Naomba ushauri kuhusu kukopa benki

M.Rutabo

Senior Member
Apr 8, 2015
161
433
Naomba ushauri nafahamu jamii forum ina wajuvi wengi. Mm nikijana miaka 30 nimejiajiri kwa kuwa na duka la nguo nimejenga na nyumba ina hati japo nipo huku wilayani.

Sasa nina shamba langu la migomba nilitaka na lenyewe nilichukulie hati ili niweze kukopa kwa kutumia hati ya nyumba kuweza kuanzisha biashara nyingine.

Wasiwasi wangu manzingira ya biashara kwa sasa nchini sio mazuri sana. Ndio maana nikaomba ushauri kwamba kwa mfano nimekopa kwa kutumia hati ya nyumba lakini katika kurejesha mkopo nikakwama siwezi kutumia biashara mpya niliyofungua kwa kutumia huo mkopo na hati ya shamba ninayotaka kufuatilia ili niweze kupewa mkopo na benki nyingine tofauti nilipe ule mkopo wa nyuma kwenye benki nyingine huku biashara ikiwa inaendelea nikishamaliza kulipa nawakopa tena kisha nalipa mkopo wa ile benki nyingine?
 
Aisee Nakushauri usikope.

Hujawa tayari. Jifunze kwanza namna ya kutumia mikopo.

Kama nia ni kufungua biashara mpya, ningependekeza utumie FAIDA inayopatikana kutoka kwenye biashara ya kwanza
 
Mkuu usijaribu kabisa kufanya hiyo bahati nasibu..utajuta...kama biashara inafanya vizuri ni bora ukatumia faida kufungua biashara nyingine...Mkopo haujawahi kumuacha mtu salama....Mimi ni mwajiriwa wa benki so nafahamu haya mambo............

Ovaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkopo ni 'suicides missions' hasa kwa awamu hii ya 5

kuna Uzi umeanzishwa unasema "umuhimu wa kuwa na Mentor" hasa katika biashara

ufuatilie utakusaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
My take, usikope kwa lengo la kuanzisha biashara mpya, rejesho litakutesa sana coz it takes time to break even for a new business

Ila kopa kuendeleza/kupanua profitable business iliyokuwepo tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikopo ya mabenki kwa sasa si vizuri kutumia vitu kama nyumba au mashamba..hali ya biashara si nzuri sana. Wenye unafuu wa kukopa kwa sasa ni watumishi wa umma ambao mikopo inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao lakini sisi wa marejesho ni pasua kichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usijaribu kabisa kufanya hiyo bahati nasibu..utajuta...kama biashara inafanya vizuri ni bora ukatumia faida kufungua biashara nyingine...Mkopo haujawahi kumuacha mtu salama....Mimi ni mwajiriwa wa benki so nafahamu haya mambo............

Ovaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
kitaulo kila sku unashnda kulr kwny uzi wa "kula 2nda kimasihara" imekuwaje ukapata mda wa kukaa iffisini???

just joking

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom