Naombeni ushauri juu ya hili

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,338
Nilitapeliwa sh 1,600,000 na ndg. fulani, kisha akatoloka kwa masiku kadhaa, nikatoa taarifa ya kuibiwa polisi urafiki ubungo na kupatiwa RB... wakati wa mizunguko ya ndugu zangu wa karibu wakamuona mwiz wangu sehemu nilipotoa taarifa polisi niliombwa sh 40000 kwa ajili ya usafiri kumfata kimala ( sikutoa), nikaenda mwenyewe nakufanikiwa kumkamata na wasamalimia wema mpaka polisi, hakatupwa ndani polisi aliyekuepo zamu akaniomba ya maji ya kumshungulikia (sikutoa na kunitishia) baadaa ya siku mbili nikapangiwa mpelelezi wa kesi hiyo naye akaniomba sh 100,000 iliafanye kazi kwa haraka sanaaa mpaka sasa tunasumbua nayeeeee n.k

je nifanyaje wakuu? ushauri na maoni karibu.

Nimejaribu kunukuu vifungu vywa katiba na sheria mbalimbali juu ya hili nimeonekana mkolofi na kutishiwa.......
 
Pole sana ndugu yangu, Mungu yupo upande wako. Usikubali hata siku moja kutoa rushwa. Jaribu kushirikiana na takukuru kama wasipokuwa na ushirikiano endelea kumwamini Mungu. Hakuna kitu kinachotokea bila kusudi la Mungu. Mungu yupo juu ya yote anajua unachokumbana nacho. Haki yako utaipata.
 
Hao ndo polisi wetu kaka. Yaani wewe una shida, umeibiwa halafu unaambiwa utoe pesa ili mwizi akakamatwe! Pengine wakienda kwa mwizi nae wanamuambia atoe pesa ili wasimkamate.. Kwanza polisi hao wanawafahamu wezi wote kwahiyo hata ukitoa pesa bado wanaweza wasifanye lolote.
Mimi kuna wakati niliibiwa yaani ilikuwa ni usumbufu na vitu havikupatikana hadi leo. So disappointing.
 
Back
Top Bottom