Ukifanya risk management na kupata discipline hapo unamaliza kila kitu. Wafanyabiashara wengi tu sio waaminifu kwa asili ila wanalazimika kuwa waaminifu kwa sababu ndio msingi wa biashara, usipoweza hili basi kajisalimishe Kyela kulima mpunga.
Mikopo unakopa ili iweje? Ni mzigo kwa biashara kukopa mkopo ili ule maisha alafu huo mkopo uulipe kwa faida inayotokana na biashara. Kopa ili uendeleze biashara, au ukiwa na emergency ambayo usipoikamilisha kwa fedha itaathiri uwezo wako wa kufanya biashara. Mfano kufanya upasuaji.
Pendelea kutumia sehemu ya faida pekee kama njia ya kukuza biashara kama huna uwezo mzuri wa kukabiliana na mikopo. Hii ni njia ndefu ya watu 'dhaifu' kama wewe. Kulingana na biashara yako inavolipa faida unaweza ifanya kama hivi mfano 50/30/20. Kwamba 50 unazungusha kwenye biashara kama inventory na running costs, 30 ni matumizi yako (reward), 20 ni savings kwa kukuza biashara baada ya kila miezi 6 maybe.
Naotea biashara zako zinakufa kwa sababu hujui stages za trade cycle ya hizo biashara.
Hujui 1. introduction (moderate sales) 2. growth (high sales & high profit) 3. maturity (entry of competitors, moderate sales) 4. decline (low sales, hasara inaanza).
Nafikiri wewe ukifika stage ya 3 unaanza kuvuruga unabaki na matumizi ya juu kama ya stage ya 2. Ukifika stage ya 4 unakopa ili uweke mambo sawa. Alafu you should be PROACTIVE, sio unaanza kupata changamoto ndio unatafuta suruhisho. Kwa nini biashara zako tofauti zife na zilikuwa kwenye faida. Ukitumia akili changamoto nyingi unaziona kabla hazijaja na unajipanga kuzikabili.
Mwisho, nimetoa general assumptions kwa vile haujawa specific ila naamini ukichezea humu unapenya.
NB: Nimejibu kulingana na madesa, mlioko field mniambie hizi mambo zipo au naingizwa chaka.