NAOMBA UFAFANUZI: Torch za kupima mwendokasi wa gari

Nukta5

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,180
1,276
Jana niliomba gari kwa jamaa angu kuna mishe nilikua nafuatilia nje kidogo ya mji sasa toka mjini hadi ukute kibao cha kuruhusu kutembea zaidi ya 50 ni kama 20+km na kote nilitembea kama sheria za barabaran zinavyotaka. Sasa nilivyokikuta kibao cha kuruhusu kama 2km mbele nikakutana na trafik wakanipiga mkono wakaniambia nimezidisha speed sehem ambayo sio wakanionyesha na picha sasa nikajaribu kumuuliza ni wapi hapo nimezidisha speed wananiambia hilo eneo ambalo ni kama 10km nyuma ndo nilipigwa torch nikabishana nao kwa kufupisha nikamalizana nao.

SWALI: Kwa nin unapokutwa na kosa usisimamishwe mbele kidogo ili iwe rahisi kutambua kosa lako maana nina uhakika 100% wanakupiga torch hapo panaporuhusu then wanakuambia sehemu waliyokupiga torch ni kama 10km nyuma ili uepukane na usumbufu wao na wao waijazie serikali fedha maana ingekua wanaonyesha video inakua rahis kutambua hilo.kosa ni muda gani na wapi lilipo hilo eneo tofauti wanavyopiga picha gari tu
 
We ulikubalije kosa pasipo ushahidi?

Swali hili ni sawa kama muulizaji ni mgeni na hizi tochi au kana ndiyo kawasili tokea sayari nyingine.

Pana ubabaishaji mkubwa sana kwenye hizi tochi. Haijulikani kwa nini hazipo jitihada za kuziondoa kero za wazi zinazoambatana na tochi hizi.

Si siri kuwa serikali hii inavuna uadui usiokuwa na haja wala tija kwenye hizi tochi aka tochi bambikizi.
 
Kifupi, umeibiwa na trafiki ili atimize hesabu ya bosi au ya mboga home!
 
A na B zote sawa
vibao vipo mbali sana unaeza ukaendesha ukahisi ushavuka kibao kumbe bado
lkn pia tochi sio za kuamini......
nlwah kukamatwa et nltembea speed 56 kwe 30 how come?

af wanakuja kistaarab kwel wanaomba lesen ukiwapa tuu wanakutolea picha af hawataki uwalipe mda ujao lasivyo hawakurudishii lesen

Chakufanya ni kua mwehu tuu au tafta bukubuku mpyaa ukisimamishwa unaikunjakunja af unamskisha mkononi(awaangaliagi ela wenyewe wanakurupuka kueka mfkoni tuu) then unatembea akija stuka ushasepa
 
Back
Top Bottom