Naombeni ushauri wenu nimsaidie jamaa

Naombeni ushauri wenu nimsaidie jamaa

Huyo rafiki yako ni Boya ningekuwa ni mimi kwanza ningemchezesha na vibao kadhaa

Inawezekana kabisa hata ujio wa huyo mwanamke umechangiwa na yeye na hilo swala la mwenyekiti limewekwa kuficha aibu tu.
Ni mtu asiyeweza kujisimamia..
 
Achana nao ndugu yangu,cha kwanza tu kama jamaa yako yupo serious angeitaarifu police kuwa muhalifu karudi akamatwe akajibu mashtaka yake .Kaa nao mbali huyo mwanamke siyo wa kawaida.kimoyo moyo Mpe mkono wa Buriani rafiki yako.
Ndicho nilitegemea kukiskia mwanzoni
Duh ..huruma !!
 
Hi ni hatari Sana,
1. Ampime kwanza HIV,
Huenda keshaukwaa uko, anatafuta pa kuugulia ili afe kwa heshima.

2. Kingine awashirikishe wazazi wa mwanamke, na arudi kwao kwa mda mpk akili yake itakapotulia na kujutia makosa yake.

Mwanamke Akigoma jamaa atoke Kama alivyo amwachie nyumba akapange,matunzo atakua anapeleka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu ..nitamwambia
 
Me siamini kwenye ulkufungana kwa ushirikina ila yote kwa yote ndoa ya kikristo ni mtihan kwa kweli yaaani mwanamke atoke kweny ndoa yake akazae kwengine uko halaf anarud kimya kimya kama kuna kitu hakijatokea vile me ningepiga mabapa ya mapanga kuanzi uyo mwenye kiti wa kitongoj pmj na uyo malaya na wote ningesabia dakik 5 t wote wapotee kwa nyumb yng 😂😂😂
 
Kwa kuwa watoto wa jamaa hawakai apo aache kutoa pesa ya matumizi , asile chakul chochote kinachopikwa na huyo mwanamke na mwisho akatoe taarifa polisi mtuhumiwa kaonekana
 
Kwa mazingira hayo c bure asee hpo jamaa ndo kwisha hachomoki tena maana mwanamke mkiachana kwa mazingira kama hyo af akaenda huko Maisha yakampiga ni kosa kubwa kurudiana nae ndo mana lazma akukamate kwanza maana ili usiskie ushauri wwte na ukimshauri chchte kuhusu huyo mwanamke basi jamaa anaenda kwambia huyo mwanamke
 
Fanya yako, asikushughulishe, huyo ni mshamba wa mapenzi, kuna hatua aliiruka kwenye mambo ya mapenzi yaani apende mtu kiasi jitu limetoroka yeye anakonda😂
 
Habari zenu wakuu.

Naomba niende mojakwamoja kwenye mada husika, ni story ndefu lakini nitajaribu kuifupisha.

Ni Mfanyakazi mwenzangu, nilishiriki kwenye zoezi zima la kumposa mkewe, mahari na sendoff kasoro ndoa sikuhudhuria kwakua walifungia mkoani na ilikua ya kibinafsi yaani hakutaka iwe kubwa wakati huo binti akiwa na ujauzito wa mtoto wao wakwanza 2016. Kiufupi kwangu ni kama ndugu yangu.

Wameishi na mkewe vizuri na kubahatika kupata mtoto mwingine, jumla wana watoto wawili. Sikumbuki vizuri ni lini ndoa ilianza kutetereka lakini mwisho wa siku yule mkewe akawa na wanaume wengine, dharau kwa jamaa, na mbaya zaidi mwanamke huyo akatelekeza familia kwa kuwaacha watoto na kutoroka kusikojulikana.

Huku nyuma akimuachia jamaa madeni makubwa mno mtaani (ilifika hatua huyo mwanamke aliweka nyumba yao rehani bila jamaa kujua), na pia aliondoka na kiasi kikubwa sana cha pesa ambayo walikua wameweka kwa kazi flani (walikua wanaendelea na ujenzi wa nyumba yao).

Jamaa alikonda mno, akawa na msongo mkubwa sana wa mawazo kiasi kwamba hata chakula alikua hali. Ilifika hatua ambayo ni kama alikua anaenda kuwehuka (alimpenda sana huyo mwanamke). Ikafika mahali jamaa anataka kuacha kazi na kurudi nyumbani kwao Ili kukwepa aibu aliyomuachia mkewe huyo (wakati huo watoto kapeleka nyumbani kwao wanalelewa na dada yake, hadi muda huu ninavyoandika hapa watoto wapo huko).

baada ya kuona hali hiyo binafsi niliumia sana, nilimwita nikazungumza naye na kumuelekeza mambo anayopaswa kuyafanya kwa kipindi kile, ikiwa ni pamoja na kuacha kulipa madeni ya huyo mwanamke.

Akaripoti kituo cha police kwamba mkewe katoroka, na katoroka na kiasi flani cha pesa ikibidi azidishe hiyo pesa ili mwisho wa siku akija kudai mali basi kwanza alipe pesa aliyochukua wakati anatoroka.

Mimi na yeye tukawa tumeishia hapo na mrejesho ukaja kwamba alienda kuripoti. Baada ya muda kupita jamaa akarudi kwenye hali yake ya awali na akanenepa zaidi ya vile alivyokuwa na yule mwanamke (lakini wakati huu wote habari zilizokuwepo ni kuwa huyo mwanamke alikua anaishi mkoa mwingine na mwanaume mwingine).

Sasa basi kilichonifanya nije hapa kuomba ushauri ni iki;

Mwanamke yule amerudi yupo kwa jamaa anamtoto mdogo wa miezi wa mwanaume mwingine (amedai kwamba pale ni kwake hivyo amerudi kwa kuletwa na mwenyekiti wa kitongoji akidai eti bado ni mkewe na jamaa kampokea).

Kwa taarifa nilizonazo nimeskia pembeni kwamba jamaa anasema hawakai chumba kimoja lakini matumizi ya ndani jamaa ananunua (mwanamke ni mama wa nyumbani), na kwasasa huyo mwanamke anadai familia irudi, yaani watoto wake na hivi ninavyoandika jamaa anakarabati nyumba.

Maswali yangu;

1. Hivi hilo jambo alilofanya jamaa la kumpokea huyo mwanamke pamoja na yote alomfanyia ni sahihi?

2. Huyo mwenyekiti wa kitongoji alichofanya ni sahihi?

3. Sheria ya ndoa inasemaje hapo, bado kuna ndoa?

4. Vipi sheria ya dini ya kikristo, nayo inaruhusu hayo? Bado hapo kuna ndoa?

Kiukweli mimi imeniuma japo siyo ndugu yangu na bado hajaniita kuniambia lolote, lakini binafsi nahisi ni kama ushirikina umetumika huyo mwanamke kurudi (ni tetesi zilizopo kuwa mama wa binti anajihusisha na hayo mambo ya ushirikina).

Wadau kwa kuzingatia hayo maswali manne hapo juu, naombeni ushauri wenu, nawezaje kumnasua huyu jamaa kwenye hili? Naona kama anaenda kupotea tena, kwasababu isingekuwa mimi na baadhi ya watu mwanzoni wa haya majanga yake pengine tungeshamsahau. Sasa naona anataka kurudi kulekule alipotoka! Nahitaji nimwuite tena nizungumze naye.

Je nitamueleza nini, au nyie watu wazima humu mnanishaurije?

Mawazo yenu naomba tafadhali.

ASANTENI.
Ongea na rfk ako anaweza hata amuue huyo mtoto mdg
Ila mim ningekua huyo rfk ako huyo manzi ningemfanyia tukio maisha yake yote asingesahau
 
Hapo sio kuuliza ni uchawi umetumika muokoe jamaa ako kwenye hilo janga
 
Waache na maisha yao mkuu, aliliae wembe acha umkate,

Nna jirani yangu hapa mhaya kaoa mkinga adi namuonea huruma, ndoa ina mwaka tu jamaa anaenda kazini na daladala wakati ana gari kulitumia adi atoke na mkewe,
Wakienda wageni wa mume anakaa nao nje chakula kikiiva anamletea mmewe tu jamaa kapoa hadi namuonea huruma, yaan marafiki zake ni dada wa kazi na mtoto wa kaka yake anaishi nae japo ananyanaswa sana, mkewe akitoka ndio unamskia akipiganao stori na kucheka nao kwa tahadhari.... Namhurumia sana jamaa lkn ndio ivo
 
Back
Top Bottom