Naomba ushauri wenu wana JF





upo sahihi kabisa dena 100%,
siyo rahisi kabisa kukubali kirahisi hivyo,wengi wanakubali baada ya kushauriwa na sana na washauri nasaha hosp,wanasaikolojia tena kwa muda wa kutosha na maelezo ya kutosha.
Lakin labda ni mwanaume mwelewa na anampenda sana mkewe,
ila ni vizuri sana wakienda bega kwa bega hosp,wakapima na kupata majibu kwa pamoja ili hata mwanamke ajihakikishie kwa macho yake kuwa kweli mumewe hajaathirika,na ni kweli anampenda anasimama na kuwa naye pamoja hata kwenye hiki cha changamoto kwake kiafya.
 


Nakwambia kuna mmoja tuliwahi kumpima (alikuwa taxi driver) alitoka angaza magomeni kwa miguu mbio mpaka kwao msasani kaacha gari pale hosipital na hiyo ni baada ya yeye kuwa negative mwanamke positive alikimbia hata kumshika wala kuongozana nae hataki.

Hizo kesi ninazo nyingi sasa huyu akisema hivi tu nishamsoma tayari wewe heehe nakwambia hivi sikiaga tu kwa watu si yakufike..............

Hii kitu ngumu bana wewe eti akubali kilaini tu hivyo........................labda ana moyo wa chuma mwenzetu
 


kumbe wewe ni mshauri, sijui wa ANGAZA? utakuwa umeshauri ya maana
 


Ha ha ha ha ha labda mwaya! hapo kwenye red nimepapenda.....
LAKIN labda ni kweli mume wake ni negative............
Duniani tumetofautiana kitabia na jinsi ya kupokea jambo/taarifa liwe la furaha au huzuni.
 

pole sana kwa yaliyokukuta dada,
hiyo ni sehemu ya maisha tu, ningependa kukwambia kuwa kwa maisha haya ya sasa,
watu wengi tu kwenye ndoa wanaishi katika hali hiyo,
unakuta baba au mama mmoja wapo ni mgonjwa,
na maisha yanasonga kama kawaida,
usihofu, huyo ni mumeo na kumbuka kuwa
utaishi nae katika raha, shida, magonjwa na kila aina ya mapito!
Ni vema kwakuwa yeye hata baada ya kugundua kuwa wewe umeathirika,
basi amependa muendelee pamoja,
"what husband"
Tena ukithubutu kumwacha na kwenda kuishi kivyako basi na mungu anaweza akakupa adhabu mbaya sana,
wewe ni mtu unaehitaji faraj, upendo na ukaribu kutoka kwa mumeo!
hebu tulia muendelee kuwakuza hao watoto!
Mungu awape nguvu!
 
Karibu Tuzungumze bali nimehama kituo kwa sasa ukitaka details ni PM

Huo ukaribisho ni mzuri sana,
lakin Dena kuja kituoni kupima si tatizo gumu sana,
ugumu unakuja pale kwenye kupokea majibu,
Mshauri anapoanza kuonesha bahasha ndiyo mtu unaona mapigo ya moyo kama,
yanataka kutoka na kijasho chembamba kinaanza kutoka hata kama humo hosp,
kuna AC ya kutosha......na ndiyo maana kipengele cha kupokea majibu wengi ni tatizo sana bila elimu ya kutosha toka kwa mshauri nasaha basi majibu mengi yataachwa vituoni......lol
 
It seems wewe ndo umeutoa huko ulikoutoa. Pole sana sana!! ingawa stori yako inashangza kidodo, ulikuwa ukitumia kondumu ulikuwa ukimweleza nini mumeo? kuwa unazuia nini? hakushangaa au ni kawaida yenu? kama yeye amekubali mshukuru Mungu, basi muishi kama atakavyo ila usimuambukize.
 
BARAKA POKEA HUO USHAURI.WA KUPIMA PAMOJA Watu wengine wanaogopa sana sero + status.anaweza kusema uongo tu aonekana yu salama. Ukweli ubainike. Hata PMTCT inatakiwa baba na mama kwa pamoja. Sio kwamba napingana sana hapana. Hii kitu sikia kwa mtu. Watu wanaogopa hata kuchukua dry ration kwa afya zao, wanakana status zao.
 


Bado kuna maswali, sasa umeishi na mumeo kwa muda wa miaka 13 na sasa umekuja kugundua hivyo sasa wewe umeutoa wapi??Na iweje mumeo asiwe nao??Nadhani hiyo ni impossible zaidi fata ushauri wa member wengine kwamba mchukue muende mkapime pamoja na muangalie..Pole sana!
 

Usihukumu usije ukahukumiwa........................
 

Katika maswali mabaya wakati wa kupima ni hili.....................................
 

Mengi tu yapo yameachwa.............................
 
thanks, ila sijui utanikonvisi vipi nikapime..nikiwa tayari nitakutafuta

Mpendwa nimecheka kweli asubuhi ya leo eti sijui ataniconvisi vipi nikapime. Kama anavyosema dena jamani kupima kwataka moyo lol, na sio rahisi mume ajue we unao ye hana akubali kirahisi rahisi hivyo, hawa wenzetu akikufumania tu ni kasheshe haya asikie umeukwaa huko si balaa.

Dena kama ndio wapimaga watu nyie watu wa ushauri nasaha mnajua kututisha, Mi nikienda kupima nawaambiaga naomba msinipe ushauri nasaha nipimeni na nipeni tu majibu. pengine umekutwa positive lakini mshauri ataanza bwana ooh unajua ukimwi this, ukimwi that mpaka jasho linakuchuruzika akimaliza ndio anakwambia hongera uko positive kha! hapo moyo karibu uachane na mwili.
 
duuh!!! ni asilimia 1/100 ya wanaume kama wako, kama ni kweli hajapata maambukizo nabado anataka muendelee kuishi pamoja.

binafsi sina cha kusema kwa kuwa yameshasemwa mengi.
 
Pole baraka,yote maisha

ila mi namsupport Dena
huyo mumeo inaelekea ni muongo hajapima au kapima nae kakutwa nao
ila hataki kuamini ndo mana kasema musiachane..ili muendelee kuuguzana
duuh!!inatatanisha though
 
Nashukuru sana wote kwa ushauri wenu, ila mimi wasiwasi wangu ni kuwa je ni kweli anamaanisha anachokisema?
Maana kwa jinsi ninavyomuelewa anaweza kusema hivyo lakini bado hajawa na maamuzi kamili. Na wasiwasi wangu umenidhihirishia baada ya sasa kuanza vituko,
Mfano jumamosi nilimuuliza kama ataenda na watoto kumuona babu yao anaeumwa akasema hajajua, baada ya mimi kuondoka kwenda kazini alikwenda nao na akawaacha walale huko bila kunitaarifu, na hapo yule mtoto wa kwetu wote naumwa na kuna dawa anatumia na ameziacha nyumbani, baada ya mimi kurudi nyumbani na kugundua kuwa mtoto hatarudi na dawa ameziacha nikampigia kumuuliza sasa tunafanyaje maana dose itaharibika, akasema subiri nakuja tena kwa hasira, na aliporudi alikuwa kimya wala hakulizungumzia na likuwa amelewa, asubuhi pia akawa kimya, sasa ni visa tu na juzi amempeleka mtoto kwa aunt yake bila mimi kujua pia mpaka leo hajarudi, yaani kama mtu mwenye bifu fulani hivi na maelewano hakuna, na jana amelala kwenye chumba cha watoto.

Hio ndioo hali halisi ndugu zangu haya naendelea kusikiliza ushauri wenu.
 
Huyo mumeo baraka ni muathirika kabla hata wewe hujaenda kupima akakaa kimya kwa sababu yeye ni msiri. Anakubali kuishi na wewe kwa sababu naye ni muathirika. Ambataneni kama Mungu alivyosema, mmekuwa mwili mmoja na binadamu asiwatenganishe.

Nakupa pongezi kwa kuwa jasiri, shupabu kwenye hili swala, siyo rahisi sana kama unavyofikiri bila uweza wa mwenyezi Mungu usingekuwa na ujasiri wa kueleza kinachokusibu. Simama katika Imani ukimtumainia Mungu kukupa nguvu za kulea mtoto wenu mkimwandaa kwa maisha yake yake binafsi ya baadae.

Jitahidi sana kumuelekeza kila kitu, ukimtumainisha kwa kusoma vitabu vya mwenyezi Mungu (Biblia, Korani), mfanye viwe kiongozi wa maisha yake.

Nawatakia kila kheri. AMEN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…