Naombeni ushauri

CHEI CHEI

New Member
Joined
Jan 28, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Habari wakuu.

Namshukuru mungu kwa kunijaalia kujiunga na familia kubwa ya JamiiForums. Nikienda Moja kwa moja katika mada. Nilihitimu Kidato cha sita (hkl) mwaka 2011 lakn matokeo yangu hayakwa mazuri kiasi cha kutoniwezesha kwenda chuo kikuu.

Sikukata tamaa mwaka 2013 nilipata kazi sehm moja ambayo iliniwezesha kujikimu kimaisha.Sikuajiliwa Kwa cheti bali uzoefu na nia ya dhati katika kazi niliyokuwa nafanya. Baada Ya kuona nimetulia kiakili, Desemba mwaka huo niliamua kuchukua jukumu la kurudi darasani kusoma tena ili mwaka 2015,mwezi mei nifanye mtihan kama mtahiniwa binafsi. Kulitimiza Hili nilipata kituo ambacho ndicho nimejisajili kwa ajili ya kusoma na kufanya mtihani.

Mwaka 2014 mwezi wa 10 mambo hapa ofisini yalikwenda mrama kiasi ofisi ikayumba kifedha,uongozi wa juu ulitoa kauli 1 kwetu wafanyakazi,ima tuendelee kufanya kazi bila mshahara,ama tufukuzwe.Binafsi Nilichagua kuendelea na kazi hata bila mshahara.

Nina kipaji cha utangazaji na pia nilijifunza mtaani maswala ya video shooting & editing,na ndio hasa nilikuwa nafanya kazi hyo katika moja ya local tv cable station hapa jijini kwetu.

jambo linaloniwia ugumu kwa sasa hata niombe ushauri ni hili;

nimepanga na sina familia japo nina mama yangu ambae ni mgonjwa wa figo kwa sasa.Natakiwa Nimuhudumie na pia kujikimu mwenyewe kimaisha, hadi sasa sijielew nifanye nini maana ninaangaika kutafuta walau kibarua cha kujishkiza sehemu sijapata.

Natumia muda mwingi kuwaza ninatokaje kimaisha kiasi sipat hata muda wa kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mtihan ambao utafanyika mei mwaka huu 2015.

Najiuliza nifanye mtihan ama nihairishe tu hadi pale nitakapokuja kupata ajira?

Naombeni ushauri ndugu zangu na mwenyez mungu akulipen kwa kile ambacho mtanishauri..

Nawasilisha
 
Pole sana kwa matatizo CHEI CHEI ndio ukubwa huo.
Pia pole kwa kuuguliwa na mama, mimi ushauri wangu ni wewe mwenyewe, ujipime kama utaweza kumudu kufanya mitihani.
Maana kujiandaa na kuufanya huo mtihani niwewe mwenyewe.

Kwahiyo kaa na ujipime pamoja na yote uyapitiayo je utaweza?
Nakutakia kila la kheri na Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi, kwa kila ufanyalo.
Mama naye namuombea apate nafuu.
 
Last edited by a moderator:
naomba ntajie kituo cha tv hiko unachofanya kazi bila mshahara
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…