Ndugu kila course ni
nzuri, inategemeana na vitu vingi kwa mtu kusomea kitu fulani.
Kila mtu ukimuuliza kwa nini anasoma kozi fulani atakupa sababu nyingi
labda mojawapo ni atakwambia "inalipa sana"
Ushauri wangu ni kuwa soma kitu unachokipenda kutoka moyoni na sio kwa
kuangalia watu wanasemaje kwa maana hakuna kitu ambacho hakilipi, kwa
kuwa kama hakilipi watu wangeshaacha kukifanya.
Kama wewe ni mdau wa teknolojia, programming, Designing, mawasiliano,
etc Computer Science itakufaa.
Na kama unapenda sana mambo ya kibenki, fedha na uchumi basi hizo kozi
za tax na finance zinakufaa.
Angalia pia unapenda kazi gani, mfano, za ofisini, za viwandani,
personal, designing, kwenye benki.
Ukisema unapenda kufanya kazi za aina gani ni rahisi sana nikakushauri
usome nini, ila kila kazi inalipa na umahiri wako ndo utakuweka
mjini.