Naombeni ushauri kwa hili.

Muce

Senior Member
Dec 19, 2011
116
14
Nina mpenzi wangu ambaye nimekuwa nae kwa muda mrefu sasa ingawaje kuna kipindi tulikorofishana na kutowasiliana nae kwa muda, lakini baada ya kuweka mambo yetu sawa na kuanza ukurasa mpya. mwenzangu amepata mimba lakini cha kunishangaza hajanipa taarifa kuwa anamimba na mimi nipo mbali nae, taarifa hizo nimedokezwa na dada yake, akinituhumu eti sitoi huduma na kumjali kama anaujauzito, ingawaje kila mwezi ninamtumia pesa za matumizi, sasa mm kwa hili nimeingiwa na shaka kuwa yawezekana nimebambikwa, wadau naombeni ushauri wenu nichukue hatua gani? nimemuuliza kama anamimba amekataa na amesema hana.
nawasilisha.
 
Nina mpenzi wangu ambaye nimekuwa nae kwa muda mrefu sasa ingawaje kuna kipindi tulikorofishana na kutowasiliana nae kwa muda, lakini baada ya kuweka mambo yetu sawa na kuanza ukurasa mpya. mwenzangu amepata mimba lakini cha kunishangaza hajanipa taarifa kuwa anamimba na mimi nipo mbali nae, taarifa hizo nimedokezwa na dada yake, akinituhumu eti sitoi huduma na kumjali kama anaujauzito, ingawaje kila mwezi ninamtumia pesa za matumizi, ....
Endelezea stori yako kutokea hapo nilipoikatizia kwa kuanza na maneno... "Nilipoomuuliza mpenzi wangu kuhusu hilo, yeye alinijibu........................................." Ukiimlizia hiyo stori tutaweza kukushauri.
Karibu, endelea...
 
Lisemwalo lipo kama halipo laja....! Fanya mchakato wa kuonana nae...kama upo mbali sana then chagua kuamini maneno yake (beibe wako)..thats it. Ukirudi utathibitisha kila kitu...
 
Nina mpenzi wangu ambaye nimekuwa nae kwa muda mrefu sasa ingawaje kuna kipindi tulikorofishana na kutowasiliana nae kwa muda, lakini baada ya kuweka mambo yetu sawa na kuanza ukurasa mpya. mwenzangu amepata mimba lakini cha kunishangaza hajanipa taarifa kuwa anamimba na mimi nipo mbali nae, taarifa hizo nimedokezwa na dada yake, akinituhumu eti sitoi huduma na kumjali kama anaujauzito, ingawaje kila mwezi ninamtumia pesa za matumizi, sasa mm kwa hili nimeingiwa na shaka kuwa yawezekana nimebambikwa, wadau naombeni ushauri wenu nichukue hatua gani? nimemuuliza kama anamimba amekataa na amesema hana.
nawasilisha.
Mambo gani hayo yaliyowekwa sawa?
 
Baba wa mtoto ni mama pekee anayejua. Kuwa mwangalifu, nadhani hisia zako ni sahihi na unabambikiziwa
 
kama umemuuliza akakataa si uchukue pregnant tester upime mkojo? tena hilo lifanye kwa kushutukiza,na kama anayo ujue hiyo siyo ya kwako
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom