Naomba ushauri wakuu

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
2,295
Reaction score
5,458
Habari za wakati huu wakuu.

Nahisi nitazeeka kama si kufa bila kutumia usafiri wa anga na wa majini.

Sijui ni kitu gani kimenikuta ila hiyo aina ya usafiri sijawahi kupanda na wala sifikirii kama ipo siku nitakuja kupanda maana nafsi yangu inahisi kama vile siku nikipanda nitakufa kabisa.

Siku moja mwaka 2002 nilipanda pantoni pale kivukoni kuelekea kule kigamboni ilipofika katikati kuna boat ya azam ilikatiza sasa ilileta mawimbi kiasi fulani ikapelekea ile pantoni ianze kuyumba mpaka watu wakaanza kupiga makelele kama vile boat inataka kuzama.

Ila kwa upande wa ndege ndio sijawahi kabisa mara kwa mara kuna jamaa yangu yupo France huwa ananialika niende kutembea kule lakini naogopa sana kupanda ndege wakuu hata mambo ya biashara zangu huwa kuna business partner wangu ndio anasafiri kwa ajili ya kufuata wateja wa nje ya nchi yaani nipo kama JPM vile ila fadahli hata yeye hapo Zanzibar au Chattle huwa anapanda ndege.

Hivi nifanyaje ili niweze kuondokana na hii hofu ya kutumia hivi vyombo wakuu.
 
Unatakiwa umuone pyschopathologist akusaidia tatzo lako....hii n mental problems,kitaalamu inajumuishwa kwenye kundi LA magonjwa ya akili yaitwayo "specific phobias" yaan hofu ya kitu fln...wapo wanaoogopa elevators,wapo wanaoogopa watu wengne so kama uko DSM nenda muhimbili ,muone psychotherapist ,tatzo lako litaisha ...
 
uliwazalo ndilo litatokea, mimi nilikuwa naogopa sana bunduki lakini siku moja nikajikuta nipo sehemu ambayo kila mtu anamiliki za kutosha tu,..muda wa kulala ukifika utaona tu angani vitu vinapita na milio ya kutosha unaambiwa sasa ndio saa ya kulala
 
.,CHUNGU LAKINI DAWA,,jitahidi kupanda utazoea mkuu,,,
 
Usipate tabu onana na sangoma uliyejirani naye ndani ya dakika 2 tu utajikuta umetua ufaransa kwa rafiki yako pasipokutoa hata senti moja.
 
Ni uoga tu mkuu.

Ila mara zote kwenye huo uoga ndio unahisi kama vile utakufa.
Usiogope Mkuu kifo hukuja hata kitandani mkuu lakin pia huenda ni tatizo la kisaikolojia so jitahdi kutafuta msaada haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…