Habari zenu!
Kwanza kabisa napenda niwafaamishe kuwa JF amekuwa rafiki, mshauri, mkosoaji, na mchekeshaji na pia mkandamizaji kwangu ndani ya miezi kadhaa toka nimejiunga.
NAKUPENDA JF.
Nirudie kwenye mada, mimi ni kijana wa miaka 29, bado sijaoa na sina mtoto bado, ingawa na-miss sana kuitwa baba.
Kuna rafiki yangu wa kike. Kwa maelezo yake yupo single toka muda sasa. Nilijuana naye miaka kama mitatu hivi iliyopita, kwa sasa ana umri wa miaka 24.
Mwaka 2012 niliwahi lala nae na akanipa papuchi kama mara tatu hivi.
Ila kunipa papuchi, haikuwa rahisi. Ni "mgumu kugawa".
Sikuwa na mtu kipindi hicho. Baada ya hapo tumekuwa "marafiki" tu.
Nami nikawa na msichana mwingine mpaka mwaka huu mwezi wa tano, uhusiano haukuwa mzuri. Huyu rafiki yangu "alijua" kuwa nina msichana lakini hakuwahi kuonana naye.
Ila mwezi wa sita nilizungumza naye (huyu rafiki) nikamwambia siko tena na msichana na sikuwa tayari kuwa kwenye uhusiano kwa muda huo sababu niliona ninahitaji muda kutafakari na kutathmini mambo yote ya mahusiano na maisha kwa ujumla.
Huyu rafiki yangu toka hapo naona amekuwa akinitembelea chumba nilichopanga mara kadhaa. Anaweza akaja jumamosi au Jumapili nzima akashinda kwangu.
Akifika saa zingine ananipikia, ananiletea CD za kuangalia, alafu tukiongea ameanza kuongea mambo ya kuwa na mtoto kama mimi.
Akidai kuwa maisha ni mafupi, binadamu anaweza poteza maisha na ni vizuri angalau kuacha mtoto.
Mimi bado nipo mtaani kwa sasa. Bado natafuta tafuta kazi na pia nina mawazo ya kujiajiri.
Huyu rafiki yangu amekuwa mida fulani ananipigia simu saa tano usiku na kuniambia kuwa kuna tangazo la kazi kaliona mahali, hivyo nifuatilie.
Yeye ni nesi, pia kuna siku asubuhi, aliniandikia message 'I NEED YOU'.
Na pia jana kaja kwangu na kashinda hapa, tumeongea mambo kadhaa, baadae mimi mwanaume mzuka ukapanda, nikajaribu kumtomasatomasa, lakini alinibania.
Nilikasirika ila nilifurahi, aliniambia kuwa hapendi "games".
Hivyo nili-stop, nilikasirika sababu aliniacha na nyege zangu, ila nilifurahi kuwa bado ni mgumu wa kugawa na ana msimamo.
Mimi Sipendi msichana mwepesi.
Mwepesi kwangu mimi ni malaya, yaani atakuwa anamvulia chupi mwanaume yeyote.
Hivyo nilipendezwa na ugumu wake, sasa usiku wa kuamkia leo, nimewaza sana.
Nimeona nisije nikawa nachezea shilingi chooni.
Nikahisi, labda Mungu ananiambia, huyu ndo wangu.
Ni mzuri tena wa asili. Ishu ni nimetoka kwenye uhusiano miezi mitatu tu iliyopita, na hatma yangu na yule wa zamani kiukweli bado ipo hewani, sababu naye ameanza kunitafuta kwenye simu akidai ananipenda sana! Je mwanishaurije?
Nivute subira na niendelee na kutafakari na kutathmini uhusiano na maisha kama nilivyokusudia kwa kipindi hiki, nimwambie kuwa nami 'I need her' huyu rafiki yangu, au nipeane nafasi na yule wa zamani tena?
Asanteni.