Naomba ushauri wako rafiki....

Naamini umenipata vyema!
Maswali mengi yaligonga kichwani mwangu na sijapata majibu!

Je huyo binti alitaka na mimi nilianzishe kwake?
Je! kuna mtu anataka kuharibu ndoa yangu kwa uzushi huo?
Je! ni kweli mke wangu anatembea na huyo bwana?


hahahhahahhahah! watoto wa mujini bana kaaaz kweli kweli.
uspate hofu na mkeo wala hakucheat ila hiyo ni stail ya mjini kwamba BORA TUKOSE SOTE KWA NINI BANA??
tena kama unajitahd kutoka na mkeo, ukampiga pamba akanoga, home kwako amani full mkeo tabasamu kila uchwao basi jua VIJOKA VYA MDIMU HAVIKOSEKANI, yaani wao ingawa hawali ndimu lkn sharti na mchumaji asiile. hawa ni ndo MAFISADI KIWEMBE, kutwa kuchwa kufisadisha penzi la wenzao.

my take: ongea na mkeo mpe caution kwamba anawindwa and that kama anamarafiki ambao hawaaminiki awapotezee, istoshe mwambie asigombane na watu kama ni mtu mgomvi. abadilishe saluni anakotengeneza nywele na eneo analopenda kutoka kupata moja baridi.
 
jenga ukaribu na huyo dada ili upate taarifa zaidi, usianze kuhisi eti na yeye anakutaka, pia huyo mkeo wewe unamuonaje? pia ulimpataje? kama hajatulia utajua tu haihitaji king'amuzi, nb.mke mwema anapatikana kwa Bwana.
kwa taarifa yako mwanamke ambaye anacukuliwa mumewe na mwanamke mwingine hana courage hata ya kumsogelea mume wa huyo mwanamke kumwambia. yaani akimjua mwaamke watatukanana wao wenyewe but hawez kuake trouble kumtafuta huyo mwanaume kisha akaja eti smjui ila nataka kumwambia kitu.

funguka akili hii hapa mjini inaitwa staili ya FISADI PAPA'' msome mzee Yusufu utamuelewa.huu ni mchezo a unachezwa na watu kati ya hawa, ndugu wa mume(dada+mma mkwe ) kama hawampendi mkewe, mashoga wa bishomvu kia anawaringia na mumewe, majirani wao na mwanamke anayemtaka huyu mume ( yaani @tutoe b)
 
Hivi mtu humjui tu akukurupukie eti mkeo amuache mume wangu!!
'
Kama ni mimi naambiwa eti mke wangu anafanya ufedhuli huu wala siwazi
'
Ningemwambia tu huyo mwanamke nimesikia halafu aende!
'
Kwanza amejuaje niko pale?
'
Huyo aliyemuambia kwenye meza ile kuna fulani ni nani?
'
Amenijuaje?
'
Mambo mengine kuyapa nafasi ni kujisumbua tu!
 
dah! Unamoyo waujasiri sana Lisa Mungu akusaidie mumeo asije akatoka nje tena coz i know how it hurts.
Niliumia sana nipokuta ni kweli,nililia sana , maana sikuamini kabisa kama angeweza kufanya hilo. Ila nimemsamehe na nampenda Mumewangu ndiyo maana bado tupo .
 

Duh! hii nayo kali, sasa mama yake alikubali vipi umchukue mtoto wake wakati yeye yupo? Ulitumia lugha ipi hadi mke mwenzako akakuamini?
 

Darubini kali mkuu; hata wale niliokuwa nao mmojawao alinambia hivyohivyo! Ahsante sana kwa mawazo yako mazuri sana.
 

Kwa kweli sikuwa na maswali zaidi ya kumuomba namba yake yasimu na ya mume mtuhumiwa! Ila kwa sasa sijisikii kufuatilia kwani nahisi kama ni mchezo wa kupangwa ili amani nyumbani kwangu itoweke!
Na nisipofuatilia nahisi alo-enginer huo mpango itam-pain zaidi.
 
Piga kimya, fanya uchunguzi kwanza, kama kweli anatemea na mume wa huyo dada.
Ukitoka hapo kapime,hiv, kabla haujafanya uamuzi mwingine
Ahsante sana kwa ushauri wako Somoe
 

Duh! sasa Dada Mzuri umekuja kivingine; kama nimeishawabumburua nifanyeje? Umeliangalia suala hili kwa mapana sana; ushauri hujanipa lakini. Nakushukuru na ninaaamini utanipa ushauri nifanyeje ili niweze kubaini ukweli uko wapi.

Na je nikigundua kwamba huyo mdada alichokiongea ni kweli; huoni kwamba ndoa yangu itasambaratika?
Watoto wangu wataishije kwa kulelewa na mzazi mmoja?
 

Nimekupata vyema tena sana! Ubarikiwe kwa busara zako.
 

Nimekupata vyema rafiki mwema. Ahsante.
 
Ahsante sana kiongozi!
 

Ahsante sana!
 
Duh! hii nayo kali, sasa mama yake alikubali vipi umchukue mtoto wake wakati yeye yupo? Ulitumia lugha ipi hadi mke mwenzako akakuamini?
Mimi nilijidai mume wangu kanituma pale nikamtizame mtoto, kuwa ni damu yetu, akaniuliza jina nikamtajia la wifi yangu ambaye tulikuwa naye, basi yule dada akampigia mume wangu kumuuliza kama anamfahamu, akaambiwa ni kweli, basi akawa huru kuongea na sisi na tukamchimba akasema yooote kwa kujua sisi wote ni wifi zake. baada ya siku tukaenda sasa kumchukua ili akashinde home ndiyo ikawa moja kwa moja.wakamalizana huko wenyewe. anaruhusa ya kuja kumsalimia .Ila kwa sasa yule dada ananiheshimu sana.
 

Hakika we ni Kamanda; nimekukubali!
 
Fuatilia ndugu usione shida . Hii itakusaidia kuujua ukweli na pia utajua kwanini yote hayo yanafanyika then utawasaidia wengine watakaopatwa na mkasa kama wako. Usiogope , ukiujua ukweli utakuweka huru even in future hautatumia hili tukio kama reference endapo utamkuta mkeo na kosa la jinsi hii otherwise utageneralize tu na kusema ndio maana kipindi fulani ulisemwa hivi , wakati huenda tukio unalo refer halikua la kweli.
 
Hizi tetesi ulizisikia toka kwa nani? kwa mke wako au?
 
wengi huwa mnakosea mtu akikutonya hivi sio unaenda eti mnywesha mtu pombe aongee kumbuka mtu mwizi huwa mjanja na hata kama iweje mwizi na mjanja huwa hawakubali labda uwakamate papo hapo katika tendo.

Hata uwakamate hapo, bado hawatakubali.
 
Hizi tetesi ulizisikia toka kwa nani? kwa mke wako au?

Kuna mwanamke tunaheshimiana sana kwa sababu nilimsaidia mme wake kupata kazi nzuri. Majirani wakaanza kumwambia mme wa huyo mwanamke kwamba nina mahusiano naye ya kimwili. Uvumi huo uliposhindikana (kwa kuwa mume wa huyo mwanamke tulikuwa tunaheshimiana sana) ndo wakamwambia huyo mwanamke kuwa tunajifanya wajanja sasa wataamia upande wa pili (wakimaanisha kwangu). Sijui nimeeleweka au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…