Naombeni ushauri wenu nimsaidie jamaa

Naombeni ushauri wenu nimsaidie jamaa

Too face

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
223
Reaction score
199
Habari zenu wakuu.

Naomba niende mojakwamoja kwenye mada husika, ni story ndefu lakini nitajaribu kuifupisha.

Ni Mfanyakazi mwenzangu, nilishiriki kwenye zoezi zima la kumposa mkewe, mahari na sendoff kasoro ndoa sikuhudhuria kwakua walifungia mkoani na ilikua ya kibinafsi yaani hakutaka iwe kubwa wakati huo binti akiwa na ujauzito wa mtoto wao wakwanza 2016. Kiufupi kwangu ni kama ndugu yangu.

Wameishi na mkewe vizuri na kubahatika kupata mtoto mwingine, jumla wana watoto wawili. Sikumbuki vizuri ni lini ndoa ilianza kutetereka lakini mwisho wa siku yule mkewe akawa na wanaume wengine, dharau kwa jamaa, na mbaya zaidi mwanamke huyo akatelekeza familia kwa kuwaacha watoto na kutoroka kusikojulikana.

Huku nyuma akimuachia jamaa madeni makubwa mno mtaani (ilifika hatua huyo mwanamke aliweka nyumba yao rehani bila jamaa kujua), na pia aliondoka na kiasi kikubwa sana cha pesa ambayo walikua wameweka kwa kazi flani (walikua wanaendelea na ujenzi wa nyumba yao).

Jamaa alikonda mno, akawa na msongo mkubwa sana wa mawazo kiasi kwamba hata chakula alikua hali. Ilifika hatua ambayo ni kama alikua anaenda kuwehuka (alimpenda sana huyo mwanamke). Ikafika mahali jamaa anataka kuacha kazi na kurudi nyumbani kwao Ili kukwepa aibu aliyomuachia mkewe huyo (wakati huo watoto kapeleka nyumbani kwao wanalelewa na dada yake, hadi muda huu ninavyoandika hapa watoto wapo huko).

baada ya kuona hali hiyo binafsi niliumia sana, nilimwita nikazungumza naye na kumuelekeza mambo anayopaswa kuyafanya kwa kipindi kile, ikiwa ni pamoja na kuacha kulipa madeni ya huyo mwanamke.

Akaripoti kituo cha police kwamba mkewe katoroka, na katoroka na kiasi flani cha pesa ikibidi azidishe hiyo pesa ili mwisho wa siku akija kudai mali basi kwanza alipe pesa aliyochukua wakati anatoroka.

Mimi na yeye tukawa tumeishia hapo na mrejesho ukaja kwamba alienda kuripoti. Baada ya muda kupita jamaa akarudi kwenye hali yake ya awali na akanenepa zaidi ya vile alivyokuwa na yule mwanamke (lakini wakati huu wote habari zilizokuwepo ni kuwa huyo mwanamke alikua anaishi mkoa mwingine na mwanaume mwingine).

Sasa basi kilichonifanya nije hapa kuomba ushauri ni iki;

Mwanamke yule amerudi yupo kwa jamaa anamtoto mdogo wa miezi wa mwanaume mwingine (amedai kwamba pale ni kwake hivyo amerudi kwa kuletwa na mwenyekiti wa kitongoji akidai eti bado ni mkewe na jamaa kampokea).

Kwa taarifa nilizonazo nimeskia pembeni kwamba jamaa anasema hawakai chumba kimoja lakini matumizi ya ndani jamaa ananunua (mwanamke ni mama wa nyumbani), na kwasasa huyo mwanamke anadai familia irudi, yaani watoto wake na hivi ninavyoandika jamaa anakarabati nyumba.

Maswali yangu;

1. Hivi hilo jambo alilofanya jamaa la kumpokea huyo mwanamke pamoja na yote alomfanyia ni sahihi?

2. Huyo mwenyekiti wa kitongoji alichofanya ni sahihi?

3. Sheria ya ndoa inasemaje hapo, bado kuna ndoa?

4. Vipi sheria ya dini ya kikristo, nayo inaruhusu hayo? Bado hapo kuna ndoa?

Kiukweli mimi imeniuma japo siyo ndugu yangu na bado hajaniita kuniambia lolote, lakini binafsi nahisi ni kama ushirikina umetumika huyo mwanamke kurudi (ni tetesi zilizopo kuwa mama wa binti anajihusisha na hayo mambo ya ushirikina).

Wadau kwa kuzingatia hayo maswali manne hapo juu, naombeni ushauri wenu, nawezaje kumnasua huyu jamaa kwenye hili? Naona kama anaenda kupotea tena, kwasababu isingekuwa mimi na baadhi ya watu mwanzoni wa haya majanga yake pengine tungeshamsahau. Sasa naona anataka kurudi kulekule alipotoka! Nahitaji nimwuite tena nizungumze naye.

Je nitamueleza nini, au nyie watu wazima humu mnanishaurije?

Mawazo yenu naomba tafadhali.

ASANTENI.
 
Habari zenu wakuu..

Naomba niende mojakwamoja kwenye mada husika..ni story ndefu lakini nitajaribu kuifupisha..

Ni Mfanyakazi mwenzangu.
Nilishiriki kwenye zoezi Zima la kumposa mkewe,mahari na sendoff kasoro Ndoa sikuhudhuria kwakua walifungia mkoani na ilikua private yaani hakutaka iwe kubwa wakati huo bint akiwa na ujauzito WA mtoto wao wakwanza 2016.
kiufupi kwangu ni kama ndugu yangu..

Wameishi na mkewe vizuri na kubahatika kupata mtoto mwingine jumla wanawatoto wawili.

Sikumbuki vizuri ni lini ndoa ilianza kutetereka lakini mwisho wa siku yule mkewe akawa na wanaume wengine ,dharau Kwa jamaa,na mbaya zaidi mwanamke huyo akatelekeza familia Kwa kuwaacha watoto na kutoroka KUSIKOJULIKANA huku nyuma akimuachia jamaa madeni makubwa mno mtaani(ilifika hatua huyo mwanamke aliweka nyumba Yao bond bila jamaa kujua)...na pia aliondoka na kiasi kikubwa sana Cha pesa ambayo walikua wameweka Kwa kazi flani(walikua wanaendelea na ujenzi wa nyumba Yao)

Jamaa alikonda mno akawa na msongo mkubwa sana wa mawazo kiasi kwamba hata chakula alikua Hali,ilifika stage ambayo ni kama alikua anaenda kuwehuka(alimpenda sana huyo mwanamke) ...ikafika mahali jamaa anataka KUACHA kazi na kurudi nyumbani kwao Ili kukwepa aibu aliyomuachia mkewe huyo,(wakati huo watoto kapeleka nyumbani kwao wanalelewa na dada yake..hadi muda huu ninavyoandika hapa watoto wapo huko)

baada ya kuona Hali hiyo binafsi niliumia sana nilimwita,nikazungumza naye na kumuelekeza mambo anayopaswa kuyafanya Kwa kipindi kile,ikiwa ni pamoja na KUACHA kulipa madeni ya huyo mwanamke.
2.AKARIPOTI kituo Cha police kwamba mkewe katoroka ,na katoroka na kiasi flani Cha pesa ikibidi azidishe hiyo pesa Ili mwisho wa siku akija kudai Mali basi kwanza alipe pesa aliyochukua wakati anatoroka.

Mimi na yeye tukawa tumeishia hapo na mrejesho ukaja kwamba ALIENDA KURIPOTI.

Baada ya muda kupita jamaa akarudi kwenye Hali yake ya AWALI na akanenepa zaidi ya vile alivyokuwa na yule mwanamke...( Lakini wakati huu wote habari zilizokuwepo ni kuwa huyo mwanamke alikua anaishi mkoa mwingine na mwanaume mwingine)

Sasa basi kilichonifanya nije hapa kuomba ushauri ni Hiki

Mwanamke yule amerudi yupo Kwa jamaa ANAMTOTO MDOGO WA MIEZI WA MWANAUME MWINGINE(Amedai kwamba pale ni kwake hivyo amerudi Kwa kuletwa na mwenyekiti wa kitongoji akidai et bado ni mkewe na jamaa kampokea.( Kwa taarifa nilizonazo nimeskia pembeni kwamba jamaa anasema hawakai chumba kimoja lakini matumizi ya ndani jamaa ananunua .(mwanamke ni mama wa nyumbani)na kwasasa huyo mwanamke anadai familia irudi Yani watoto wake na hivi ninavyoandika jamaa anakarabati nyumba.

Maswali yangu..

1.hivi Hilo jambo alilofanya jamaa la kumpokea huyo mwanamke pamoja na yote alomfanyia ni SAHIHI?

2.HUYO mwenyekiti wa kitongoji alichofanya ni SAHIHI?

3.SHERIA ya ndoa inasemaje HAPO BADO KUNA NDOA?

4.vipi SHERIA YA DINI YA KIKRISTO nayo inaruhusu hayo ? Bado hapo Kuna ndoa?

Kiukweli Mimi imeniuma japo si ndugu yangu na bado hajaniita kuniambia lolote lakini binafsi nahisi ni kama ushirikina umetumika huyo mwanamke kurudi(ni tetesi zilizopo kuwa mama wa Binti anajihusisha na hayo mambo ya ushirikina)

Wadau Kwa kuzingatia hayo maswali manne hapo juu
Naombeni ushauri wenu NAWEZAJE KUMNASUA HUYU JAMAA KWENYE HILI? Naona kama anaenda kupotea tena..
KWA sababu isingekua ni Mimi na baadhi ya watu mwanzoni wa haya majanga yake pengine tungeshamsahau... Sasa naona anataka kurudi kulekule alipotoka...

Nahitaji nimwite tena nizungumze naye..
Je nitamueleza Nini ...
Au nyie watu wazima humu mnanishaurije...

Mawazo yenu naomba please..

ASANTENI.
Itakua huyo bibie Ni mtamu Sana au ndo alimtoa wenge
 
Aisee muite mwambie ukweli, tena nwambie huyo mwanamke kakufunga wapigie ndugu zake wambie na huyo dada aliekuwa anakaa na mtoto,
Tafadhali usimuache jamaa apotee
Maana kama siku hiyo dawa inaisha nguvu anaweza kwenda jela kwa kosa la kuua maana huyo mwanamke hiyo siku atakosea atamkumbuka makosa yake yote.
 
Achana nao ndugu yangu,cha kwanza tu kama jamaa yako yupo serious angeitaarifu police kuwa muhalifu karudi akamatwe akajibu mashtaka yake .Kaa nao mbali huyo mwanamke siyo wa kawaida.kimoyo moyo Mpe mkono wa Buriani rafiki yako.
 
Habari zenu wakuu.

Naomba niende mojakwamoja kwenye mada husika, ni story ndefu lakini nitajaribu kuifupisha.

Ni Mfanyakazi mwenzangu, nilishiriki kwenye zoezi zima la kumposa mkewe, mahari na sendoff kasoro ndoa sikuhudhuria kwakua walifungia mkoani na ilikua ya kibinafsi yaani hakutaka iwe kubwa wakati huo binti akiwa na ujauzito wa mtoto wao wakwanza 2016. Kiufupi kwangu ni kama ndugu yangu.

Wameishi na mkewe vizuri na kubahatika kupata mtoto mwingine, jumla wana watoto wawili. Sikumbuki vizuri ni lini ndoa ilianza kutetereka lakini mwisho wa siku yule mkewe akawa na wanaume wengine, dharau kwa jamaa, na mbaya zaidi mwanamke huyo akatelekeza familia kwa kuwaacha watoto na kutoroka kusikojulikana.

Huku nyuma akimuachia jamaa madeni makubwa mno mtaani (ilifika hatua huyo mwanamke aliweka nyumba yao rehani bila jamaa kujua), na pia aliondoka na kiasi kikubwa sana cha pesa ambayo walikua wameweka kwa kazi flani (walikua wanaendelea na ujenzi wa nyumba yao).

Jamaa alikonda mno, akawa na msongo mkubwa sana wa mawazo kiasi kwamba hata chakula alikua hali. Ilifika hatua ambayo ni kama alikua anaenda kuwehuka (alimpenda sana huyo mwanamke). Ikafika mahali jamaa anataka kuacha kazi na kurudi nyumbani kwao Ili kukwepa aibu aliyomuachia mkewe huyo (wakati huo watoto kapeleka nyumbani kwao wanalelewa na dada yake, hadi muda huu ninavyoandika hapa watoto wapo huko).

baada ya kuona hali hiyo binafsi niliumia sana, nilimwita nikazungumza naye na kumuelekeza mambo anayopaswa kuyafanya kwa kipindi kile, ikiwa ni pamoja na kuacha kulipa madeni ya huyo mwanamke.

Akaripoti kituo cha police kwamba mkewe katoroka, na katoroka na kiasi flani cha pesa ikibidi azidishe hiyo pesa ili mwisho wa siku akija kudai mali basi kwanza alipe pesa aliyochukua wakati anatoroka.

Mimi na yeye tukawa tumeishia hapo na mrejesho ukaja kwamba alienda kuripoti. Baada ya muda kupita jamaa akarudi kwenye hali yake ya awali na akanenepa zaidi ya vile alivyokuwa na yule mwanamke (lakini wakati huu wote habari zilizokuwepo ni kuwa huyo mwanamke alikua anaishi mkoa mwingine na mwanaume mwingine).

Sasa basi kilichonifanya nije hapa kuomba ushauri ni iki;

Mwanamke yule amerudi yupo kwa jamaa anamtoto mdogo wa miezi wa mwanaume mwingine (amedai kwamba pale ni kwake hivyo amerudi kwa kuletwa na mwenyekiti wa kitongoji akidai eti bado ni mkewe na jamaa kampokea).

Kwa taarifa nilizonazo nimeskia pembeni kwamba jamaa anasema hawakai chumba kimoja lakini matumizi ya ndani jamaa ananunua (mwanamke ni mama wa nyumbani), na kwasasa huyo mwanamke anadai familia irudi, yaani watoto wake na hivi ninavyoandika jamaa anakarabati nyumba.

Maswali yangu;

1. Hivi hilo jambo alilofanya jamaa la kumpokea huyo mwanamke pamoja na yote alomfanyia ni sahihi?

2. Huyo mwenyekiti wa kitongoji alichofanya ni sahihi?

3. Sheria ya ndoa inasemaje hapo, bado kuna ndoa?

4. Vipi sheria ya dini ya kikristo, nayo inaruhusu hayo? Bado hapo kuna ndoa?

Kiukweli mimi imeniuma japo siyo ndugu yangu na bado hajaniita kuniambia lolote, lakini binafsi nahisi ni kama ushirikina umetumika huyo mwanamke kurudi (ni tetesi zilizopo kuwa mama wa binti anajihusisha na hayo mambo ya ushirikina).

Wadau kwa kuzingatia hayo maswali manne hapo juu, naombeni ushauri wenu, nawezaje kumnasua huyu jamaa kwenye hili? Naona kama anaenda kupotea tena, kwasababu isingekuwa mimi na baadhi ya watu mwanzoni wa haya majanga yake pengine tungeshamsahau. Sasa naona anataka kurudi kulekule alipotoka! Nahitaji nimwuite tena nizungumze naye.

Je nitamueleza nini, au nyie watu wazima humu mnanishaurije?

Mawazo yenu naomba tafadhali.

ASANTENI.
Huyo amekuja kumuua rafiki ako! Msaidieni vinginevyo mtamzika na mali zote zitapotea za jamaa
 
Hi ni hatari Sana,
1. Ampime kwanza HIV,
Huenda keshaukwaa uko, anatafuta pa kuugulia ili afe kwa heshima.

2. Kingine awashirikishe wazazi wa mwanamke, na arudi kwao kwa mda mpk akili yake itakapotulia na kujutia makosa yake.

Mwanamke Akigoma jamaa atoke Kama alivyo amwachie nyumba akapange,matunzo atakua anapeleka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee muite mwambie ukweli, tena nwambie huyo mwanamke kakufunga wapigie ndugu zake wambie na huyo dada aliekuwa anakaa na mtoto,
Tafadhali usimuache jamaa apotee
Maana kama siku hiyo dawa inaisha nguvu anaweza kwenda jela kwa kosa la kuua maana huyo mwanamke hiyo siku atakosea atamkumbuka makosa yake yote.
Sawa mkuu nitafanya hivyo.thanks
 
Back
Top Bottom