo upande wao. Ila nna imani mafanikio yao uwanjan yanaonekena.

6). Mtibwa Sugar, hawa nadhani pia wanauwezo wa kujidhamini wenyew kama ilivyo kwa azam, so hata wakitia nembo ya mtibwa sugar kwenye kifua chao bado wapo vizur pamoja na matatizo madodgo yaliyomo.

7). Mbeya City. Hawa ndugu zetu kule kusini najua hawawezi kosa mdhamini tena naona wakipata mdhamini mkubwa ambaye ni mmoja ya kampuni kubwa ya simu za mikononi, na kupiga ktk kifua chao.

8). Tz Prison, hawa wajelajela original kutoka Mbeya. Hawa wa majeshi nadra sana kuwa na wadhamini lakini ingekuwa sawa, kutia nembo ya Tz Prison kwenye Uzi wao km ilivyo
kwa Jkt Tanzania, walivoweka nembo yao kifuani.

9). Alliance fc. Hawa wanafunzi wa kule Mwanza, wamesumbua vilivyo ligi pamoja na uchanga wao kwenye ligi, ukiacha Alliance school kwenye Uzi wao nadhan pia GF truck pamoja na mbao fc wana udhamini huo.

10). Singida Utd, hawa kampuni moja ya vinywaji isipowatia udhaminni msimu ujao basi wataanza mchakato, lakini pia kwao nyumbn Kuna mafuta ya alizeti nadhani kampuni waangalie hapo, pakutangazia biashara.

11). Biashara Utd, sasa unaingia Tarime, hawa ndugu zetu, ni muda sasa migodi ya pale(nyamongo na mingnie) nyumbani iangalie kwa jicho la tofauti kuipatia udhamini timu na kujitangaza pia wabunge wa pale najua ni wapenda michezo wataliangalia hilo.

12). Ruvu Shooting, hawa walikuwa na cow bel msimu unaoisha lakini pia wakitafuta najua watapata kuitangaza mlandizi na pwani kwa ujumla, wakiongozwa na Mwl Bwire.

13). Coastal Union, wagosi wa kaya wa mkwakwan kule tanga, kama sijakosea hawa ndo wanaongoza kwa kuchafuka wadhamini kwenye Uzi wao, ambapo kuna bin sulum,tsn,mo faya na wengine. Nadhani pia wakiongeza sio mbaya.

14). Ndanda fc, wanakuchere, pamoja na kuwa wanao ndanda spring lakini ni wakati wa mtwara na wengineo kuweka udhaminni wao, kusimam pamoja na club hii, sio tu wakiwa kwenye mafanikio ndo wawaangalie.

15). Namungo fc. Hawa najua wapo vizuri kwa juhudi za Waziri mkuu watapata udhamini mnono kuelekea msimu ujao, Naona washaanza kutunishiana misuli na timu za ligi kuu.

Pia changamoto kwa TFF msimu ujao, kuwapatia timu udhamini angalau kujikwamua na adha ndogondogo.

Nawasilisha...

screenshot_20190604-112850_1559637090023-jpeg.1117301
 
Manofu

Manofu

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2018
Messages
1,306
Points
2,000
Manofu

Manofu

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2018
1,306 2,000
Timu za tanzania ni hovyo kabisa hiv kuna timu ilikuwa na wadhamini wengi kama Singida united? Jezi yao ilikuwa imechafuka kwa nembo za wadhamini ila kukosa consistency kumeighalimu timu. Kwa upande wa TFF na Bodi ya Ligi uko wamejazana ndugu jamaa na marafiki ambao awana creativity yoyote wao kazi yao nikupiga mpunga basi. Hv ni mdhamini gani ataingia mkataba na chama ambajo mpaga ligi imeisha kilikuwa kinashindwa kujuwa ni timu zipi zinashuka daraja na zipi zinacheza play off?
 
usser

usser

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2015
Messages
11,313
Points
2,000
usser

usser

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2015
11,313 2,000

Hiv kwan singida united waliachana Na mdhamin
Wao mkuu sport pesa???

TFF pale n muozo mtupu

Africa Bora tukabak Bila mpira Na ndoo
Maana wazungu wanatudharau kila kukicha
 
usser

usser

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2015
Messages
11,313
Points
2,000
usser

usser

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2015
11,313 2,000
Cha kushangaza zaid Na hii lig
Ya tff et lig imeisha Na haijulikan
Nan ameshuka daraja Na n Nan
Anapanda lig kuu
 
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Messages
2,021
Points
2,000
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2015
2,021 2,000
Mkuu upo sahihi, viongozi wengi wanaangalia matumbo yao, Mh Sanga yy yupo na anaishi huko lakini timu IPO singida hata kujua nini kinaendelea hataki, akiulizwa anasema anakuza brand ya timu, matokeo yake hali inazidi kuwa mbaya.

Kwa upande wa bodi ya ligi na TFF wamefeli kwa mdhamini, matokeo yake wanaponda vilabu kuwa daraja lakwanza walidhaminiwa na nani.
Uongoz wa TFF huu,nauona ukiozea keko kuliko hata ule wa malinzi
Timu za tanzania ni hovyo kabisa hiv kuna timu ilikuwa na wadhamini wengi kama Singida united? Jezi yao ilikuwa imechafuka kwa nembo za wadhamini ila kukosa consistency kumeighalimu timu. Kwa upande wa TFF na Bodi ya Ligi uko wamejazana ndugu jamaa na marafiki ambao awana creativity yoyote wao kazi yao nikupiga mpunga basi. Hv ni mdhamini gani ataingia mkataba na chama ambajo mpaga ligi imeisha kilikuwa kinashindwa kujuwa ni timu zipi zinashuka daraja na zipi zinacheza play off?
 
smarte_r

smarte_r

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Messages
1,046
Points
2,000
smarte_r

smarte_r

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2013
1,046 2,000
Timu za tanzania ni hovyo kabisa hiv kuna timu ilikuwa na wadhamini wengi kama Singida united? Jezi yao ilikuwa imechafuka kwa nembo za wadhamini ila kukosa consistency kumeighalimu timu. Kwa upande wa TFF na Bodi ya Ligi uko wamejazana ndugu jamaa na marafiki ambao awana creativity yoyote wao kazi yao nikupiga mpunga basi. Hv ni mdhamini gani ataingia mkataba na chama ambajo mpaga ligi imeisha kilikuwa kinashindwa kujuwa ni timu zipi zinashuka daraja na zipi zinacheza play off?
kudorora kwa singida united kulitokana na mwigulu nchemba kuwaaminisha wanasingida kwamba angetumia ushawishi wake wa kisiasa kuifikisha mbali. hawakujua kuwa jamaa alikuwa anaitumia kwa malengo yake binafsi ya kujitengeneza image yake.

matokeo yake alipotumbuliwa kwenye nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani na timu ikaanza kushuka kiwango.

kwa sasa ipo kama vikinda vya njiwa. nina wasiwasi sijui kama itaweza ku survive kiuchumi msimu ujao.
 
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Messages
2,021
Points
2,000
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2015
2,021 2,000
Bado yupo SportPesa
Hiv kwan singida united waliachana Na mdhamin
Wao mkuu sport pesa???

TFF pale n muozo mtupu

Africa Bora tukabak Bila mpira Na ndoo
Maana wazungu wanatudharau kila kukicha
 
Turnkey

Turnkey

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Messages
4,706
Points
2,000
Turnkey

Turnkey

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2013
4,706 2,000
Stand United imeshuka daraja futa namba 15. Ila uzi mzuri .
 
MAGO

MAGO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Messages
1,416
Points
2,000
MAGO

MAGO

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2011
1,416 2,000
hao wote ni wadhamini wa vilabu siyo ligi...
 
Goodluck Mchika

Goodluck Mchika

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2018
Messages
577
Points
500
Goodluck Mchika

Goodluck Mchika

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2018
577 500
Kichwa na content havihusiani
 
Slim5

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
22,572
Points
2,000
Slim5

Slim5

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
22,572 2,000
Azam Fc yule GF Truck alikuwa maalum kwa ile Final ya ASFC tu
 
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Messages
2,021
Points
2,000
evonik

evonik

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2015
2,021 2,000
Utofauti upo, kuna mdhamini wa ligi, kuna mdhamini wa Vilabu na kuna mdhamini wa jezi, mfano vodacom alikuwa medhamini ligi nzima msimu 2017/2018, lkn pia jezi zilikuwa na nembo ya voda
hao wote ni wadhamini wa vilabu siyo ligi...
 
Forum statistics

Threads 1,336,151
Members 512,550
Posts 32,528,670
Top