Naona kuna haja ya kufanya jitihada kudhibiti maneno yanayotoka kwenye mdomo wa rais!

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Kuna wakati unaona rais akipewa taarifa na kuifanyia kazi papo hapo!
Hili linaweza kuwa jambo jema mara nyingine ila kuna wakati linaweza kuwaumiza watu!

Sijui ufikiri wa wengi kwenye hili ila kwenye nchi zetu hizi ndogondogo rais anakuwa almost 'semi-god'.
Rais alipaswa kuwa kama judge mahali fulani kwenye uongozi wake, 'sio kwa kudukua sms za watu lakini!'.
Kama kuna jambo tata la kufanyia maamuzi rais anapaswa kuzisikiliza pande zote kwa busara na kutoa uamuzi.

Mimi naona hata hao watu wanaompa taarifa mara nyingi wanaweza kumlisha matango pori tu hata bila ya wao kujua ukitegemea na hiyo taarifa wameipata wakiwa upande gani wa jambo- (Obsevars au active participants au na wao wamesikia tu kutoka watu ambao nao wanawaamini).

Rais anaweza pia kutokuingia kwenye makosa mengi ya kimaamuzi kama ataacha hierarchy (bottom-up) ifanye kazi yake. Kuharakisha kufanya maamuzi ni jambo moja na kufanya maamuzi sahihi ni jambo lingine.

Maamuzi ambayo yanaumiza watu au yanagusa maisha ya watu wengi yanapaswa yafanye kwa busara kubwa ambayo inatanguliwa na sikio linalosikia pande zote.

Tumeshuhudia watu wakifukuzwa kazi kwa maamuzi ambayo sio sahihi.
Kampuni zikisimamishwa kwa maamuzi ya kuwahi.
Watu wakifilisiwa kwa maneno tu yanayomponyoka rais.

Rais akishaongea mara nyingi kama sio mara zote ndio inakuwa mwisho wa jambo.
Waitaliano hupenda kusema "ROMA LOCUTA CAUSA FINITO". Yaani Roma ikishaongea ndio mwisho wa jambo.
Shida inakuja pale ambapo Roma inaponyokwa tu na maneno.

Tuanze kwa kusema rais aandaliwe hotuba na wakati wote aongee kilichoko kwenye hotuba.
Halafu tutafute namna ya kumbana rais afanye kazi kama taasisi na sio kujiwakilisha yeye mwenyewe tu na kutumia rasilimali zetu kujaribia mawazo yake! (Katiba mpya)

Karibu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu bwana mkubwa yupo magogoni huu unaenda mwaka wa nne, mada kama hii ya Paul sio mara ya kwanza kuja jukwaani.

Ndivyo alivyozaliwa, ndivyo alivyo. Sana sana mrejesho wa mada kama hii huwa ni matusi ambayo hayana faida yoyote.
 
Nimewahi kupata msemo huu kutoka kwa Mmarekani mmoja: you can take a man out of the bush but you can never take the bush out of a man! Au Waingereza husema: you can not teach an old dog new tricks
 
"Balozi wa Kanada ameongea Kiswahili mimi nimefarijika sana,..sasa nivizuli tuwafunze watoto wetu kilugha,Mwangaluka baba"....kudadaadek!..Kichwa inapata moto haraka sana.
 
Tuanze kwa kusema rais aandaliwe hotuba na wakati wote aongee kilichoko kwenye hotuba.
Halafu tutafute namna ya kumbana rais afanye kazi kama taasisi na sio kujiwakilisha yeye mwenyewe tu na kutumia rasilimali zetu kujaribia mawazo yake! (Katiba mpya)

Sent using Jamii Forums mobile app
Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!. - JamiiForums

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums
 
Mi nasubiri Majaliwa aendelee kujichekesha apokonywe mke nadhani ndipo ataelewa
 
Back
Top Bottom