wicalumtata
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 329
- 113
Natanguliza shukrani kwanza , naombeni mnisaidie nifanyaje maana simu yangu sikuitumia takribani miezi 4, kwasabu ya kuwa na ubovu wa betri na sasa betri imepatikana nikaiweka alafu nikacharge lakin muda wa saa 1 nkaitoa nikaanza kuifanyia setting lakn ilipoanza kupungua chaji ikanibd nichomeke chaji tena cha ajabu ikawa haijai ila asilimia zinazidi kupungua . Ikabd niizime afu niwashe . Nilipofanya ivo ndio ikaonesha kiwango sahihi cha chaji kwa asilimia . Ikawa inaendelea kuchajiwa lkn bado haioneshi ikiongezeka katika ile alama ya betri pale juu ila inapungua tu, ikanibid nifanye soft reset ambapo nikabonya power button na volume down had ilipovibrate . Lakin ilipovibrate ikaandika nokia logo alafu ikaweka rangi ya blue ikiwa na alama katikati yake, alama ile inaanza na semi coloni au nukta pacha na alama ya fungua mabano alafu inakaa sekunde chache afu inazima. Sasa sijajua tatizo ni nini , au kwasabu imekaa muda bila kutumika au nini hasa? Naombeni msaada .