naombeni msaada wenu jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

naombeni msaada wenu jamani

Discussion in 'JF Doctor' started by combra, Aug 1, 2012.

 1. combra

  combra Senior Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nina tatizo la mba kichwani ambalo ni la mda mrefu.ni hivi nikiziacha nywele zangu kwa mda wa mwezi nywele zinakuwa na mba aina ya ungaunga na kuniwasha sana tena nikizichana bila kutia maji zinawasha sana.lakini nikizinyoa mba wote unakwisha.Nilijaribu kutumia dawa za kupaka na kumeza bila mafanikio. naombeni ushauri na kwa yeyote anaye jua tiba yake.unanipa sana aibu nikienda kunyoa saloon nakuutwa nina mba.msada plz kwa mwenye uelewa
   
 2. S

  Short white Senior Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni Dandruff. Tumia anti- dandruff yenye Salicylic Acid 2%. The commonest brand available yenye Salicylic Acid ni Sulfur 8 spray. Zinapatikana kwenye maduka ya dawa baridi au supermarkets. Apply 6 hourly , tatizo lako litakwisha.
   
 3. combra

  combra Senior Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  asante sana
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama Dawa aliyokupa.@Mr Short White haijakusaidia Tumia Dawa yangu ya Tiba Mbadala huenda ikakusaidia kuondowa huo Mba kichwani mwako. Pata Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji hayo ya Uvuguvugu kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

  (Fenugreek) kwa kiswahili inaitwa Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya (fenugreek) Uwatu unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote Mba wataondoka Inshallah bila tabu yoyote. tumia kwa muda wa siku 10 kisha unipe feedback Mkuu.@combra
   
Loading...