Naombeni msaada wa mawazo

Posher

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
61
Reaction score
113
Poleni kwa Majukum ya siku nzima, naomba mwenye Uzoefu na hichi kitu anisaidie;

Niko kwenye mahusiano ni binti mmoja nilikutana nae faragha wiki mbili zilizopita juzi nowadays anajiskia uchovu sana, kichwa kuuma, juzi aliniambia ana hamu na maembe mabichi, nikampelekea kazini kwake akasema hamu ya maembe imeisha.

Alienda kupima kipimo cha mimba akakuta mstari Mmoja umekolea na mwingne hauonekani vizuri.(Sijui kama mimba tayari au laah)

Jana alinambia ana bleed! Ndo akanichanganya. Hivi inawezekana mwenye mimba aka bleed??.

Nishajiandaa kuwa Baba, nahitaj tu kujua ili niandae mazingira sawa ya kuhudumia. Asanteni
 
Unauza mechi kindezindezi, yapo makubwa yenye kutisha ya kuyahofia kuliko mimba mzee
 
Anakuandalia mazingira akupige na kitu kizito.
FANYA HIVI

1.Muite siku na umwambia mwende mkafanye vipimo.PAMOJA

2. Akikutwa na mimba doctor akwambie ni miezi mingapi.

Maana anaweza asiwe na mimba akawa anakutoa pesa tuuu

Au akawa na mimba ila sio ya kwako.
Mimba huwa haileti shida ndani week hizo 2 hata iweje.!!!!

SHTUKA!!!!
 
Huyo amenasa mimba wala usiwe na shaka kijana JIANDAE KULEA MAANA
MIMBA HUWA INAONEKANA WEEK 2 Na kuendelea though kuna ambao dalili huonekana mapema sana.

Hebu tuangalie hivu vitu hapa.

1. Kuna kitu kinaitwa 'implantation bleeding" hii hutokea pale yai lililorutubishwa tayari linapojichimbia /kujishikisha kwenye mji wa mimba hapa mwanamke atapata damu kidogo ambayo wengi huwa wanaichanganya na damu ya hedhi thogh hii damu huwa si nzito.

2. Uchovu na maumivu ya kichwa ni moja ya vitu vinavyoambatana kwa yule mwenye mimba changa hii ni kutokana na mabadiliko ya ki hormone .

3. Appetite pia huwa inabadilika kutokana na mabadiliko ya kihomoni yanayotokea kwa haraka kwenye mwili wa mwanamke mwenye mimba changa ndiyo maana akaomba maebe mabichi.

4. Kwa sababu mmefanya rapid test (i.e mmepima mkojo) kuonekana mstari uliokolea na uliofifia inamaanisha mimba ipo na ni changa (i.e kiwango cha Human chorionic gonadotrophin homone (hcg) kipo kwa kiwango cha chini ).

Ushauri wangu
Jiandae kwa ajili ya kumlea mama na mtoto wake afuate lishe na mazoezi yaliyo bora ili asije jifungua kwa operation .

HUWA WANAPENDA CHIPSI AISEE ZUIA ASILE HOVYO MACHIPSI MAANA WATOTO WANAKUWA WAKUBWA MWISHO WA SIKU ATAONGEZWA NJIA.

ALL IN ALL HONGERA MKUU AKISHA ZAA MUOE SASA UACHANE NA UKAPEL
 
Doctor hawezi kujua exactly mimba ni ya miezi mingapi maana yai likisharutubishwa kipimo na dalili huwa zinaonekana 2 weeks after sasa kujua exact day ni ngumu.

Huwa inajulikana baadae sana baada ya minba kukuwa sana au baada ya kujifungua acheni kumpoteza mtu.
 
Kwa maelezo yako mkuu huyo amenasa mimba na kuna high possibility ikawa ya kwako ,nimeangalia ushauri wa wayu wengi humu wanatoa tu ushauri bila ku back up na scientific explanations hii ni mbaya .
 
Shukran mkuu umefafanua kisomi zaidi
 
Mkuu kwahio yale makadirio ya kujifungua ambayo wanawake huwa wanapewa na madaktari na huwa kwel huwa wanapigiwa Ramli au.???
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…