Naomba ufafanuzi wa "Usipochukua mshahara benki unarudi hazina"

Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
3,169
6,515
CAG amesema hayo wakati akiwasirisha ripoti yake.

Je, alikuwa na maana gani aliposema "mabenki hayarudishi pesa hazina"?

nawasilisha.
 
Mshahara ni haki ya mtu aliyefanya kazi na akalipwa hapangiwi lini autoe kwenye Bank account yake wala jinsi ya kuutumia.
 
Ngoja nitarudi tena kusoma soma comments za wenzangu maana kichwa cha taarifa na maelezo vimenichanganya
 
CAG amesema hayo wakati akiwasirisha ripoti yake.

Je, alikuwa na maana gani aliposema "mabenki hayarudishi pesa hazina"?

nawasilisha.
Siku nyingine usirudie kuweka vitu nusunusu hapa, weka habari kamili. Unaona sasa tumekutukana bure kumbe hicho ulichokuwa unahoji kimo kwenye ripoti ya CAG!! Hiki hapa chini!!

"Mishahara kwa kawaida isipochokuliwa benki inaitwa unclaimed salaries na inatakiwa kurejeshwa hazina lakini tumefatilia hairejeshwi na mabenki".
 
Sijaisoma wala kuisikiliza hiyo taarifa. Ila nafikiri wanamaanisha pesa zikitumwa benki kama mshahara wa mwajiriwa na kukawa na tatizo kwa namna moja ama nyingine, hizo pesa hazirudishwi hazina.

Mfano, kama mfanya kazi alifariki au ameacha kazi au ni hewa, ki utaratibu hizo pesa zinatakiwa zirudishwe hazina zisibaki benki kwa sababu lengo ilikua kulipa mshahara.
 
I agree with u, mi binafsi nimeangalia kwenye TV hasubui Leo Azam two nimeiyelewa hivyo
 
Hiyo iko hivi, Halmashauri mtumishi anapokuwa na matatizo ya kusababisha asipewe mshahara wanachofanya hawamuondoi Mtumishi kwenye payroll mara moja lakini wanawaandikia benki barua ya kutomuingizia Mtumishi husika mshahara.

Hivyo hazina watapeleka benki mshahara wa Mtumishi X,huo mshahara ukifika kabla ya kuwekwa kwenye akaunti ya Mtumishi husika benki wanakutana na barua ya kutoka Ofisini kwake kwamba mwezi huu huyu mtumishi X hastahili kupata mshahara,hivyo benki hawaweki fedha hizo kwenye akaunti husika wanakaa nazo.

Fedha hizo ambazo halmashauri mbalimbali ilizizuia benki zisiingizwe kwenye akaunti za watumishi ilitakiwa zirudishwe hazina lakini benki hawafanyi hivyo(Wanakaanazo tu).
 
Back
Top Bottom