Naombeni ushauri, nataka nizae naye tu kisha nitulie

AChana nae mapema kabla jua halijachwea
Huyo bint hakupendi , wewe ni mbadala tu, akishayatimba ndo anakutafta

hatokuja kuachana na mzazi mwenziye , ila km utaweza kuishi kwenye maumivu miaka yote basi endelea nae mkuu
Kila la heri
 
Habari zenu jamani, Mimi ni kijana Nina Miaka 25 nina jambo langu linaeda kama ifuatavyo.

Kipindi nipo chuo mwaka wa kwanza ambapo nilikuwa nasomea kada ya Afya, Kuna Binti nilikuwa naye kozi moja ila hakuwa vizuri sana darasani hivyo aliniomba niwe namfundisha nikaona sio mbaya nikakubali,katika kumfundisha nilitokea kumpenda lakini nilipomtongoza akawa kama sitaki nataka, akaanza kuniomba hela ya kusuka, mara matumizi yake mbalimbali na kwa sababu nilikuwa nampenda nikawa nampatia, ila Cha ajabu alikuwa hayuko tayari kunipa tendo, Wala kiss hata kumkumbatia alikuwa hataki,,nikavumilia ila sikupata kitu.

Ikafika muda wa kwenda field, Mimi nikaenda mkoa mwingine na yeye akaenda mkoa mwingine ambapo ndio kwao kabisa, pale alipokuwa akifanya Field Kuna daktari mmoja alimtongoza na Dem akajaa box maana jamaa alikuwa anavihelahela na alikuwa DMO msaidizi. Muda huo akakata mawasiliano na Mimi lakini taarifa zake nikapata kupitia rafiki zake.

Yule daktari alikuwa ana miaka kama 36 hivi na huyu dada alikuwa na 20, halafu huyu daktari alikuwa na mke wake pamoja na mtoto mmoja. Ikatokea huyu Binti akapata mimba na Jamaa akagoma kuhudumia mpaka ahakikishe kama mtoto ni wake, Binti hakuwaambia kwao na karudi chuo akapanga geto na kuajiri mfanyakazi kwa hela za ada anazotumiwa muda huo Mimi na yeye tushakata mawasiliano.

Baada ya miaka miwili huyu Binti akarudi kuendelea na masomo muda huo Mimi nipo mwaka wa tatu, nilikuwa nikionana naye hamna kusemeshana Kila Mtu anashika njia yake. Siku moja njiani akanisimamisha na akaniomba namba ya simu na nikampatia, kama kesho yake akanipigia simu akaniomba msamaha na kuniomba turudiane, nikamwambia asa Wewe so ushazaa na Mtu mwingine.

Akaniambia kuwa wameshaachan na mzazi mwenzake na wanalea mtoto tu ,kwa sababu nilikuwa nampenda ikabidi nimsamehe tu na tukaanza mahusiano na yakawa matamu mpaka akawa analala kwangu Kila siku kasoro jumapili tu, ambapo kwake anakaa na mtoto wake pamoja na mfanyakazi wake, akaniambia hata geto nisiwe napika niwe nakula kwake, chakula kikiiva napigiwa simu naenda kula na nilikuwa nachangia pesa nusu ya msosi pale kwake,tukawa kama familia.

Yule mzazi mwenzake akawa anapiga simu usiku wa saa Saba au saa nane kuulizia mtoto anaendeleaje,, Ikabidi nimwambie kama kweli wameachana ampigie simu mzazi mwenzake mbele yangu na amwambie kuwa asiwe anapiga simu usiku Sana awe anapiga mapema kuulizia habari za mtoto na amwambie kuwa ana mahusiano mengine kwa sasa na kweli akafanya hivyo mbele yangu wakakubaliana Walee mtoto.

Kipindi tunamalizia semister ya pili mwezi wa saba ikitokea yule Binti akapata mimba na Akaenda nayo kwao likizo lakini mm nikamwambia siko tayari kuwa na mtoto na nikamwambia atoe Ile mimba,,alitaka abaki ailee mimba ila Nika force mpaka akaniomba nitume hela akatoe,ni kweli alitoa na mama yake alijua akanipigia simu na kunitukana sana ila nikamuomba msamaha yakaisha.

Yule Binti kiufupi alifeli tena chuo na kwao wamechoka kumsomesha wakamwambia aende kwa aliyemzalisha Ili aolewe maana Binti kwao maisha sio mazuri sana, yule mzazi mwenzake ameshaachana na mke wake wa kwanza kwa sababu ya tabia zake za kulala na wanawake sana.

Sasa Binti akaanza kurudisha mahusiano na mzazi mwenzake bila mimi kujua mda huo akaanza kuwa bize Kila mda Yani hanipi mda kuwa naye mpka akasajiliwa laini mpya na mzazi mwenzake ambayo Mimi Sina na siijui.

Sasa siku moja Akaenda kwa mzazi mwenzake akakuta jamaa kavusha demu hapo ndo akakasirika na kunihadithia kuwa alitaka aniache, niliumia ila nikakaa kimya. Sasa huyu Binti amesusa kabisa kuolewa na mzazi mwenzake kwa sababu ya tabia za jamaa mpaka mahali akakataa, asa ananitaka nimtambulishe kwetu au nimpe mimba Ili iwe gia ya kutokuona na mzazi mwenzake Ili awe na mimi, huyu Binti ana jeuri sana, kiburi, dharau na mdomo wa kutosha, nimeshajaribu kumuacha ila najikuta narudi mulemule.

Kwa Sababu ninampenda nataka nizae naye tu halafu nitulie.

Je ndugu zangu mnanishaurije, NAOMBA USHAURI WENU WAKUU BILA KUTUMIA LUGHA CHAFU
Nyinyi ndio mnaosababisha wanaume wachukuliwe poa na hawa wanawake.
 
Pole sana kaka
Ila umevuka tamaa ya namna mungu alivyo kuumba muache huyo mwanamke kwa kumwambia ukweli kwamba kuwa naye ni sawa na kuoga tope wakati maji safi yapo

Ila usimchukie
Hakufai
Hawez kuwa mke
Uzaifu wa kushindwa kuacha sio mzuri


Mwishowe atakupiga mzizi ndio utakoma sasa
Asante kwa ushauri wako mkuu
 
Mh huu upendo gani mbona sijawahi kuuona mimi Achana na huyo dada.
Mimi najishangaa najaribu mpka kum block lakini akinitafuta kwa namba ngeni akanikasirikia msamaha najikuta nimemsamehe
 
Back
Top Bottom