Naombeni ufafanusi juu ya maombi

Mathika

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
279
Reaction score
320
Kuna best yangu kaniuliza ila nikawa sina jibu la uhakika la kumpatia.katika maombi ya kuomba rehema kwa Mungu ni lazima uwekewe mkono kichwan na pastor au waweza jiombea mwenye na Mungu akakusamehe? Pia kwa nn linapoongelewa ovu lolote madhabahuni huwa anatetemeka?
 
Labda tumuulize bashite kwa nini anapoombewa analia kama mwanamke
 
Tenda mema bila kumshirikisha Mungu.
Pia, Ukitenda maovu usimuhusishe Shetani wala kumsingizia kwa njia yoyote ile.
 
Anatetemeka kwa sababu ya hatia alonalo moyoni juu ya dhambi alizotenda. Si wakati wote tunahitaji kuwekewa mikono na watumishi. Mawazo na midomo yetu mara nyingi hutusaliti. Je, kama ni usiku anataka ulinzi wa MUNGU kabla ya kulala, atamtafuta kwanza mchungaji amwombee? Hapana. Ataomba Rehema na kulala.
Ila kwa situation Yake, aonane na mchungaji wake. Sio kanisani kwa staili ile ya "wenye ...... Wapite mbele waombewe!" Hapana. Akazungumze naye private ofisini. Pamoja na kuombewa, mazungumzo pia huweza kumfungua mtu. Na huyo "mtumishi" atakuwa specific hata katika maombi yake.
 
Kuna maombi ya rehema na maombi ya toba. Kuna mtu anahitaji toba na kuna mwingine anahitaji rehema.
Kama tayari alishafanya maamuzi totally ya kukataa dhambi kwa kumpokea Yesu huyo mtu anapotenda dhambi huhitaji rehema .Na maombi ya rehema mtu huweza kujifanyia yeye mwenyewe tu sirini.
Kama hajawahi kufanya maamuzi ya moja kwa moja ya kumpokea Yesu na kuacha dhambi huyo anahitaji toba na toba mtu hufanyiwa na mtu mwingine aliyeamini na kuishi maisha masafi.
Kuhusu kutetemeka nitashindwa kulizungumzia kwa undani kwakuwa sijajua huyo mtu yuko katika kundi lipi kati ya hayo mawili niliyoyataja.
 
Nashukuru sana nimeelewa
 
Nimeelewa asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…