Mkuu usije ukakubali kuingia huo mtego. That is deadly. Mpaka sasa ushafanya damage kubwa kwenye urafiki wenu.
Chondechonde, kama hii habari ni ya kweli na sio ya kutunga, then nakushauri hilo wazo la kumgegeda shemejio uliondoe kabisa.
Kwasasa hakikisha huendi hapo nyumbani kwa rafiki yako kama mume wake hayupo. Pia epuka kuwa faragha (sehemu isiyo ya wazi) naye popote pale.
Hata kama kumetokea tatizo hapo nyumbani kwake, unaweza kulitatua bila wewe kwenda physically. Tumia hata hela ikibidi kwa kutuma fundi au mtu yeyote. Toa visingizio vya kushindwa kwenda hata kama rafikio atakuomba yeye mwenyewe uende.
Ukienda kuna siku anaweza hata apige makelele kuwa umembaka au unataka kumbaka. Bora urafiki wenu ufe kwa yeye kukuzushia uongo lakini sio kwa kufanya kweli. Mwishowe ukweli utakuweka huru. Acha mazoea kabisa na huyo mwanamke. Hajui anachokifanya...anasukumwa na nyege. Au labda kuna kitu hakimfurahishi kwa upande wa mumewe na hivyo anataka kumkomoa au kulipiza. In that state anakuwa hajali matokeo.
Hata hao wadogo zake achana nao...au oa mmoja wa hao ingawa inaweza pia isababishe bifu kati yao ambalo linaweza kukuletea stress zisizo na ulazima. Be careful bro!!!!