Naombeni Ushauri Nifanyeje

Naombeni Ushauri Nifanyeje

Yaani ulitumia fursa ulitumia fursa ya kuaminiwa na mjomba kama kichaka cha kufanyia mambo yako mabaya huku ukijua wazi kuwa ni mabaya. Yaani ulishindwa kabisa kwenda kuwinda huko porini hadi ukaamua kuwinda mifugo ya mjomba? Kibaya zaidi ni kuwa unaishi kwake!
 
Ulivokuwa unamgalagaza binamu yako kwa bed, unamkunja bila hata ndomu mbona hukuja kusema huku
 
mkuu huyo ni dada yako, na umeamua kumpa mimba makusudi maana ungepita nae siku moja ningekutetea kuwa ulizidiwa ila miezi 8? mkuu kaongee na mama yako na umweleze bayana ili yeye akamkabili kaka yake
 
mkuu huyo ni dada yako, na umeamua kumpa mimba makusudi maana ungepita nae siku moja ningekutetea kuwa ulizidiwa ila miezi 8? mkuu kaongee na mama yako na umweleze bayana ili yeye akamkabili kaka yake
ahsante mkuu
 
Hiyo ID yako jina lako ni kama vile ni mkurya na kama ni ndio basi kama unavyojua mila na desturi zetu unaruhusiwa kuona mtoto wa mjomba ila wa shangaz ndio haruhusiwi kwa hyo vuta jiko chap kidogo kijana
 
kama ulikua unajua mjomba anakuamini kiasi icho na hutaki kummumiza kwanini ulianzisha mahusiano ma binti yake?
oa tu mzee hamna namna hapo
 
Kula nguruwe sawa ila sasa uchague aliyenona!! Vipi ndugu yangu binamu yetu anachura wakusisimua?
 
Mimi nimekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na dada yangu binamu tangu mwezi wa nne mwaka huu. Huyo dada yangu binamu ni binti wa mjomba wangu.

Sasa, kwa kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi ni wa muda mrefu kidogo (kutoka mwezi wa 4 hadi mwezi huu wa 12 ni sawa na miezi 8 katika uhusiano huo) jana dada binamu alikuwa analalamika tumbo linamuuma. Nikampeleka hospitali na pikipiki, alipopimwa, daktari akaniambia kwamba dada yangu binamu ni mjamzito! Mimi nikajua wazi kwamba ujauzito huo lazima nimempa mimi.

Mjomba wangu, yaani, baba wa dada yangu binamu niliwahi kumsikia kwa masikio yangu akisema kwamba ana mpango wa kumwendeleza binti yake huyo kielimu. Na mimi ndio tayari nimeshampa mimba binti yake huyo na mpaka sasa mjomba hajajua kwamba binti yake ni mjamzito na kwamba huo ujauzito nimempa mimi.

Mjomba siku zote ananiamini sana na hawazi kabisa kwamba ipo siku naweza kumtendea jambo lolote baya. Aliwahi kuniambia waziwazi kwamba hakuna mtu anayemuamini kuliko anavyoniamini mimi. Ni kweli ananiamini sana maana hata akisafiri funguo za nyumbani kwake huwa ananiachia mimi na funguo zingine anamwachia mkewe.

Hofu yangu kubwa ni kwamba mjomba atanielewaje atakapojua kwamba binti yake ni mjamzito na ujauzito huo nimempa mimi maana mjomba ananiamini sana kwa kweli. Yaani, niko kama nimechanganyikiwa sasa hivi maana sijui ni nini nifanye. Mjomba ananiamini sana na malengo yake ya kumwendeleza binti yake kielimu nimeyaharibu kabisa kwa kumpa binti yake huyo mimba.
Watu Kama wewe ndo mnafanya wanaume watukanwe na waonekane Kama watoto wasiofikiria kesho, hukujua Kama binamu yako anaweza kuzaa?
 
Hiyo ID yako jina lako ni kama vile ni mkurya na kama ni ndio basi kama unavyojua mila na desturi zetu unaruhusiwa kuona mtoto wa mjomba ila wa shangaz ndio haruhusiwi kwa hyo vuta jiko chap kidogo kijana
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri mzuri mura!
 
Ungekuwa karibu ningekuzaba kofi moja ujikojolee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom