Naomba ushauri

Naomba ushauri

nkumbizi

New Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
4
Reaction score
1
Baba mtoto alinitenda sn wkt mtoto ana miezi 4 alipofika miezi 9 nikaamua kuachana naye nikajianzia maisha yangu,leo mtoto ana miaka 2 na nusu anaomba msamaha turudiane. Ushauri plziiii!
 
Hakuwa karibu na wewe kipindi ambacho alitakiwa azidishe sana ukaribu na wewe! Umehangaika mwenyewe, mtoto ana miaka 2 ndio anakuja! Atakuwa amekaa huko amegundua mtoto labda ndio huyo huyo ndio anajileta! Msamehe ila usikubali kurudiana nae, asiwe karibu na wewe hafai!
 
...alikutenda vp dada yetu?
...mlioana kwa taratibu zote?
...na alienda wapi?
 
Ukitaka kuskia ya walimwengu basi kila mtu atakushauri kulingana na uchungu uliojaa moyoni mwake + uzoefu.
Wewe usikilize moyo wako kama bado unamuhitaji na unampenda.
Kwani hakuna mema amekufanyia maishani mwako ni hilo baya tu? Na ni kwa nn baya lichukue nafasi kuliko yale mema mengi?
 
-Wewe bado unampenda?
-Hayo madhambi yake unaweza kumesa and kuishi nae tena pamoja?
-Wakati huo mliochana alikuwa anasupport malezi ya mtoto?
-Je anaonekana kubadilika?
-Je mliooana kisheria au kidini au tu mlizaa?
 
Baba mtoto alinitenda sn wkt mtoto ana miezi 4 alipofika miezi 9 nikaamua kuachana naye nikajianzia maisha yangu,leo mtoto ana miaka 2 na nusu anaomba msamaha turudiane. Ushauri plziiii!

Akikupa mimba ya pili, atakukimbia na atarudi tena kwako mtoto akiwa na miaka 2 ndiyo utajua lengo lake kwako ni nini!!! By the way, wewe unafikiri nini juu ya hilo ombi lake?
 
Samehe tu...

Maisha yana mambo mengi sana na hayo yaliyokukuta si mwisho wa yatakayoendelea kukukuta....
 
Ukitaka kuskia ya walimwengu basi kila mtu atakushauri kulingana na uchungu uliojaa moyoni mwake + uzoefu.
Wewe usikilize moyo wako kama bado unamuhitaji na unampenda.
Kwani hakuna mema amekufanyia maishani mwako ni hilo baya tu? Na ni kwa nn baya lichukue nafasi kuliko yale mema mengi?

fuata ushauri wa huyu boy
 
Ukiwa mbali nae unajihisi vp? Unadhani Hisia zako kwake zitafunika makosa yake? na je kwa tabia hawezi kukutenda tena? kama majibu yote ni YES basi fanya fasta kumkubali asije akabadili mawazo
 
Baba mtoto alinitenda sn wkt mtoto ana miezi 4 alipofika miezi 9 nikaamua kuachana naye nikajianzia maisha yangu,leo mtoto ana miaka 2 na nusu anaomba msamaha turudiane. Ushauri plziiii!

mpaka unaomba ushauri maana huna uhakika na unachokitaka.
na tafsiri yake ni kwamba kuna sehemu ya moyo wako inataka umrudishe, nyingine ina mashaka.
alivyokutenda ni wewe ndio unayejua,
na alicyokuwa anakufurahisha ni wewe unajua.
shirikisha akili yako upime mbivu na mbichi na usiyajutie maamuzi utakayoyafikia.
anaweza kuwa kajirekebisha na labda kwa afya ya makuzi ya mtoto huenda ni vizuri mkirudiana; lakini pia anaweza akarudi kukuumiza na kuathiri makuzi ya mtoto hivyo ni vyema kutokuwa pamoja.
Maamuzi sahihi ni yale ambayo umeyafanya wewe mwenyewe ukimshirikisha Mungu pia; na yanaweza kuwa ni sahihi kwa wakati na mazingira fulani tu.
 
mmefunga ndoa? kama mmefunga ndoa, nakushauri mwende mkapime vvu halafu umsamehe tu; na urudiane naye. huo ndio ushauri pekee ambao ninaweza kukupatia kwasababu mtoto ni bora akapate upendo wa baba na mama wakiwa pamoja tena kwenye ndoa asije kukua akijua yeye ni mtoto wa kambo...nimesema kama mlifunga ndoa huna jinsi, ulishampenda huyo hivyo huna budi kumsamehe na kuanza ukurasa upya. kama hamkufunga ndoa, mlikuwa mahawara tu hivyo you are not bound to him basi kama unampenda na unataka kuendelea naye mkapime vvu na mwende mkafunge ndoa msiwe mnazini, ila kama haumpendi, mwambie sikupendi tafuta mwanamke mwingine, ila mpange namna atakavyohuduma mtoto wako kwasababu responsibilities kwa mtoto iko palepale. bofya hapa upate kitabu kitakachokusaidia namna ya kudai matunzo ya mtoto na mambo mbalimbali ya ndoa. SHERIA KWA KISWAHILI

View attachment 105052View attachment 105052
 
maamuzi unayo wewe vile unajua alivyokutenda na pia wamjua kwa mema yake kuwa mwangalifu isijekuwa anarudi kutaka kuharibu
 
Baba mtoto alinitenda sn wkt mtoto ana miezi 4 alipofika miezi 9 nikaamua kuachana naye nikajianzia maisha yangu,leo mtoto ana miaka 2 na nusu anaomba msamaha turudiane. Ushauri plziiii!

msamaha haunaga muda. Tafuta nafasi kwenye moyo wako umsamehe. Kabla sijaendelea naomba niulize swali. mlishaoana?
 
Anataka mtoto wa pili, kisha atasepa tena. Akirudi anaongeza wa tatu, hapo ujanja wako utakuwa kwisha kabisa maana mwanamke na watoto watatu labda kibabu cha miaka 70 ndia kitakua tayari kumalizia umri wake kwako.
 
Tulikuwa tuko mioni kubariki ndoa baada ya vituko hv mi nikasitisha kwanza "alikuwa akirudi asbh amewahi sn sa 8 au 9 za usiku na amelewa top, mapnz hakuna tn, anaondoka ata sumni haachi na hata kujua hali yangu au ya mtoto ilikuwa ni ngumu sn, alikuwa anijali kwa lolote yalinishinda kwa kweli.
 
-Wewe bado unampenda?
-Hayo madhambi yake unaweza kumesa and kuishi nae tena pamoja?
-Wakati huo mliochana alikuwa anasupport malezi ya mtoto?
-Je anaonekana kubadilika?
-Je mliooana kisheria au kidini au tu mlizaa?

kwa ukweli tulikuwa tuko mbioni kubariki ndoa lkn mm ndo nilisitisha baada ya vituko na maudhi yake kwangu. alikuwa anamjali mtoto tu tn kwa asilimia ndogo na ni pindi ajisikiapo
 
Kama muda wote huo ulikuwa single, basi haujawa tayari kumuacha. Mpe nafasi tena ila this time uwe tayari kwa nyendo zake. Usizae haraka tena. Usisahau kupima
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom