Naomba ushauri wa kupata matibabu ya meno

Mundamushimu

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
752
432
Habari wana jf Doctor,

Mimi nina umri wa miaka ....... nina nina mke mmoja watoto 3 na wajukuu 4. Tangu mwaka 2014 nimeanza kusumbuliwa na meno yakaanza kuuma, mpaka 2015 mwezi wa 8 tayari yalikuwa yameng'olewa meno 6. Nikaamua kwenda kupata matibabu zaidi Nkinga Hospital iliyopo mkoa wa Tabora.

Huko meno yalisafishwa yote na kupewa dawa ambazo mwa kiasi fulani zilisaidia. Baadaye likaanza tatizo la kutoa harufu mbaya kinywani, mimi mwenyewe nilijisikia vibaya sana pamoja na usafi wa kuyasafisha meno mara 3 kwa siku kwa dawa za meno. Nilijihisi mpweke kwani nilishindwa kuongea karibu na wenzangu na mke wangu ni kama alinitenga naye alikuwa analala mzungu 4.

Nikaamua kurudi tena Nkinga Hospital, nikapatiwa dawa za kunywa na kusafisha Kunywa. Nashukuru Mungu kinywa kikaacha kutoa harufu. Tatizo ambalo limenipata tena 2017 mwezi wa 6 meno yalianza kulegea pasipo maumivu yoyote, yakapoteza mpangilio kinywani yakawa hovyo hovyo tu na sasa siwezi kutafuna vitu vigumu, kwa kukosa mpangilio nimekuwa naung'ata ulimi mara kwa mara nimeenda mpaka Buhando Hospital lakini dawa ninazopewa hazinisaidii.

Naomba kupitia jukwaa hili kama yupo anayejua dawa anielekeze maana ni mateso kinywa hakitoi harufu tena ila meno yamelegea yote. Asanteni.
 
Kama inawezekana nenda Muhimbili utaweza kupata tiba na kurekebishwa huo mpangilio wa meno
 
Lucas Sabuni. Kwa umri wako (Maana umesema unawajukuu, lazima utakuwa above 40+, ), na kwa hosp ulizopitia, nakushauri usiendelee kupoteza muda. Nenda Muhimbili kitengo cha meno moja kwa moja, ila nakushauri uwe na Bima ya Matibabu, hasa NHIF
 
Habari wana jamvi?daktari mimi meno yanauma upande wa kulia tu na ni ucku tu sasa hapa kwakweli napata shida ninacku kama ya 3 hivi,naomba msaada
 
Habari wana jamvi?daktari mimi meno yanauma upande wa kulia tu na ni ucku tu sasa hapa kwakweli napata shida ninacku kama ya 3 hivi,naomba msaada
Hakuna daktari humu mkuu, nenda hospital.
Huu uzi ni mtu alikuwa anaelezea matatizo yake ya meno naye pia ameshauriwa aende Hospital
 
Mkuu dawa ipo gharana yake ni Elfu 15 TU hutang'oa meno Tena hata Kama yangekuwa yanatoa damu au usaha yangepona na hayata Uma Tena.
 
Back
Top Bottom