Naombeni Ushauri Nifanyeje

Naombeni Ushauri Nifanyeje

amatolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2017
Posts
690
Reaction score
713
Mimi nimekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na dada yangu binamu tangu mwezi wa nne mwaka huu. Huyo dada yangu binamu ni binti wa mjomba wangu.

Sasa, kwa kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi ni wa muda mrefu kidogo (kutoka mwezi wa 4 hadi mwezi huu wa 12 ni sawa na miezi 8 katika uhusiano huo) jana dada binamu alikuwa analalamika tumbo linamuuma. Nikampeleka hospitali na pikipiki, alipopimwa, daktari akaniambia kwamba dada yangu binamu ni mjamzito! Mimi nikajua wazi kwamba ujauzito huo lazima nimempa mimi.

Mjomba wangu, yaani, baba wa dada yangu binamu niliwahi kumsikia kwa masikio yangu akisema kwamba ana mpango wa kumwendeleza binti yake huyo kielimu. Na mimi ndio tayari nimeshampa mimba binti yake huyo na mpaka sasa mjomba hajajua kwamba binti yake ni mjamzito na kwamba huo ujauzito nimempa mimi.

Mjomba siku zote ananiamini sana na hawazi kabisa kwamba ipo siku naweza kumtendea jambo lolote baya. Aliwahi kuniambia waziwazi kwamba hakuna mtu anayemuamini kuliko anavyoniamini mimi. Ni kweli ananiamini sana maana hata akisafiri funguo za nyumbani kwake huwa ananiachia mimi na funguo zingine anamwachia mkewe.

Hofu yangu kubwa ni kwamba mjomba atanielewaje atakapojua kwamba binti yake ni mjamzito na ujauzito huo nimempa mimi maana mjomba ananiamini sana kwa kweli. Yaani, niko kama nimechanganyikiwa sasa hivi maana sijui ni nini nifanye. Mjomba ananiamini sana na malengo yake ya kumwendeleza binti yake kielimu nimeyaharibu kabisa kwa kumpa binti yake huyo mimba.
 
Nyege nyegezi hadi kwa mtoto wa kaka wa mama ako.Mueleze Mama ako halafu yeye ndo atamueleza Mjomba wako,kwakuwa wao ni ndugu bhasi watayamaliza vizuri.
 
Mimi nimekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na dada yangu binamu tangu mwezi wa nne mwaka huu. Huyo dada yangu binamu ni binti wa mjomba wangu.

Sasa, kwa kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi ni wa muda mrefu kidogo (kutoka mwezi wa 4 hadi mwezi huu wa 12 ni sawa na miezi 8 katika uhusiano huo) jana dada binamu alikuwa analalamika tumbo linamuuma. Nikampeleka hospitali na pikipiki, alipopimwa, daktari akaniambia kwamba dada yangu binamu ni mjamzito! Mimi nikajua wazi kwamba ujauzito huo lazima nimempa mimi.

Mjomba wangu, yaani, baba wa dada yangu binamu niliwahi kumsikia kwa masikio yangu akisema kwamba ana mpango wa kumwendeleza binti yake huyo kielimu. Na mimi ndio tayari nimeshampa mimba binti yake huyo na mpaka sasa mjomba hajajua kwamba binti yake ni mjamzito na kwamba huo ujauzito nimempa mimi.

Mjomba siku zote ananiamini sana na hawazi kabisa kwamba ipo siku naweza kumtendea jambo lolote baya. Aliwahi kuniambia waziwazi kwamba hakuna mtu anayemuamini kuliko anavyoniamini mimi. Ni kweli ananiamini sana maana hata akisafiri funguo za nyumbani kwake huwa ananiachia mimi na funguo zingine anamwachia mkewe.

Hofu yangu kubwa ni kwamba mjomba atanielewaje atakapojua kwamba binti yake ni mjamzito na ujauzito huo nimempa mimi maana mjomba ananiamini sana kwa kweli. Yaani, niko kama nimechanganyikiwa sasa hivi maana sijui ni nini nifanye. Mjomba ananiamini sana na malengo yake ya kumwendeleza binti yake kielimu nimeyaharibu kabisa kwa kumpa binti yake huyo mimba.
Kwa nini hamkutumia kinga naomba mjomba achukue maamuzi magumu juu yako ili iwe fundisho,
 
Mambo ya ajabu ajabu sana.

Wenzako wanaharibu wanaiba kwa jirani wewe unafanyana humo humo ndani.
 
Hata kama utailemba na kuita "Dada yangu binamu"

Ukweli nikwamba.,Ndugu yako ni ndugu yako tuu!!.

Najarib kutafuta maana ya kusudio lako la kumla dada yako lkn sipati picha!!

Kuna mwenzako aliandikaga humu kua "Amesex na Mama yake mdogo na kampa mimba"

Kisa ma mdogo analingana naye umri
 
Acha tamaa ila hiyo ni aibu kubwa na huna pa kuificha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom