Naombeni majibu juu ya hili kwa yeyote atakayefungua hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni majibu juu ya hili kwa yeyote atakayefungua hapa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ISACOM, Oct 6, 2009.

 1. ISACOM

  ISACOM JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kuuliza si ujinga.Nataka kujua hivi kama umepata degree ya kwanza halafu ikakuwezesha kupata Masters.Halafu ukagundua kuwa ile first degree yako haina soko na uliamua kubadili ukachukua masters tofauti na ile first degree yako.Je ukiamua kurudi chuo kusoma miaka mingine mitatu kama umri unakuruhusu na ukafanikiwa kupata degree pure nyingine.Swali linakuwa hivi'' hiyo degree uliyoipata kwa awamu ya pili ukiamua kutumia na Masters uliyopata kwa degree ya kwanza itakubalika?Na je kigezo cha kuwa hiyo Masters na degree kupishana miaka,ikionekana Masters imeitangulia miaka degree uliyoombea kazi haitoleta utata?
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kama uliweza pata Masters kwa degree ambayo wewe unadhani haifai, then huna haja ya kufanya tena Bachelor.
  Mfano umepata Bachelor ya Engineer lakini baadae ukafanya Master ya
  Law then you don't need to do Bachelor of Law!
  Pia you can do Bachelor of Arts and the do a postgraduate diploma (equivalent to Masters) in any other subject
   
 3. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa nini kurudia bachelor tena wakati hiyo uliyokuwa nayo mwanzo ilikuwezesha kupata hiyo masters ya sasa?? nini maana ya kusoma hiyo masters?
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nitapenda kuchangia kama ifuatavyo:
  1.Unaweza kusoma bachelor hata tatu kwa mapenzi yako na kuendana na knowledge unayotaka kupata.Epuka kusoma kama fashion.Lenga kwenye kutafuta maarifa na pia uangalie matumizi ya hizo degree.

  2.Kuna namna mbalimbali za kuji position hata kama degree uliyoipata mwanzo unashindwa kuitumia. Unaweza kuitafutia linkage na masomo mengine maana dunia ya sasa inataka mtu multi-disciplinary na siyo mwenye mtizamo mmoja tu.Mfano, siku hizi kila mtu anakimbilia kusoma Law..ati kwa vile wanadhani inalipa kwa kuwaangalia mawakili wanavyotengeneza pesa! Wanasahau kuwa huko tuendako kuwa na degree ya LLB peke yake si mali kitu... unatakiwa uwe na taaluma nyingine kama Finance, management, medicine, forensic, development management,IT etc. maana specialisation ni muhimu.

  Unaweza kusoma kozi fupi fupi kwenye masuala ya afya ya jamii ( public health), environment, HIV/AIDS, POVERTY,Human Rights, NGDOs etc HAYA siyo lazima uyachukulie degree bali waweza kusoma postgrad ukaichanganya na fani yako nyingine uliyoisomea ukajikuta mambo yako ni poa sana.
  3. Kuhusu kutumia hizo degree kutafutia kazi, inategemea jinsi utakavyofanya maombi ya kazi na kazi husika zinataka mtu mwenye vyeti gani.Pia unashauriwa kupata uzoefu hata kama ni kwa kujitolea.Watz wengi hawajaielewa concept ya volunteersim na hapa ndipo wenzetu wazungu na wahindi au hata watu wa nchi nyingine za Africa hutupiga bao.Kujitolea bila hata kulipwa kuna faida zake a). Unapata fursa kuingia kwenye taasis na kujifunza chini ya watu mahiri na hapo hapo b). unajenga CV yako kiasi kwamba utakapokuja kuomba kazi ukiulizwa una uzoefu unaweza kujibu kwa ma confudence kuwa unayo.Watu wawe na malengo kila hatua kuanzia kusoma hadi kujiandaa kutafuta kazi.
   
 5. ISACOM

  ISACOM JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa ushauri wenu mzuri.
   
 6. M

  Menyous Senior Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ungesema kabisa hizo first degree ni zipi na the masters degree ni ipi haswa, si ajabu hutohitaji kufanya first degree nyingine kufukia ile ya mara ya kwanza ili iende sambamba na Masters unayoitaka.
   
 7. Robweme

  Robweme Senior Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "Ilo ni tatizo la watu kusoma kwa kufuata mkumbo, mtu unaenda chuo kikuu hata hujui kwanini unaenda pale au unataka kuwa nani? na kufanya kazi gani katika maisha yako.Lazima kuomba ushauri kabala ya kusoma,na lazima hujue unasomea nini?.Sasa fikiria unasoma 4 years alafu unatafuta njia za kufukia degree ya kwanza, unapoteza muda.
   
 8. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280

  Pamoja na ushauri mzuri wa wanajamvi, nakushauri uache harakati za kusoma ili upate kazi tu (kuwa manamba). Soma kwa mchepuo wenye lengo la kuwa na maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha kwanza na kazi ya kuajiriwa ifuate kama unapenda. Ukiwa na mtizamo wa kusoma ili uwe manamba mkubwa utatumikishwa sana dunia ya sasa. Pole kama nimekuudhi.
   
 9. SONGEA

  SONGEA Senior Member

  #9
  Oct 24, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hapa JF anafaidi aliye uliza na aliyesoma!
   
Loading...