Naomba ushauri kabla ya ndoa

Spaghetti

Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
78
Reaction score
7,575
Habari wana JF,

Nimekua kwenye mahusiano tangu mwaka 2014 na binti mmoja na nikabahatika kupata mtoto wa kiume 2015 mwishoni.

Alipata kazi mkoani mbali na ninapokaa. Tatizo kubwa kati yetu imekua ni mawasiliano kwa upande wa mwenzangu, japo najitahidi kumuunganisha na vifurushi, ni nadra sana kwa yeye kunitafuta au kunijulia hali.

Kuna siku niliugua mpaka kulazwa na mpaka natoka sijapata simu yake hata moja. Sasa nimekua na wasiwasi mkubwa hivi kweli ananopenda au lah maana hata yale mahaba tu yakuitwa baby, hny, mume, sikumbuki mara ya mwisho yalikua lini.

Ukimuuliza unanipenda jibu linatoka kwa shida na kisingizio kikubwa kwake ni kazi zimembana. Nikifananisha na mahusiano ya nyuma yote niliyopitia wanawake wana affection kubwa sana kwa wapenzi wao but hii imekua kinyume chake. Kitu ambacho sipendi; ni mwanangu kuwa na malezi ya pande moja kama mimi nilivyolelewa lakini hali halisi ndo kama ivyo.


Naomba ushauri wenu, nifanyeje kabla sijafunga nae ndoa.

Karibuni.
 
Maswahibu tumeumbiwa wanadamu....pole sana ila huyo amepata mwingine na wala usihangaike kulazimisha upendo...weka akili yako kwa mwanao na ujipanga upya
 
Sijaelewa hapo mwishoni tafadhali......
Ni kwamba utalazimika kumuoa tu sababu mmezaa nae mtoto?? Usithubutu rafiki
 
Unauliza Mkyundu wa mbuzi wakati mkia unauona?
 
Sasa wewe unaulizaa nin hapoo????? Achagaa ufalaa mzee...
 
Uwepo wa mtoto na umbali unaweza kuwa sababu ingawa haihalalishi ukimya. Hata wanandoa wanaoishi pamoja hufikia mahali pa mahaba kupoa lakini wanasonga mbele kutokana na ndoa zao kusimamishwa na vitu vingine vya msingi pia. Mawasiliano ni muhimu sana hasa kwa wenza wanaoishi mbali lakini sikushauri kukurupuka. Labda mahasidi wamemwambia umepata mwingine kwa hiyo amenuna, au kapata mwingine kweli. Tafuta muda umpandie huko huko aliko ujue mbivu na mbichi.

Wanaodogosha umuhimu wa mtoto kupata malezi ya wazazi wote wanaweza kuwa sahihi kwa sababu zao lakini wewe ni utu na upendo unaokusuma kumuwazia mwanao mema. Na upendo wa kweli ni kujikana kwa ajili ya mwi/wengine. Waza kumwacha huyo mzazi mwenzio kama atakwambia hataki kufunga ndoa na wewe au kama atakataa kuzungumizia hii hali iliyopo kati yenu na kama utaona kama kweli kuwa pamoja kutaathiri makuzi ya mtoto wenu.
 
Na kwa kuongezea, usifananishe wanawake. Sio kila mwanamke anaonyesha mahaba kama hao wa kwako wa nyuma. Kila mtu ana jinsi yake ya kuonyesha upendo na kupokea upendo. Kasheshe ni pale mnapotofautiana. Sasa kama wewe unapenda na ulizoea kuitwaitwa bebi lazima uwe na wakati mgumu. Pia ukimuuliza kama anakupenda akikujibu kwa shida haimaanishi moja kwa moja kuwa hakupendi. Inawezekana anaona kama unauliza wagonjwa hospitali. Unaonyesha dalili za kutokujiamini au kutomwamini. Kwa ufupi bado una safari ndefu ya kufahamu mahusiano ya binadamu wa jinsi ya ke na me. Pia kama ulilelewa na mzazi mmoja ulitakiwa uwe umekata mnyororo mapema lakini umeshtuka baada ya kuunganisha mnyororo. Hujachelewa sana.
 
kwanza usiaze ndoa maana huja comfirm hata kwake...
inaonesha una harusinate mwenyewe ...
ndoa ni wawil kuijenga ila hapo kwa sasa upo mwenyewe...
huyo kapata mwingine , mwanamke single mother anahitaj attention sana...maana anahis ana mzigo..wa kuwa na mtoto kumbania kukosa dyudyu ovyo..sasa wewe upo mbali nae ,,unategemea nini kwa mfano..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…