Habari zenu wanajamii forum..ndugu zangu hali yangu ni mbaya kiuchumi nikiwa katika wakati huu mgumu wa kusubiri ajira ,nashindwa mpaka kupata mahitaji ya muhimu !.,nimekaa nikafikiria nikaona nianzishe biashara ndogo ya ngenge japo iweze kunisaidia kwa kipindi hiki kigumu lakini tatizo ni mtaji ,kitu pekee cha thamani nilicho nacho ni hii tecno M3 ambayo ndio naitegemea kupata habari mbalimbali na hata niiuze kupata mtaji pia hautatosha, kwa hiyo naomba mwenye kuguswa na hitaji langu anisaidie chochote hata mia ili niweze kupata mtaji niweze kujishkiza na hii biashara .
Mchanganuo:
-Nahitaji mtaji Wa sh.60,000 kwa ajili ya kuweka kibanda na kununulia bidhaa.
- Sehemu ninayotarajia kufungua genge ni nje ya nyumba ninayokaa ambapo ni kwa shangazi yangu.
-sehemu ninayoishi ni Vijibweni Kigamboni
Hitimisho;
-Najua kuna wengine watachukulia kama ni utapeli ,naheshimu mawazo na mitazamo yao ,lakini nawahakikishia kuwa hii ni shida imenibana mwenzenu na najaribu kuwashirikisheni mnisaidie kama si kwa hela hata kwa ushauri Mzuri utakao nifaa..Kwa atakaye guswa naomba ani PM .Ahsanteni.
Wewe ni me au ke?Nipo serious ,
Mkuu sasa ataendaje kijijini kulima ilihali PEMBEJEO zote zipo mjini?Kama wazazi wako kijijini ni heri shambani, patakutoa fasta, mjini hapa bila kazi maalum ni hatareee
Kwani wazazi wake wanafanya nini? Pembejeo ziko zaidi vijijiniMkuu sasa ataendaje kijijini kulima ilihali PEMBEJEO zote zipo mjini?
Mkuu kwa nini tunapenda kulima kilimo cha magazetini kijini ardhi bado INA rutuba yakutoshaMkuu sasa ataendaje kijijini kulima ilihali PEMBEJEO zote zipo mjini?
Mkuu unajua kuna watu hawajawahi kwenda kijijini wanasikia tu hawajui kijijini kuna fursa zaidi ya mjiniKwani wazazi wake wanafanya nini? Pembejeo ziko zaidi vijijini
And trust me, kama mtu anakaa mahali pamoja alafu analia njaa, huyo ni muongo maana misumari haija mchoma vizuri mpaka kimfanye ahame kwenye comfort zone!Mkuu unajua kuna watu hawajawahi kwenda kijijini wanasikia tu hawajui kijijini kuna fursa zaidi ya mjini
Mkuu kuna vitu vimetufanya tuwe vipofu japo tuna macho ya kuonaAnd trust me, kama mtu anakaa mahali pamoja alafu analia njaa, huyo ni muongo maana misumari haija mchoma vizuri mpaka kimfanye ahame kwenye comfort zone!
Kwa kweli! Lakini ipo siku Mola ni mwaminifu mileleMkuu kuna vitu vimetufanya tuwe vipofu japo tuna macho ya kuona