Naombeni kujua

J C

JF-Expert Member
Dec 12, 2013
2,915
2,350
Wasalamu wajumbe wote wakubwa kwa wadogo. Kutokana na sintofahamu kuhusu nini kinaendelea kuhusiana na gonjwa hili la corona nchini Tanzania naomba kujua tafuatayo.

1. Hivi vipimo vya wagonjwa wa corona bado viko mjini Dar es salaam pekee au hata kwenye hospitali za mikoa na wilaya vinapatikana incase mtu akitaka kujua afya yake?. Maana mara ya mwisho kabla ya kugundua kuwa vipimo vinapima mpaka oil chafu sample zote kitaifa zilikuwa zikitumwa Dar na majibu kurudishwa baada ya siku kadhaa.

2. Kama bado ni Dar es salaam vipi kuhusiana na hospitali binafsi hasa mikoani kama Mwanza, Arusha, Mbeya ni wapi vipo?. Na vipi kuhusiana na matibabu binafsi ya hili gonjwa zinatolewa?. Naomba kama hospital binafsi zipo mkoani zinazotoa huduma hii zijitanabaishe hapa ili wenye fedha zao waweze kwenda na kupata huduma ya vipimo na matibabu.

Asanteni sana na nitashukuru kwa majibu ya yakutia moyo kutoka kwenu wadau.
 
Ngoja wajeee... japo sidhani kama vimesambaa mikoani, labda hivi karibuni..

Mkuu ukipima ukakutwa nayo....
Sidhani kama watakuachia utoke.
 
Ngoja wajeee... japo sidhani kama vimesambaa mikoani, labda hivi karibuni..

Mkuu ukipima ukakutwa nayo....
Sidhani kama watakuachia utoke.
Asante. Ndio maana nimeulizia hospitali binafsi maana huko inaweza kuwa rahisi kidogo rejea hata mke kujifungua unaweza kumtia moyo pembeni kuliko government.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom