Ndugu Bilionea,
Mwanzo nilishawishika kusema kwamba watu wanaokuambia kuwa Bongo huwezi kupata kazi kama wako Bongo basi wanaogopa ukija utakuwa tishio kwao, lakini najua Watanzania hatuko hivyo. Kwa aliye Tanzania akisema hivyo basi ni kwamba ana wasi wasi tu na maisha hivyo anahamishia hofu zake (ambazo ameshindwa kuzishinda) kwako.
Na kwa anayekushauri hivyo aliyeko US, kama walivyochangia wadau wengine, inawezekana aliamua kubaki US na akahalalisha uamuzi wake kwa sababu hiyo hiyo ambayo anaiuza kwako sasa.
Kwa ujumla elimu ya US inathaminiwa sana Bongo kwa hiyo kama ni ajira ukitafuta utapata.
Kitu pekee ambacho wabongo wengi hawapendi ni majivuno. Kwamba ukija na mentality ya "super power" basi usishangae kuona raia wanakuchunia. Hawakupi michongo. Na hii nadhani ni duniani kote katika ulimwengu wa biashara. Humbleness ni kitu muhimu sana.
Pia angalia familia yako. Je ni kweli hawajiwezi au kwa kuwa uko Marekani ndio wanadhani "umeukata"?
Kuna wakati wadogo zangu walikuwa wananisumbua nikiwa nje lakini nikawaambia kwamba sina hela ya kuwatumia. Iliwachukua mwezi mmoja tu wakawa wamepata alternative, na hawakuniomba tena toka hapo.
Hiyo ndio siasa ya kujitegemea ambayo inafaa tuikazanie.
Kama utaamua kurudi Bongo njoo kijasiriamali. Unaweza kufanya kazi mwaka mmoja au miwili ili upate picha ya politics za maofisini, lakini longterm iwe ni ujasiriamali. Kuna fursa nyingi ziko wazi hapa. Mtaji hata wa $5,000 tu utakupeleka mbali Bongo. Ukishaanzisha kitu tu, safari moja itaanzisha nyingine.
Na mwisho kabisa, my friend Bilionea, The US is the land of winners, optimists, positive thinkers and opportunists. When you step out of the US (especially after 8 years) into the outside world you should probably fear nothing except fear itself. Americans have done a great job projecting a positive image of their nation that even Al Jazeera have not succeeded to erode yet.
Njoo na maconfidence. Carry that image of the US with you. You are a winner my friend.
Karibu sana.