mkwawa gabriel
Senior Member
- Apr 7, 2012
- 100
- 23
Mie ninamchumba wangu ambae nimedumu nae takribani sasa miaka 5.Tulianza mahusiano mie nikiwa nimemaliza kidato cha sita yeye cha nne,nikaenda chuo kikuu yeye akaenda advance level lakini mahusiano yetu yalikuwa mazuri sana na nilijitahidi kumpatia kila kitu na kumwonyesha penzi la dhati nilipo maliza chuo kikuu mwaka jana yeye akajiunga jeshi na kurudi kuendelea na masomo chuo kikuu cha Dar es salaam sasa ameanza kubadilika mawasiliano yanapungua kila siku,matusi kila kukicha na cha ajabu zaidi nikimkosoa pale anapokuwa amekosea anakuwa mkali sana na kunambia tuvunje uhusiano wetu,na kwa sasa ameanza kutoa sababu nyingi sana ni kama vile hataki kuonana na mie tena na pia amefika mbali za kuanza kuniita mie maskini wa kutupwa naombeni ushauri wenu jamani nifanye nini kwa sababu alipata mimba akaitoa na nikimgusia suala la kuoana anasema hayupo tayari kuolewa kwasababu mie sina chochote,na cha ajabu anajeuri,kiburi,dharau,na kujisikia na mie nampenda sana kwasababu miaka yote nimewekeana malengo ya kuoana nae!!!