tunasongaMbele
Member
- Apr 1, 2021
- 57
- 51
Poleni na majukumu ndugu zangu,
Nianze Kwa kumshukuru Mungu muumba wa mbingu,nchi na vilivyomo. Kuna habari njema nimeipokea ila imekua na walakini Kwa moja ya washauri wangu,Kwa muda sasa yapata miaka miwili nimekuwa natafuta kazi/ajira na sikuweza kufanikiwa kupata kazi ya matamanio yangu ila nimeishia kupata kazi za kinyonyaji mno Hadi Leo hii mwenyezi Mungu kaniona.
Leo asubuhi nimepata email kutoka kwenye kampuni ya SHELL yenye makao makuu mjini London Uingereza kabla ya barua ya Leo (employment offer) nilipokea tena barua ya kukubaliwa ombi la kazi(kumbuka kwenye tangazo la kazi ilikua ni graduate training program and employment) mnamo December 30,2021 iliyonitaka nijaze taarifa zangu baadhi kama leseni ya udereva na vinginevyo,na badae niliisaini na kuituma kabla ya saa 48 zao kuisha na nilifanyia hivo.
Hivyo basi ninavyoandika hapa Leo nimepokea form ya ajira na taarifa zote za ajira yangu nikatakiwa niisaini Kwa mkono then Nii submit na nimefanya hivo pia,,form hiyo imeelekeza natakiwa kuwa na visa ya kusafiria ndani ya siku 14 kabla hawajanitumia ticket ya Ndege kwenda kuanza kazi mnamo mwezi wa pili mwishoni na aina ya kazi ni ya mkataba wa miaka mitatu.
Hivo basi kabla sijaanza harakati za kutafuta passport na visa imebidi nipite Hulu mnishauri kitu Kwa kuwa kuna ndugu mmoja kashanitia wasiwasi ya kwamba hawa ni matapeli wakati huo mimi niliomba kazi kupitia official website yao ya shell.
Nimeenda ubalozi wa UK mchana huu nikaambiwa nifatilie na kujidhihirisha juu ya hii kazi na kitu kibaya zaidi aliyenijibu hivi ni mlinzi Kwa kuwa kasema kuna wengine wameenda kuulizia ila wamejibiwa wapitie mtandaoni wajidhihirishe kwanza hivo kutokana na majibu hayo wamenipunguzia asilimia na ari ya kupambana.
Naomba Kwa ambaye ashawahi kuomba kazi Kwa hawa watu wa Shell Oil Exploration and production UK anipe ushuhuda kabla sijaanza kupambania passport na visa.Jamani naombeni ushauri na maelezo zaidi,,soko la ajira ni gumu Sana Kwa sasa tanzania
#asanteni
Nimeweka barua niliyotumiwa hapo chini