Naombeni ushauri wazo la biashara

Haematology

Member
Jan 7, 2019
18
9
Habarini za majukumu ndugu zangu?

Mimi ni mwajiriwa katika moja ya sekta binafsi. Sijaridhika na hela ya mshahara ninayopata, nimejitahidi kuweka akiba kila mwezi hadi sasa nina kama 800,000.

Natamani kuanza kufanya biashara sema kila wazo ninalofikilia naliona sio sawa. Pia napata hofu kuhusu makato ya kodi ya TRA na sehemu nyingine zinazohitaji makato na ushuru.

Naombeni ushauri kwa wazoefu wa biashara.
 
Mkuu hapo kwanza uwe na leseni ya biashara then mengine watakuja wajuvi. Au kama vipi lima tu boss
 
- fungua biashara ambayo haitakuhitaji udaiwe kodi, leseni, ushuru na vibali vyovyote kutoka mamlaka husika ili uweze kukuza mtaji wako na hatimaye baadae ndo ufungue biashara yenye anuani na vibali rasmi.
Mf: Banda la chips, kibanda cha matunda, kiosk
- Kama utakuwa na uhitaji wa kuwa na mtu wa kukusimamia biashara yako, epuka kuweka ndugu na marafiki na jitahidi uwe na muda mwingi kufuatilia biashara yako hasa katika kipindi hiki ambacho unaanza
- Epuka kuwajulisha au kuomba ushauri kwa watu wa karibu wanaokujua kuhusu hili unalotaka kulifanya. Tumia mitandao kama hii ambapo ni vigumu kujuana.
- Wazo la biashara litokane na unayopenda kuyafanya, unayoyaweza, unayoyaamini (hata kama hujawahi kuyafanya), yanayowezekana na unayotamani kuyafanya kuliko kuangalia kitu gani kinalipa na wewe ufanye au kuangalia flani anafanya nini na wewe uige ufanye.
- Kila la kheri, mtaji ulionao unatosha sana kuanza safari yako ya kujiajiri. Tegemea changamoto na vikwazo lakini visikurudishe nyuma.
 
Kiukweli sijasoma maelezo yako nimesom kichwa cha habar tuu point yangu au ushauri wangu biashara huwez kupewa idea IPI ufanye coz biashara ni interest yako ...in short its like this " kitu ulicho na interest nacho kwenye maisha yako ya kila siku ndo wazo lako la biashara usitafute wazo .look on ur interest and take a step " nasem hivi kwasabb utakifanya kwa passion and love coz unakipnda hta kwa kukiangalia ....am out good luck
 
Back
Top Bottom